Askofu Emaus Mwamakula akamatwa na Polisi kwa kuhamasisha Maandamano ya kudai Katiba Mpya

Askofu Emaus Mwamakula akamatwa na Polisi kwa kuhamasisha Maandamano ya kudai Katiba Mpya

Mungu wa kweli, yaani Mungu wa Ibrahim, Mungu wa Isaka, Mungu wa Yakobo. Siyo yule Mungu wenu wa kuchonga aliyetangazwa na Lugola.
Wangekuwa wanamwamini huyo wangeomba tu Mungu mambo yakabadilika.Israel walitoka misri bila kurusha jiwe wala maandamano!!! Hawana nguvu yeyote ya KIroho wala MUNGU HAO
 
Mambosasa nakusalimia popote ulipo , Umezimika kama mshumaa jangwani

Ama Hakika Utukufu wa Mungu ni wa ajabu sana ! unasalimiwa na MO

RIP Akwilina
 
View attachment 1703071


View attachment 1703070



View attachment 1703379


====

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
KUKAMATWA KWA ASKOFU EMMAUS BANDEKILE MWAMAKULA
KWA KOSA LA KUHAMASISHA MAANDAMANO HARAMU

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Polisi Dar es Salaam leo tarehe 15.02.2021 limefanikiwa kumkamata anayejiita Askofu EMMAUS BANDEKILE MWAMAKULA wa kanisa la Uamsho la Moravian kwa kosa la kuhamasisha maandamano nchi nzima kwa njia ya ujumbe wa maneno katika mitandao ya kijamii. Taarifa ilikuwa ikihamasisha wananchi wajitokeze kwa wingi ili kuandamana wakishinikiza na kudai katiba mpya jambo ambalo ni kinyume na taratibu na sheria za nchi.

Aidha awali Jeshi la Polisi kupitia idara ya upelelezi kanda Maalum Dar es salaam walifanikiwa kupata taarifa hiyo na kumkamata Askofu huyo kwa ajili mahojiano kwa jambo hilo ambalo lilileta taharuki kwa umma katika mitandao ya kijamii.

Jeshi la Polisi linatoa onyo kwa yeyote ambaye ameshawishika na kupanga kuandamana kuahirisha mara moja nia hiyo ovu ambayo iko kinyume na sheria.

Pia ifahamike ni kosa kufanya maandamano bila kuwa na kibali cha Polisi ili kupewa ulinzi, na atakayejaribu kuandamana atashughulikiwa kwa mujibu wa sheria. Hivyo wananchi wote wa jiji la Dar es salaam waendelee na shughuli zao za kukuza uchumi na kujipatia vipato vyao vya kila siku.


LAZARO B. MAMBOSASA– SACP
KAMANDA WA POLISI KANDA MAALUM
DAR ES SALAM.
15.02.2021

Zaidi, soma:


Weldone. Hawa wachunaji wanatupotezea muda kwa kujiingiza kwenye siasa chini ya kisingizio cha neno la Bwana. Waunde vyama. Wavue majoho waonje joto ya jiwe wanayoonja akina Mbowe. Vinginevyo ni uonga wa kawaida unaotaka kuonyeshwa kama ushujaa.
 
Polisi waliomkamata Mwamakula kwa kuhamasisha Katiba mpya wanajisikiaje leo
 
Weldone. Hawa wachunaji wanatupotezea muda kwa kujiingiza kwenye siasa chini ya kisingizio cha neno la Bwana. Waunde vyama. Wavue majoho waonje joto ya jiwe wanayoonja akina Mbowe. Vinginevyo ni uonga wa kawaida unaotaka kuonyeshwa kama ushujaa.
Wewe mpumbavu unajisikiaje
 
Back
Top Bottom