PostGE2025 Askofu Rweyongeza: Kuwaombea Marehemu wa Oktoba 29, 2025, Si kuvuruga amani

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections
Jiulize kwanin huo ujinga unafanywa na maaskofu wa kikatoliki tu?
Mkuu wewe chukulia kuombe wafu ni ujinga kwa mtizamo wako inatosha kabisa. Na acha hao wanondeleza imani yao ya kuombea wafu waendelee nayo. Historia inaonyesha kuwa imani zote za dini zimepitia udhalilishaji wa aina moja au nyingine mpaka kufika leo hii. Pia Tanzania haikufika hapa kwa bahati mbaya bali ni matunda ya seriakli na wazee wetu kuvumiliana katika imani zao tofauti tofauti.
 
Hao hao TEC mtu akijinyonga huwa hawaruhusu hata kumuingiza kanisani, vp HOA waliochoma na kuharibu Mali za watu, vip kuhusu hao walioharibu miundombinu yetu, vipi hao waliofanya watu wakafa kwa kukosa huduma za afya?
 
Huwa najiuliza hawa maaskofu wa TEC (katoliki) ni watumishi wa Mungu ukweli?
Mimi binafsi nasema hawa si watumishi wa Mungu ni watumishi wa shetani, hii inajidhihirisha kwa kauli zao wakiwa madhabuni kwakweli ni aibu Mno kuona askofu anahubiri uchochezi, kuona askofu anachochea vurugu aisee so painful 😭😭😭
Amechochea nini huyo Askofu
 
Uzuri hata ukiandika ujinga wako hauzuii watu kwenda ibadani utatoa milio tu nyie si mna bunduki wauweni Sasa si mnatishaga watu na kuwaharras leo hii mnataka diplomacy? Wakati mmeua watu
 
Hii nchi ina baadhi ya watu wenye akili ndogo na ndio hao huwa wanapotosha viongozi wetu. Kama mimi ningekuwa kiongozi wa serikali ningewaunga mkono katoliki na ningewaomba viongozi wa dini nyingine wafuate mfano wao. Kwa sababu watu wakienda makanisani na misikitini kwa wingi siku hiyo itaondoa kabisa au itapunguza idadi ya watu wenye mtizamo wa kufanya maandamano. Kwa sababu sitaki kuamini kuwa mtu atakayeenda kanisani au msikitini siku hiyo akapta neno la Mungu vizuri halafu aandamane.

Na sio siri kuwa ni kweli watu walikufa kwenye maandamano na kati yao waliokufa wapo waamini wa kanisa katoliki na kanisa katoliki linaamini katika kuwaombea wafu sasa hapo tatizo linatoka wapi. Na kila mtu kwa imani yake au nafsi yake huwa anafanya ibada ya kukumbuka na kuenzi ndugu zake waliotangulia mbele za haki kwa kufanya ibada kadiri anavyoona yeye mwenyewe inavyofaa.

Kama kuna kiongozi yoyote wa dini akithibitika kutumia mwanya huo kuhamsisha maandamano basi akamatwe yeye kama yeye na achukuliwe hatua yeye binafsi badala ya kukaa tu kutunga uongo kuwa dini fulani inataka kuleta vurugu. Hebu wakati mwingine tuwe positive ili kuondoa taharuki zisizo na msingi.

Ni mtizamo tu.
Andiko bora kabisa, lakini nchi hii ina viongozi wenye akili kama Tlaatlaah na Lucas, sasa hapo unategemea nini? Tutafika tu japo tutakuwa tumechoka sana
 
Hao hao TEC mtu akijinyonga huwa hawaruhusu hata kumuingiza kanisani, vp HOA waliochoma na kuharibu Mali za watu, vip kuhusu hao walioharibu miundombinu yetu, vipi hao waliofanya watu wakafa kwa kukosa huduma za afya?
Kuna daktari aliuawa nje ya get lake akitoka hospitali kwenye shift yake, kuna askari magereza alipigwa risasi akitoka msikitini mchana kweupe tena askari mwenzao, kuna mtu alitunguliwa akiwa amejipumzisha kwenye ghorofa lake.

Kuna mfanya kazi wa mashine ya kusaga na kukoboa amepigwa akiwa sehemu yake ya kazi, hao wameharibu mali ya nani, waharibu miundo mbinu ya nani? Mbona mnapotetea akili zenu mnazificha? Tulisema fanyeni uchunguzi basi mpaka sasa mwaka mmoja hamna chochote mmesema yaani mnaona kama mnaongoza mang'ombe na hakuna wa kufanya chochote
 
Uzuri hata ukiandika ujinga wako hauzuii watu kwenda ibadani utatoa milio tu nyie si mna bunduki wauweni Sasa si mnatishaga watu na kuwaharras leo hii mnataka diplomacy? Wakati mmeua watu
Mtabaki mnazunguka wenyewe kanisani
 
Huyo Daktari alikuwa anafanya vurugu...hyo shift aliendaje na watu tumezuiwa kuzurula
 
Uzuri hata ukiandika ujinga wako hauzuii watu kwenda ibadani utatoa milio tu nyie si mna bunduki wauweni Sasa si mnatishaga watu na kuwaharras leo hii mnataka diplomacy? Wakati mmeua watu
Na ibadani tutaenda, tuombe toba kwa mauaji yaliyotokea, lakini pia tutaombea Kiti cha raisi kinaonea watu

Mithali 28:16-17

"Mkuu aliyepungukiwa na akili huwaonea watu sana;
Bali achukiaye kutamani ataongeza siku zake."

"Aliyelemewa na damu ya mtu
Atalikimbilia shimo; wala mtu asimzuie."
 
Kamkamateni mnashindwa nini siyo nyie mnajitapa mna jeshi mna police mna mahakama mna magereza?
 
Huyo Daktari alikuwa anafanya vurugu...hyo shift aliendaje na watu tumezuiwa kuzurula
Si unaona akili yako, Daktari amekaa siku tatu, anarudi kwake kapigwa getini kwake, haya huyo Askari magereza alifanya vurugu msikitini? Vipi huyo aliyekuwa kwake juu ya ghorofa ametunguliwa? Na huyo baba msagishaji wa mashine yuko eneo lake la kazi anauawa hapo. Je kuna uchunguzi umefanyika, kuna taarifa imetoka juu ya hayo mauaji?

Wakatoriki kwenye liturugia yao kuna ibada ya kuombea waliokufa na inafanyika mara kwa mara, kwa hiyo hii ibada yao inakuhangaisha nini? Hutaki wafanye kwa sababu zipi?
 
Waliambiwa wabakie ndani
Huyo alikuwa anachoma vituo vya mafuta
 
Waliambiwa wabakie ndani
Huyo alikuwa anachoma vituo vya mafuta
Kweli umeamua kubwa zezeta Mkuu samahani lakini, madaktari na manesi waliendelea na kazi, maduka ya kuuza vyakula yaliamuliwa kufunguliwa na nadhani umesahau Katazo lilikuwa usionekane nje kuanzia saa 12 jioni, hao nazungumza wamepigwa risasi mchana wa saa 7 mpaka saa nane

Ila kwakuwa uko kutetea ugali endelea
 
Back
Top Bottom