Elections 2015 Askofu Mwingira: "Rais wa awamu ya tano siyo katoliki wala uislam"

Elections 2015 Askofu Mwingira: "Rais wa awamu ya tano siyo katoliki wala uislam"

haya ni mambo ya kawaidatu. Najua jambo hili linawaumiza sana watu wa ccm. Hawapendi kusikia mambo haya.

Tb joshua. Alitabiri uchaguzi wa kenya. Na hikawa hivyo, akatabiri na uchaguzi wa nchi yake nigeria na hikawa hivyo hivyo.

Na hata hapa kwetu alishatabiri juu ya lowassa kuchukua nchi mwaka uhu. Sasa wanaobisha tukutane baada ya uchaguzi.
Umenifurahisha kweli mzazi. Eti mwaka UHU. Halafu tena eti "Na HIKAWA hivyo..." Wakuache kwa raha zako na Eddo wako bana. Na HIKAWE hivyo hivyo tu!
 
Why awataje waislam wakati wagombea wawili powerful hakuna muislam?
halafu ana wa group waisla na wakatoliki kundi moja...why?

Na why washabiki wa Lowassa wanaamini Lowassa ni mlokole wakati yeye anasema ni mlutheri?

Why, why, why! Sababu Lowassa ndie next coming presidaa
 
Why awataje waislam wakati wagombea wawili powerful hakuna muislam?
halafu ana wa group waisla na wakatoliki kundi moja...why?

Na why washabiki wa Lowassa wanaamini Lowassa ni mlokole wakati yeye anasema ni mlutheri?
Hata walutheri wanaweza kuwa walokole; Lowasa ni mlokole - ameokolewa toka dhambini CCMs na alikiri kwa kinywa, Yesu kristo amemuokoa toka mikononi mwa shetanii.. CCMs.
 
Kumbe ni dili la walokole wameungana na waprotestanti? Shughuli mwaka huu; na tuone kama kura zao zitatosha

Kama kitu hikujui unauliza,waprotestant ni madhehebu yote kikristo yaliyoasi kutoka romancatholic ukiondoa wasabato,upo hapo!.
 
Hapo mnapoingiza dini ktk siasa kama ilivyoasisiwa na ccm ndipo mnaharibu. Mi mkatoliki siungi mkono Magufuli. Sasa tuambieni ni vita ya Kidini niturn into hostile? Hili taifa tunalipeleka wapi jamani, hawa ndio wanaharibia wagombea. Sisi tutushasema ni mwaka wa mabadiriko basi, na wala hoja si dini gani. kama hoja ni dini basi magufuli lazima atashinda kitu ambacho hatuombi kitokee
 
Dr Slaa alisema maaskofu wamenunuliwa na Lowassa mkataka ushahidi..haya ushahidi ndi huu sijui mnataka nini kingine...Na ndugu zangu wa chadema mkiitwa ni chama cha wakristo sijui bado mtakataa.

Kwahiyo unataka kuwaminisha watanzania kuwa ccm pia ni chama cha waislam manake nawenyewe wanatasisi inayoitwa Bakwata.
 
Mwingira huwa haongeagi mara nyingi lkn neno moja tuu akitoa halirudi. 2005 alisema nchi itapita kipindi kigumu cha uongozi mbovu kwa miaka kumi na imekuwa hivyo!!!!

Akamwambia Dr. Slaa mwezi huu wa nne kabla ya michakato ya kukatwa alipomtembelea kwa semina ya wachungaji "ukombozi ni lazima ila kuna mtoto atazaliwa, je utampokea au utamua? imekua hivyo!!!

Hili alilosema this time halizuiliki!!!!!! Nyie pigeni kelele sababu hamtaki ukweli ila soma bible na vitabu vyote vya dini kabla ya kuanguka ufalme wowote Mungu huwaambia watumishi wake.
 
Mihela hiyo. Chezea masai wewe?. Mbona wakati wa mafuriko au balaa lolote hawatabiri au Mungu anakuwa kalewa na kuuchapa usingizi? Fankuuuurooo
 
Lakini mwaka2005 kuna viongozi kadhaa wadini zote walidai kuwa Kikwete ni chaguo la MUNGU,hatukusikia watu wakilalamika.tena walitamka maneno haya wakiwa ndani ya nyumba za ibada.
 
Mbona hawazungumzi na Mungu wao wakati wa gharika za mafuriko? Au Mungu wenu anakuwa kalewa kalala?
 
Askofu Josephat Mwingira asema Raisi wa awamu ya tano atatoka nje ya madhehebu ya katoliki na uislam.

Pia askofu huyo mwenye makanisa kila pande ya nchi na wafuasi lukuki aliendelea kusema kwamba uongozi wa Raisi huyo utakuwa na nguvu sana na atabadilisha mambo mengi kwa kipindi kifupi sana (Maono kutoka mbinguni)


Akiri za kuambiwa changanya na za kwako ..Lengo ni mabadiliko.


jisikilizie mwenyewe Audio hii nime attach hapo wanajamvi

wehu nyie. Mbona hawazungumzi na Mungu wao wakati wa gharika za mafuriko? Au Mungu wenu anakuwa kalewa kalala?
 
Back
Top Bottom