Uchaguzi 2020 Askofu Gwajima: Naimudu Kawe. Mimi sio kilaza, nilienda Marekani mwaka jana na nimeshaandika vitabu 5 kwa kijapani, vipo Amazon

Hilo swali umewahi kumuuliza Mbowe lini atajenga ofisi ili muhame kwenye ile servant quarter?
Hakuna watu masikini kama wafuasi wa Gwajima; na bado li ligwajima linawakamua sadaka kila Jumapili.

Huko Birmingham Marekani sijui Japan sijui utopolo wa Boat za uvuvi , sijui treni na chuo cha uvuvi angeanza na waumini wake.

Gwajima Tapeli huyo hata kanisa ameshindwa kujenga huku anatembelea Hammer kwa sadaka za mazuzu wake.
 
Una maoni gani kwa CHADEMA ambao na wao licha ya kupokea ruzuku nono toka serikalini, kupokea michango ya lazima kwa wabunge wake na kutembeza bakuli kwa wanachama wake ila bado wameshindwa kujenga jengo la ofisi? Miaka kibao wapo kwenye servant quarter
 
Mimi nikiwa kama muumini wake napinga huyu baba askofu kugombea ubunge.

Baba, kwa nini usiboreshe mazingira ya kanisa kwanza. Tunashindwa hata kuwaleta marafiki zetu, aibu. Kanisa limekuwa kama banda la kuku. Unamuaibisha Mungu. Hizo ndege ungeuza uboreshe sehemu unayopatia riziki ya sadaka.
 
Hivi ni huyu huyu aliyesema hawezi kugombea Urais wala kuwa Waziri au Ubunge kwa kuwa akifanya hivyo atakuwa kajishusha, au mimi nimechanganya mkuu?
 
Atawaboreshe hizo madrasa!
Bwashee Gwajiboy anataka kutupeleka kwa mabeberu inakuwaje tunamkubalia tena? Yani atupeleke kwa mabeberu na mababeru yaje kwetu? Si yatamuhujumu Magufuli mzalendo wa kweli anayepingana na wanyonyaji mabeberu?
 
So wamchague yule aliyesema kugombea ubunge ni kujishusha cheo?
 
Kwani kugawa ambulance ni mpaka upelekwe bungeni au uwe mbunge!! 🙄🙄🙄🙄 sisi tunataka mwakilishi bungeni maamuzi ya kitaifa yanapofanyika, siyo mfadhili wa jimbo. Kawe siyo Morogoro wanapochagua matajiri wa kihindi na kiarabu wakawawakilishe bunge still wananchi wake ni miongoni mwa masikini kabisa na backward kielimu
 
Njia ya mwongo ni fupi sana.

Kama anatangazia watu kuwaanauwezo wa kuwaponya na anafufua misukule, Ambulance za nini tena? Si awaombee ili wagonjwa wapone?

kwanini anasuburi mpaka awe mbunge kama ana uwezo ? Kama ana nia ya kusaidia kwanini hajafanya hivyo siku za nyuma! Mbona Mengi alikuwa anasaidia shule bila kuwa mbunge!
 
Mimi ni mkazi wa Mbezi Beach toka mwaka 2008. Changamoto kubwa za jimbo la Kawe ni miundombinu ya barabara tu, pengine kidogo kwa huduma za maji ya uhakika kwa maeneo yaliyoendelezwa hivi karibuni kama kule Goba.

Ahadi kama hizi peleka huko ulikotokea, pengine labda ungekuja ahadi za kuweka barabara za lami ktk maeneo ambayo tushefanya uwekezaji mkubwa na hata kutoa ajira za uhakika ktk sekta binafsi, na pia tunalipa kwa kodi na maduhuli ya serikali kwa "recognizable extent".
 
Hiyo ni Mihemko ya watoa mawaidha wala siyo mambo ya kuchukulia siliasi!
Kuna maustadhi wengi wanaongeaga maneno zaidi ya hayo lakini watu wa dini nyingine wala hawachukulii maananani wanaendelea na shughuli zao !
Waweza toa mfano mkuu?
 
Achaguliwe Mara ngapi?,alipaswa kusema nikiapishwa màana mpaka sasa wananchi wanajua kuwa gwajima ndo mbunge na anasubiri kuapishwa tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…