PreGE2025 Askofu Gwajima: Sitayumba, sitabadilika na wala sitabadili msimamo!

PreGE2025 Askofu Gwajima: Sitayumba, sitabadilika na wala sitabadili msimamo!

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Yule ponjoro usikubari yahishe kumbuka ya bashite .sasa kama unataka mziki wa misomisondo tulia na unamakashabraka yako kwa gwajima.
leo kakuweka kiporo.
kumbe majina kama chura,kasongo na leo pnjoro tumelijua ni lako.
Anasema kama mtu atakaye mchokoa kwa wiki hataitisha press mara mbili kwa wiki.
SASA WASANII KUWENI MAKINI
Akiingia kwenye kumi na nane za Gwajima tu,tunaenda kujua kwanini degree yake ya kwanza Ud ni mwaka mmoja badala ya mitatu.
 
Ila siamini kuwa wanaoteka ni viongozi , naona kama ni chawa tu na kutokana wanafanya uchawa kuna namna kuna kuwa na kaaibu fulani kuchukua maamuzi,ila nimewaza tu 🤔
Ni hao wakubwa
Kwanini wanaopotea ni wapinzani wake Kisiasa na chura hakemei chochote.

Haiwezekani watu zaidi ya 20 kupotezwa na mamlaka zisihusuke
 
Gwajima anajifanya kenge kubadilisha gia hewani hana lolote
 

View: https://www.youtube.com/watch?v=NhpB9Zh2_6Y

Askofu Gwajima ameanza kwa kuwaambia waumini wasimame na kuimba wimbo wa 'Tanzania Tanzania', na kuongeza japokuwa tuna makabila tofauti tofauti lakini Tanzania ni yetu sote.

--
Gwajima anawaelezea waumini kuhusu mkutano wa waandishi wa habari aliofanya kuhusu suala la utekaji nchini lakini pamoja na mapendekezo aliyotoa kuhusu uteuzi wa vyombo vya ulinzi na usalama.

Anasema baada ya kuongea, Sheikh Jabiri huko Zanzibar alitekwa juzi tarehe 28 na mwili wake kupatikana ukiwa umetelekezwa. Watekaji wanateka MwanaCCM na watu wengine.

Chama cha Mapinduzi hakikubali utekaji, na mimi ni mwanachama wa CCM, hivyo naungana na waasisi na waliowahi kutangulia uongozi kuwa hatukubaliani na hili. Anayeteka watu ni kwa malengo yake mwenyewe. Yeyote anayepingana na mimi wenyewe mtajua mtamuitaje.

Gwajima ameongezea mifano ya watoto wa viongozi (Mwinyi, Kikwete, Majiliwa, Magufuli) ikiwa watatekwa na kung'olewa macho wazazi wao watajisikiaje?

Baada ya kukemea mauaji na utekaji, imezaliwa terminology ya Gwajimanization. "Sasa nilipoona Gwajimanization nikataka niitafasiri, hii Gwajimanization maana yake nini?" aliuliza Gwajima kabla ya kufafanua.

"Gwajimanization ama Gwajimanizing ni ujasiri usioteteleka wa kusema kweli, haijalishi ukweli huo ni mchungu au hauwapendezi walioko madarakani, ni dhamiri thabiti ya kutetea maslahi ya taifa kuliko maslahi ya mtu binafsi na kuinua sauti kwa uthubutu mkubwa bila kuyumba, kiasi cha kusababisha ivume ndani ya himaya za mamlaka na kutikisa misingi ya ufisadi na dhulma katika nchi."

Kwenye hili suala la utekaji sitayumba, nitahakikisha kila aliyetekwa anajulikana yuko wapi na anafanya nini. Vaeni silaha kamili za Bwana ili kushindana na pepo wabaya na tutashinda.

Kwa CCM, Gwajima ni hazina yenu, mnaye mtu ambaye hamjamjua bado. Ni mtu wa Mungu wa watu wote. Natetea waislam waliotekwa, Wakristo waliotekwa bila kujali chama. Kama mtu amekosea si apelekwe mahakamani. Vyombo vya ulinzi na usalama hawateki, bila shaka kunaweza kuwa na kakikundi ka utekaji na ndiko nakatumia ujumbe.

Ponjoro wa Kinondoni anachezesha kamari ambazo hata Mungu hapendi, mimi nilitaja watoto wa watu wengi ila Ponjoro kasikitika kisa mtoto mmoja niliyemtolea mfano. Nampa onyo, nikimuamkia atabaki vipande vipande na atanuka kinyesi maana mimi ni Jasusi la Mbinguni.

Naishia hapo, ila mtu akinichokoa chokoa, nitaitisha press. Na nikiitisha ya pili moshi utafuka hutoweza kufumbua macho.

Tutashusha maombi, ili damu ya mtu anayetekwa imrudie yule anayeteka.

Salamu ziwafikie maponjoro wote pale walipo
 
Aibu gani Sasa? Watekaji wanavaaga musk wewe unawajuaje?
Kwa maneno na matendo Yao utawatambua tu
We binadamu mwenzako wanatekwa anakufa, watu wanakemea, wewe unabeza.
Hivi uko timamu kweli?
Kuwa hata na utu, huo ushetani achana nao
Fikiria wewe ndo ufe halafu sisi tuliobaki tupuuze, familia yako, mke na watoto wawe Yatima kisa madaraka
 
Kombora moja tu la Moshi mzito mtekaji katoka mafichoni , Bi tunu alikosea sana kumjibu uyu jamaa sijui hana washauri maana hapakuwa na kibaya cha kujibu, dhahiri kaonyesha umma ye ni muhusika
Yule ni mwanamke shekhe hawanaga Kaba, ni mwendo wa mipasho bila kuangalia cheo chako
 
Video ya Askofu Gwajima inaonekana kuwa na athari kubwa kwa umma, ikizua mjadala kuhusu usalama wa raia na jukumu la serikali katika kushughulikia utekaji. Kauli zake zinaonyesha msimamo wa wazi dhidi ya vitendo vya utekaji, lakini zinakabiliwa na changamoto za uaminifu kutokana na historia yake ya kauli za utata na ukimya wake wa awali juu ya masuala sawa. Ingawa video yenyewe haipatikani tena kwa sababu ya uondoaji wake, maudhui yake yameathiri wengi, na yanaendelea kutoa changamoto kwa serikali kushughulikia masuala ya haki za binadamu.
 

Attachments

  • tweeload_a1a62061.mp4
    8 MB
Back
Top Bottom