Mimi nasema asipigiwe kura mtu yoyote kigeugeu ambaye yuko tayari kufanya lolote apate anachotaka ni bora mumpigie kura mtu hata kama kuna mambo hamkubaliani naye lakini amekuwa anasisimama katika yale anayoamini, watu mpaka wanataka kubadili dini? mbona hawa watu wanataka kuleta udini hata kama unaitwa Mohd ndio iweje? kwa kweli miaka hii mitano tumeanza kuona hii migawanyiko kila siku na viongozi sababu ndio wanashabikia yanazidi kukua hii ni hatari ni lazima wapigwe stop huko tunakoenda sio salama. Nadhani viongozi waanze hakuna tena viongozi wa dini kwenda katika kuomba du'a katika mikutano ya kisiasa hata shughuli za kiserikali marufuku, kila mtu ataomba katika nyumba zao za ibada na mbaya zaidi du'a zenyewe kama kumdhihaki Mungu tu hakuna uhalisia. Naomba viongozi wasikie hili viongozi wa dini hawatakiwi katika mikutano yoyote katika uchaguzi na baada.