Askofu Dkt. Philemon Mollel: Kuteuliwa kwa Makonda ni fursa kwa wakazi wa Arusha kutatuliwa kero zao

Askofu Dkt. Philemon Mollel: Kuteuliwa kwa Makonda ni fursa kwa wakazi wa Arusha kutatuliwa kero zao

Jaji Mfawidhi

JF-Expert Member
Joined
Feb 20, 2016
Posts
15,835
Reaction score
23,776
monaban.jpeg
xxxx.jpeg

Askofu Dkt. Philemon Mollel (Monaban) , ambaye pia ni kada wa CCM, mfadhili mkuu wa CCM Arusha, anayejiita mtu wa kiroho, wa Kanisa la Kilutheri Afrika Mashariki[Aliasi kutoka KKKT akafungua Kanisa lake la KKTA] amesema kitendo cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kumteua Paul Makonda kuwa Mkuu wa mkoa wa Arusha kinatoa mwangaza na fursa kwa wakazi wa mkoa huo wakiwemo kutoka vyama vya upinzani kupeleka matatizo yao yanayowakabili ili ayatafutie majawabu ya kina.

Wadau wamelaumu Jaji Mkuu Ibrahi Juma kukaa kimya kwa tabia ya Watu kujigeuza mahakama, ni kama vile ni wanyonge kwa huyu last born[Makonda].

Monaban ambaye pia ni Mfanyabiashara na mkazi wa Arusha amesema Makonda mara zote amekuwa na sifa za kipekee hasa linapokuja suala la kupigania haki ya mtu/watu kwa kuwa sio muoga na haitaji kufanya kazi kwa majungu

Amesema baada ya uteuzi wake kutangazwa wakazi wengi wa mkoa huo (Arusha) kutoka kwenye kada mbalimbali ikiwemo wafanyabiashara wameoneshwa kufurahishwa kwa kuwa wanaamini kero zao zitapatiwa ufumbuzi kwa haraka .

Aidha, Askofu huyo amesema wakazi wa mkoa huo si watu wanaoamini kwenye fitina na ugomvi bali ukweli na uwazi kwa kuwa wanataka kuishi kwa amani mara zote,Katika hatua nyingine Askofu Dkt. Mollel (Monaban) amesema viongozi wa Dini mkoani humo wamekubaliana kufanya maombi maalumu kwa ajili ya kumuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan na Mkuu mpya wa mkoa huo Paul Makonda ili pamoja nao na viongozi wengine watimize majukumu yao kwa kumtanguliza Mwenyezi Mungu.
 
Kero zipi?Makonda ana Bajeti? ana excutive power? Bajeti inasomwa Dodoma, sasa makonda ana influnce vipi hio Bajeti?

Changamoto za hii nchi sio kukosa wakuu wa mikoa wala wilaya bari ni serza za kiduwanzi za CCM.
 
Askofu Dkt. Philemon Mollel (Monaban) , ambaye pia ni kada wa CCM, mfadhili mkuu wa CCM Arusha, anayejiita mtu wa kiroho, wa Kanisa la Kilutheri Afrika Mashariki[Aliasi kutoka KKKT akafungua Kanisa lake la KKTA] amesema kitendo cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kumteua Paul Makonda kuwa Mkuu wa mkoa wa Arusha kinatoa mwangaza na fursa kwa wakazi wa mkoa huo wakiwemo kutoka vyama vya upinzani kupeleka matatizo yao yanayowakabili ili ayatafutie majawabu ya kina.
That reminds me of our proverb Which says that " An Elephant 🐘 that swims in coconut oil doesn't use ATM to buy meat from the pharmacy.🙂
 
Kero zipi?Makonda ana Bajeti? ana excutive power? Bajeti inasomwa Dodoma, sasa makonda ana influnce vipi hio Bajeti?

Changamoto za hii nchi sio kukosa wakuu wa mikoa wala wilaya bari ni serza za kiduwanzi za CCM.
Sasa ndio akili ya phD holder, jiulize UVCCM walioishia lasaba shule za kata, si ndio wanondoa kesi mahakamani wanampeleka Makonda jukwaani.
 
Back
Top Bottom