''Askofu Mwingira'' aliwahi kutuambia kuwa Lazaro Nyalandu atakuwa Rais wa Tanzania mwaka 2015!
Kauli kama hizi za 'Wachungaji, Maaskofu na Manabii'' tumezisikia sana na tuna kumbukumbu nazo hizi;
“Raisi ajae wa Tanzania ni Lowassa licha ya kuwa baadhi ya watu wamepanga mambo mabaya dhidi yake. Aidha alisema kwamba Mungu alimwambia awaambie wana CCM kuwa amemtuma yeye (Askofu Komanya) aseme kuwa Mungu ndiye aliyemchagua Lowassa” (Chanzo: Gazeti la Jambo Leo la tarehe 21/03/2014 siku ya Ijumaa).
Kwa Mtanzania yeyote aliye na hulka na tabia ya kuheshimu na kuamini viongozi wa dini anajenga imani ya dhati kwamba Mheshimiwa Lowassa ni lazima atakuwa Raisi wa Tanzania tu kwani hayo sio mawazo ya wanaadamu bali ni maono yaliyotoka kwa Mwenye ezi Mungu.
Pamoja na kuaminishwa hivyo na Askofu Komanya, Watanzania pia walipokea “maono” mengine kutoka kwa Nabii Josephat Mwingira wa Huduma ya EFATHA.
“Siku chache baada ya kutangaza kujitosa rasmi kuwania ukuu wa dola (uraisi), Waziri wa Maliasili na Utalii, Mheshimiwa Lazaro Nyalandu aliadhimisha sherehe za mwaka mpya wa 2015 katika Kanisa la EFATHA huku Mchungaji wa Kanisa hilo Josephat Mwingira alimtabiria ushindi wa safari yake aliyoianza.
Zaidi Mchungaji Mwingira alisema neno hilo ni la kinabii na kusisitiza hakuna wa kumzuia Nyalandu kwa sababu ukuu umeamriwa juu yake. Mwingira ambaye alisema neno hilo limetoka kwa Bwana alisisitiza kuwa vikwazo juu ya Nyalandu havitakuwepo tena” (Chanzo: Gazeti la Mtanzania la tarehe 02/01/2015 ukurasa wa tatu).
Pamoja na maono hayo kuonekana yanapingana juu ya ni nani haswa ndiye atakuwa Raisi wetu katika awamu ya tano.
Kwa sasa tunajua hatma ya maono yao ya mwaka 2015 lakini kwa kushangaa wameanza tena kuja na kile wanachodai ''maono'' kutoka kwa Mungu!
Tanzania kuna vituko!