Askofu Mwingira: Nimenusurika kuuawa mara tatu na watu wa Serikali

Acha kelele ndugu, hao unaowaona kuwa hawawezi kufanya kizembe ndio hao hao waliweka camera na ndio hao waliondoa camera, wangelikuwa sio wazembe wangelikuwa wameshamdaka aliyemshambulia Lissu.

Hebu fikiri kiutu uzima "wamekwama wapi kumbaini aliye mshambulia Lissu?"
 
Wajivunia ushetani?
 

Nabii Askofu Mwingira agoma Kupima DNA, ni katika kesi ya kuzaa na mke wa mtu
 

Walinzi Wa Nabii Mwingira Wakata Masikio Wananchi Rukwa Shamba la Milonje!!!!
 

Wananchi wavamia shamba la Nabii Josephati Mwingira Break Throw Mapinga
 
Haa yote yametokea miaka ya 2011 mpaka 2013,halafu aje mtu hapa aseme Nabii fake anaonewa,mtumishi wa mungu unatembea na walinzi unaogopa kudhuriwa na nani kama uko clean?
 
Maoni gani ulinyimwa uhuru wa kuyatoa?
 
Mungu ndiye hupanga kesho ya Mtu na sio mwanadamu, Kila tukio ambalo humoata mwanadamu Mungu anakuwa ameshajua. Kwa hiyo usiogope wanaopanga kukuangamiza kesho yake ,Mungu huwaangamiza wao na kukuaxha
 
Ndio kama hadithi ya mchimba kisima. Au kama ile hadithi ya Victor Frankenstein ya miaka ya 1800s aliyeunda zimwi lililotaka kumuangamiza yeye mwenyewe, familia na ndugu zake.

Waliofanikisha kuigeuza CCM kuwa “deep state” au “mhimili uliojichimbia chini zaidi” kama alivyokuwa akijinasibu Jiwe, ndio walioleta adha yote hii. Hakuna atakayekuwa salama. Hata wapenzi wa Jiwe wanaamini alizimishwa na “deep state”!

Wapo wanaoamini kuwa hata muasisi mwenyewe, Mwalimu JKN na kijana wake Mkapa waliondolewa na deep state! It is crazy!
 
Kamera ziliondolewa BAADA ya tukio. Ndio serikali ishindwe kuwapata wahusika hadi leo. Labda kama ina ushirika na hao wahuni.

Halafu awamu ya tano kwenye “misheni” za kuzimisha ni kama vile haikuwa ikitumia professionals. Au ilikuwa ikipenda kujulikana. Tukio kama la Lwajabe data zilikuwa nje kabisa hadi EU na US kutoa tishio la “kimya kimya”.
 
Hiyo kazi ilifanywa na wahuni waliokuwa ndani humohumo. Na lengo lilikuwa clear from the beginning kuwa indicators zote zioneshe serikali ya JPM inahusika.
Na wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa kwa sababu hata Lisu mwenyewe anaamini ile kazi ilikuwa ni ya JPM.
Lakini kumbuka Tanzania's intelligence Unit ni among the BEST in Africa.
Samia alishawaambia ile kazi haikuwa na Baraka za serikali ya JPM.
Serikali ya Tz haiwezi kukosea pakubwa kiasi kile.
Yaani SMG full magazine risasi 30 zinaisha. Unapachika Magazine nyingine eti umetumwa na JPM umuue lisu?
 
Kwa sasa hao wanaoitwa 'deep state' wanaonekana kama mhimili wa 4 (japo tuna mihimili 3 tu inayotambulika kikatiba).
 
Hao 'wahuni' walipatikana?
 
Hao 'wahuni' walipatikana?
Huwa inside jobs za aina hii mnaminyana ndani kwa ndani kimya kimya kwa sababu, namna mchoro unavyosukwa kunakuwa hakuna jinsi serikali ikakosa kuwa implicated.
Ndio maana hata Interpol hawakuruhusiwa, because lengo lilikuwa interpol waje wasindilie kuwa ni serikali na JPM iliyompiga risasi Tal ili ikiwezekana mabeberu yapate pa kuingilia kwa kisingizio cha JPM muuaji.
 
Mmeamua kuimba pambio sasa 😂
Ila hamna majibu kuhusu udhaifu wa intelligent ya nchi maana hadi leo hamjabaini ni nani alimimina hizo risasi 30.

Hii ni tz 😂😂
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…