Askofu Mwamakula kuongoza matembezi ya hiyari kuhamasisha Katiba Mpya na Tume Huru ya Uchaguzi

Askofu Mwamakula kuongoza matembezi ya hiyari kuhamasisha Katiba Mpya na Tume Huru ya Uchaguzi

ASKOFU KUONGOZA MATEMBEZI YA HIARI YA RAIA KUHAMASISHA UUNDAJI WA TUME HURU YA UCHAGUZI NA UANDIKAJI WA KATIBA MPYA NCHINI TANZANIA!

Wapendwa Watanzania!

Tunapenda kuwajulisha kuwa Askofu Mwamakula, anakusudia kuongoza Matembezi ya Hiari ya Raia yasiyopungua umbali wa Kilometa 15 katika Mikoa mbalimbali nchini Tanzania na nje ya nchi. Watu watakaoshiriki Matembezi hayo watatokea kila kona za mji husika hadi sehemu ya kukutania ambapo watu wote watakusanyika kwa ajili ya kufikisha au kutolea ujumbe. Ili kuepusha usumbufu, watu watakuwa wanatembea kimakundi lakini kila kundi halitazidi watu 20 na kama watu watakuwa wengi kutokea njia moja kutakuwa na muachano au umbali wa kilomita moja kati ya kundi na kundi njiani!

Lengo la Matembezi hayo ni kuwahamasisha Watanzania umuhimu wa Kuunda Tume Huru ya Uchaguzi na Kuandika Katiba Mpya kabla ya Mwaka 2025. Kwa mazingira yaliyopo sasa ambapo Bunge la Tanzania limekuwa ni Bunge la Chama kimoja ambacho katika Ilani yake hawana hoja ya Tume Huru na Katiba Mpya, hatuwezi kutegemea mambo hayo kuanzishwa na Bunge hili. Hata hivyo, watu wa makundi yote watahamasishwa kushiriki Matembezi hayo pasipo kujali vyama na itikadi zao.

Kila mkoa au mji utakuwa na Timu ya Uratibu ambayo itasaidia kuratibu na kuandaa Matembezi hayo. Wale watakaopenda kusaidia au kuwezesha Matembezi hayo wataelekezwa kuwasiliana na Timu ya Uratibu ya Kitaifa itakayosaidia Uratibu kwa niaba ya Askofu. Timu hiyo ya Uratibu wa Kitaifa sambamba na Timu za Mikoani zitatangazwa mapema kuanzia Januari 2021 baada ya kuundwa!

Kwa taarifa hii, tunaomba Watanzania wote wajiandae kushiriki Matembezi hayo katika kila Mkoa. Matembezi hayo yataanza mapema mwaka 2021 na tarehe ya kila Mkoa itatangazwa na utaratibu wote. Kuanzia Januari 2021, Askofu atatangaza rasmi utaratibu wa namna ya kushiriki ikiwemo Waratibu wa Matembezi katika kila Mkoa!

Kwa Watanzania walioko nje ya Tanzania, Askofu anaweza kufika katika nchi hizo endapo wataweza kuandaa mazingira.

Kwa sasa Askofu anamuomba kila mtu kusambaza ujumbe huu ili kuwaandaa Watanzania wote kwa matukio hayo ya kihistoria!

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!

Askof Mkuu Emmaus Bandekile Mwamakula
Hili ndilo jambo la msingi na muhimu kwa nchi yetu.Katiba mpya kama siyo kumaliza utata mwingi,itapunguza kwa sehemu kubwa.
 
I don't think anything will come out of this. Others have tried with no results. Tanzanians are simply not ready for this.
 
Ni muda wa kazi, si wa kuandamana - watu wafanye kazi na tusiweke mahusiano yetu na Serikali njia panda
 
Kwamba serikali haipendi haki wala tume huru, mpaka wananchi wakidai tume huru serikali italaumiwa?
Nipatie vigezo vya tume ya sasa kutokuwa na uhuru unaodaiwa na wenye nia ya kuandamana
 
Askofu ana raha gani kulisha kondoo ambao wapo oppressed? Ni dhambi kwa Mungu kwa watumishi wa Mungu kufumbia macho udhalimu. Askofu huyu hataki kubeba hiyo dhambi.
Usitumie lugha juimuishi kwenye masuala personal ,nakupa mfano usiseme sisi atupendi sema sipendi ,sasa kama uko oppressef mimi siko oppressed naitaji maneno ya Mungu zaidi kutoka kwa Askofu
 
canular
Fanya kazi uvivu nyumba ya njaa utamlaumu Mungu,wazazi ,majirani ,serkali ,etc
 
In almost all cases, Katiba Mpya haiji tu (hupewi) kwa kufanya “matembezi ya hiari”.

Haarafu haya matembezi yanaratibiwaje ili yalete tija? Matembezi hayo kwa mfano yataanzia wapi mpaka wapi kwa muda gani? Watanzania sisi tunajijua wenyewe!

Askofu ni bora angejikita zaidi na zaidi kuhubiri na kujaribu kuokoa roho za waumini wake katika safari yao kuelekea mbinguni
 
ASKOFU KUONGOZA MATEMBEZI YA HIARI YA RAIA KUHAMASISHA UUNDAJI WA TUME HURU YA UCHAGUZI NA UANDIKAJI WA KATIBA MPYA NCHINI TANZANIA!

Wapendwa Watanzania!

Tunapenda kuwajulisha kuwa Askofu Mwamakula, anakusudia kuongoza Matembezi ya Hiari ya Raia yasiyopungua umbali wa Kilometa 15 katika Mikoa mbalimbali nchini Tanzania na nje ya nchi. Watu watakaoshiriki Matembezi hayo watatokea kila kona za mji husika hadi sehemu ya kukutania ambapo watu wote watakusanyika kwa ajili ya kufikisha au kutolea ujumbe. Ili kuepusha usumbufu, watu watakuwa wanatembea kimakundi lakini kila kundi halitazidi watu 20 na kama watu watakuwa wengi kutokea njia moja kutakuwa na muachano au umbali wa kilomita moja kati ya kundi na kundi njiani!

Lengo la Matembezi hayo ni kuwahamasisha Watanzania umuhimu wa Kuunda Tume Huru ya Uchaguzi na Kuandika Katiba Mpya kabla ya Mwaka 2025. Kwa mazingira yaliyopo sasa ambapo Bunge la Tanzania limekuwa ni Bunge la Chama kimoja ambacho katika Ilani yake hawana hoja ya Tume Huru na Katiba Mpya, hatuwezi kutegemea mambo hayo kuanzishwa na Bunge hili. Hata hivyo, watu wa makundi yote watahamasishwa kushiriki Matembezi hayo pasipo kujali vyama na itikadi zao.

Kila mkoa au mji utakuwa na Timu ya Uratibu ambayo itasaidia kuratibu na kuandaa Matembezi hayo. Wale watakaopenda kusaidia au kuwezesha Matembezi hayo wataelekezwa kuwasiliana na Timu ya Uratibu ya Kitaifa itakayosaidia Uratibu kwa niaba ya Askofu. Timu hiyo ya Uratibu wa Kitaifa sambamba na Timu za Mikoani zitatangazwa mapema kuanzia Januari 2021 baada ya kuundwa.

Kwa taarifa hii, tunaomba Watanzania wote wajiandae kushiriki Matembezi hayo katika kila Mkoa. Matembezi hayo yataanza mapema mwaka 2021 na tarehe ya kila Mkoa itatangazwa na utaratibu wote. Kuanzia Januari 2021, Askofu atatangaza rasmi utaratibu wa namna ya kushiriki ikiwemo Waratibu wa Matembezi katika kila Mkoa.

Kwa Watanzania walioko nje ya Tanzania, Askofu anaweza kufika katika nchi hizo endapo wataweza kuandaa mazingira.

Kwa sasa Askofu anamuomba kila mtu kusambaza ujumbe huu ili kuwaandaa Watanzania wote kwa matukio hayo ya kihistoria!

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate.

Askof Mkuu Emmaus Bandekile Mwamakula
Ana hamu ya viboko huyo, naona kazhindwa kupata sadaka za kutosha.
 
Mungu mbariki Baba Askofu Mwamakula
Mungu gani huyo? Hao wanaaongozwa na shetani,
1 mwamakula
2 katimba
3 Bagonza
4 ponda
Hao wote mungu katupilia mbali maombi yao, inawezekana wana mahirizi na ndio maana hata ubunge wamepoteza kabisa kwa chama chao.
Sasa ni mungu gani unamsemea?

Kwenye Corona walijificha nyuma ya vichaka na hawakumtumainia mungu, sasa yeye huyo mungu apoteze muda kwa watu wasio muamini?
Wakatubu kwanza pia waache kurudia dhambi kama wanavyotaka kuanza sasa.
 
Haya matembezi ingependeza zaidi kama yangeratibiwa na kina Halima Mdee. Huyu Askof angejikita kwenye kazi yake ya kuchunga Kondoo Kanisani.

Sina hakika kama atapata hicho kibali, maana tushaambiwa uchaguzi umekwisha kinachofuata ni kuijenga nchi.
 
Sijawahi kuona uhamasishaji wa hovyo kama huu humu JF! Uchaguzi umekwisha sasa ni ujenzi wa uchumi PERIOD! Hawa wengine ni waleta fujo tu hapa nchini; hivyo vijisenti walivyopewa kama ruzuku wavitumie vizuri visije vikawaletea matatizo kwani sheria haibagui, itachukuliwa hata dhidi ya hivyo "vi color" vyao wanavyo vaa shingoni! Wasije wakalaumu mtu! Nawashauri waendelee na "kazi ya kulisha kondoo" haya mengine wawaachie wenyewe kazi zao!
 
Unajiita mzee, lkn huna busara.
 
Back
Top Bottom