Uchaguzi 2020 Askofu Gwajima: Nina Jina la Kiislamu, ninaitwa Rashidi

Uchaguzi 2020 Askofu Gwajima: Nina Jina la Kiislamu, ninaitwa Rashidi

Atuambie na jina lake la kutengenezea sinema za ngono!
 
Mimi nasema asipigiwe kura mtu yoyote kigeugeu ambaye yuko tayari kufanya lolote apate anachotaka ni bora mumpigie kura mtu hata kama kuna mambo hamkubaliani naye lakini amekuwa anasisimama katika yale anayoamini, watu mpaka wanataka kubadili dini? mbona hawa watu wanataka kuleta udini hata kama unaitwa Mohd ndio iweje? kwa kweli miaka hii mitano tumeanza kuona hii migawanyiko kila siku na viongozi sababu ndio wanashabikia yanazidi kukua hii ni hatari ni lazima wapigwe stop huko tunakoenda sio salama. Nadhani viongozi waanze hakuna tena viongozi wa dini kwenda katika kuomba du'a katika mikutano ya kisiasa hata shughuli za kiserikali marufuku, kila mtu ataomba katika nyumba zao za ibada na mbaya zaidi du'a zenyewe kama kumdhihaki Mungu tu hakuna uhalisia. Naomba viongozi wasikie hili viongozi wa dini hawatakiwi katika mikutano yoyote katika uchaguzi na baada.
Nakuunga mkono 100%.

Hata hizi salamu za kidini kwenye mikutano ya kisiasa na kiserikali ni unafiki tu. Salamu ya dini yako mpe wa dini yako huko mnakokutana. Tunapokuwa wengi wa dini tofauti hizo salamu zinaamsha hisia za ubaguzi tu.

Unapotusalimia 'Tumsifu Yesu Kristo' unadhani yule asiyeamini kuhusu hilo anajisikiaje? Angalao salamu ya "assalaam alaykum" katika maana yake ya "amani iwe nawe" inaweza kuwa nafuu kidogo kwa maana ya kwamba amani ni jambo zuri kwa kila mtu, lakini bado wapo wengi wasiojua maana ya maneno hayo na watasema ni salamu ya kiislamu (kumbe hata wakristo wa Syria, Morocco, Tunisia wanasalimiana hivyo hivyo). Hivyo kwa nia nzuri ya kutunza maelewano, tusalimiane tu kiujumla kwa salamu ambayo iko neutral.

Au kama unataka kushirikisha hadhira yako, tumia vibwagizo vilivyozoeleka kama 'hoyeee', mfano kama uko Iringa sema "Iringa hoyeeee!" utajibiwa kwa uchangamfu mkubwa "hoyeee!" imetosha, endelea kumwaga sera.

Kama ni kwenye chama tumia salamu za chama chako. Hivi mtu wa CCM unaona salamu ya "Kidumu Chama cha Mapinduzi" haitoshi hadi utumie salamu za kidini, wengine wanasema "asaramareko" sijui hata ni kitu gani hii! Mwingine roho haitaki kabisa lakini anajikakamua tu ili amfurahishe mdini, masikini ya Mungu anatamka "Bwana Yesu asifiwe" lakini ukimtazama usoni unaona kabisa hii kajisemea basi tu kumtumikia kafiri apate mradi wake!
 
Kwa hiyo Mtumishi jina la Rashid bado unalo siyo ? Ubatizo wako una maana gani leo kama mtu wa kale bado unaendelea kumtambua na kumtumia kuombea kura?

Sisi Tunashirikiana na tunasaidiana sio kwa sababu ya lmani zetu; bali kwa ubinadamu na utu wetu.
Kwa Maoni yangu Bado Haujawekwa Huru; wala hutendi Haki ya Bwana wetu Yesu Kristo Mungu aliye hai.

#Uhuru wa Kuabudu pasipo kuaimangwa ; Haki ya Kukosoa na Maendeleo ya Mtu.moja mmoja Rohoni
 
Kamati kuu ya Ccm imetudharau sana watu wa Kawe kutuletea hiki Kinyago
Sio kamati Kuu, ni JPM mwenyewe alitamka akiwa Tanganyika Packers kwamba alimkata mtoto wa dada yake kwa sababu aliona hatashinda...

Sasa uchaguzi wa ndani wa CCM ulikuwa wa nn kama tayari M'Kiti ana matokeo anayoyataka ?

CCM kawe imegawanyika, Rashidi hapendwi na CCM, hapendwi na upinzani

hapendwi na Waislam na hapendwi na Wakristo. Mkristo utampendaje mtu ambae kila siku anachokonoa watu wa dini nyingine kutujengea migongano na uhasama wa kidini?
 
Kwa hiyo Dr. Rashid kawatosa waumini wake Sasa atasali msikitini.

Kweli ukiwa mwanasiasa lazima uwe mwongo, mnafiki, na wakati fulani usitumie akili uliyopewa.

Kuna wakati huyu Bwana alikua anapambana na Makonda kwamba Hana akili, Sasa yeye ndiyo kawa Makonda sasa
 
Back
Top Bottom