Askofu Mwamakula: Tundu Lissu aomba hifadhi Ubalozi wa Ujerumani baada ya vitisho vya uhai wake

Ukiacha ujinga kando, hivi mwandishi yupi wa habari anayeweza kuripoti/kuandika hivi kama Askofu alivyoripoti/andika?
 
Mkuu Lissu kwa sasa ni raia Kama raia wengine anapoona anatishiwa Kuna mamlaka zipo,,,,aende police aripoti na sio ubalozini ....
 
Ahaaa... Lisu anazuia kitu gani?

Niambie Lisu atafanya nini jiwe akiamua kukaa milele madarakani?

Lisu kwa sasa ni debe tupu,

Mwambieni aache uoga atulie

Uko sahihi kabisa, fungulieni basi internet kwani jiwe anaogopa nini?
 
Ahaaa... Lisu anazuia kitu gani?

Niambie Lisu atafanya nini jiwe akiamua kukaa milele madarakani?

Lisu kwa sasa ni debe tupu,

Mwambieni aache uoga atulie
Hizi kufuru zina najis utawala dhalimu uliopo madarakani.
Nakuambia/nakuhakikishia ujinga wenu huu unaiharakisha hukumu ya Mungu juu ya udhalimu huu.
Hesabuni siku,mtaanza kugawana fito!!
 
Dah nilijua tu kwa kusumbua kule kwenye uchaguzi hawezi kuacha tu atambe hii miaka mitano
 
Yaliyosemwa wakati wa kampeni za 2020 zimemfanya mgombea wa CCM Mpya kujisikia ile sifa yake ndani na nje ya nchi imefutika.

Hata wapambe wake wanalifahamu hilo na wanahasira sasa zile sifa zote zimeyeyuka na uhalisia wa utawala wa CCM Mpya kufahamika.

Ndiyo ilivyo katika demokrasia na chaguzi, mshindi anaweza kuibuka lakini anatangazwa akiwa amejeruhiwa "heshima" yake mbele ya hadhara yote waliokuwa wanafuatilia uchaguzi huu. You Can Win The Battle, But Lose The War .

Hapa CCM Mpya, Viongozi wake na makada wameshinda "pambano" lakini Vita imewashinda. Vita ni ile heshima ya kilemba cha ukoka walioyokuwa wanaipigania ibaki imetoweka wamebaki watupu na ndiyo maana wanamsakama Tundu Lissu na viongozi wengine wa upinzani kwa kuweza kuiabisha CCM Mpya sura yake halisi (CCM Mpya) ionenake baada ya kuvuliwa joho na mask / barakoa iliyoficha ukweli kilichopo nyuma ya haya mavazi-sitiri .
 
Lini serikali iliwahi kusema inatoa ulinzi kwa Lissu?

Sijui unawaza nje ya box gani, anyway; najua hao "marafiki" zake ndio walimnyima pesa za matibabu alivyoenda kutibiwa nje.
 
Atleast today umeingiwa na ubinadamu.
 
Ukiondoa Serikali, hivi Lissu hana maadui kweli?

kwanini mlazimishe serikali itoe tamko kama vile

adui wa Lissu nchi hii ni serikali tu?? yani Lissu bana kuna vitu

huwa anafanya anajisahau kabisa,anabaki kusingizia serikali,kila kitu.
 
Ushahidi basi.

Wa vitisho.

Wa maombi ya hifadhi.

Wa kukataliwa kibali.

Lissu atoe ushahidi mara ngapi?mara ya kwanza alisema hvi hvi na akipigwa risasi
 
Ukiondoa serikali,hivi lissu hana maadui kweli?

kwanini mlazimishe serikali itoe tamko kama vile

adui wa lissu nchi hii ni serikali tu?? yani lissu bana kuna vitu

huwa anafanya anajisahau kbsaaa,anabaki kusingizia serikali,kila kitu.
Mara ya kwanza alisema hivi hivi,akapuuzwa na kikamkuta kilichomkuta!Ben Saanane naye alisema humu humu jamvini mpaka akaweka wazi vitisho alivyopewa na akaambiwa hataandika tena,ikawa kweli!
Tuwe na utu,uhai ni zawadi kutoka kwa Mungu!Inakuwaje binadamu wengine wanajipa haki ya kusitisha maisha ya watu?
 
Lini serikali iliwahi kusema inatoa ulinzi kwa Lissu?

Sijui unawaza nje ya box gani, anyway; najua hao "marafiki" zake ndio walimnyima pesa za matibabu alivyoenda kutibiwa nje.
Walimnyima pesa za matibabu na akarudi akiamini watampigia kura za Urais.
Vihoja vya upinzani haviishagi
 
Mkuu umesema mengi lakini mengine umeyaacha ambayo ni. Lisu huyu huyu ambae Mwenyezi Mungu amemnusuru kifo baada ya kupigwa risasi lukuki na watu wasiojulikana lakini wanaeleweka.

Na ni Lisu huyu huyu ambae serekali ilikataa kugharamia matibabu yake alipokuwa akitibiwa nnje ya nchi. Ni lisu huyu huyu ambae spika aliamua avuliwe ubunge kwa vile alikuwa yeye spika hafahamu Lisu aliko japo alikuwa kwenye tiba. Ni Lisu huyu huyu ambae alinyimwa mshahara wake wakati akitibiwa nnje ya nchi.

Ni lisu huyu huyu ambae amewafanya ccm na washirika wake wafanye dhambi kubwa ya uharamia wa kughushi matokeo ya uchaguzi kwa kuogopa mteule wao wa kiti cha uraisi kushindwa vibaya kwenye uchaguzi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…