Atakayeigusa Saudia, tutambomoa na kumfuta duniani

Atakayeigusa Saudia, tutambomoa na kumfuta duniani

marekani hachukuwi mafuta saud,
anachukua venezuela :nigeria na pia mafuta anayochimba yeye.
Saudi anauza mafuta ulaya,japan,china etc
Siyo kweli. Mafuta ya Mmarekani yanatoka hapa: (1) Yeye mwenyewe - 38.8% (2) Latin America (Mexico - 7.5% na Venezuela - 5.9% etc) (3) Canada - 15.1% (4) Persian Gulf (Saudia 8.1% etc) 5. Afrika (Nigeria - 5.2% etc) 6. Others - 3.1%.

Saudia actually ni ya pili kwa nchi zinazoiuzia mafuta kwa wingi USA. Ya kwanza ni Canada. Narudia tena Mmarekani yuko pale kwa ajili ya mafuta tu japo upepo wa uzalishaji umeanza kubadilika hasa kwa Marekani yenyewe kuanza kuzalisha mafuta yake kwa wingi kwa kutumia teknolojia ya fracking.
be67151e759bf78c32f5942adbcb6766.jpg
 
Siyo kweli. Mafuta ya Marekani yanatoka hapa: (1) Yeye mwenyewe - 38.8% (2) Latin America (Mexico - 7.5% na Venezuela - 5.9% etc) (3) Canada - 15.1% (4) Persian Gulf (Saudia 8.1% etc) 5. Afrika (Nigeria - 5.2% etc) 6. Others - 3.1%.

Saudia actually ni ya pili kwa nchi zinazouza mafuta kwa wingi USA. Ya kwanza ni Canada. Narudia tena Mmarekani yuko pale kwa ajili ya mafuta tu japo upepo wa uzalishaji umeanza kubadilika hasa kwa Marekani yenyewe kuanza kuzalisha mafuta yake kwa wingi kwa kutumia teknolojia ya fracking.
be67151e759bf78c32f5942adbcb6766.jpg
could be,maana naona data zako ziko update,baada ya kudoublecheck
 
Saudia ni nchi iliyobarikiwa sana kiasi nchi nyingi zimekuwa na wivu mkubwa juu yao. .
 
Viscious Circle Of Ignorance. Unajua Hija Pekee Inaingiza Saudia Mabilioni Mangapi Ya Dola?
 
saudia yenyewe inapewa misaada ya kijeshi from america
 
saudia arabia hapigwi na wala hatapigwa alishafanya kitu kimoja na marekani kinaitwa SAUDI ARABIA MONEY LAUNDERING AFFAIR... ile ilikuwa ni protection yake ya milele


someni hii hapa inatoka kwenye kitabu kilichoandikwa na Ex CIA kinaitwa confession of an economic hitman



CHAPTER 15. The Saudi Arabian Money-laundering Affair

In 1974, a diplomat from Saudi Arabia showed me photos of Riyadh, the capital of his country. Included in these photos was a herd of goats rummaging among piles of refuse outside a government building. When I asked the diplomat about them, his response shocked me. He told me that they were the city’s main garbage disposal system.

“No self-respecting Saudi would ever collect trash,” he said. “We leave it to the beasts.”

Goats! In the capital of the world’s greatest oil kingdom. It seemed unbelievable.

At the time, I was one of a group of consultants just beginning to try to piece together a solution to the oil crisis. Those goats led me to an understanding of how that solution might evolve, especially given the country’s pattern of development over the previous three centuries.

Saudi Arabia’s history is full of violence and religious fanaticism. In the eighteenth century, Mohammed ibn Saud, a local warlord, joined forces with fundamentalists from the ultraconservative Wahhabi sect. It was a powerful union, and during the next two hundred years the Saud family and their Wahhabi allies conquered most of the Arabian Peninsula, including Islam’s holiest sites, Mecca and Medina.

Saudi society reflected the puritanical idealism of its founders, and a strict interpretation of Koranic beliefs was enforced. Religious police ensured adherence to the mandate to pray five times a day. Women were required to cover themselves from head to toe. Punishment for criminals was severe; public executions and stonings were common. During my first visit to Riyadh, I was amazed when my driver told me I could leave my camera, briefcase, and even my wallet in plain sight inside our car, parked near the open market, without locking it.

“No one,” he said, “would think of stealing here. Thieves have their hands cut off.”

Later that day, he asked me if I would like to visit so-called Chop Chop Square and watch a beheading. Wahhabism’s adherence to what we would consider extreme puritanism made the streets safe from thieves—and demanded the harshest form of corporal punishment for those who violated the laws. I declined the invitation.

The Saudi view of religion as an important element of politics and economics contributed to the oil embargo that shook the Western world. On October 6, 1973 (Yom Kippur, the holiest of Jewish holidays), Egypt and Syria launched simultaneous attacks on Israel. It was the beginning of the October War—the fourth and most destructive of the Arab-Israeli wars, and the one that would have the greatest impact on the world. Egypt’s President Sadat pressured Saudi Arabia’s King Faisal to retaliate against the United States’ complicity with Israel by employing what Sadat referred to as “the oil weapon.” On October 16, Iran and the five Arab Gulf states, including Saudi Arabia, announced a 70 percent increase in the posted price of oil.

Meeting in Kuwait City, Arab oil ministers pondered further options. The Iraqi representative was vehemently in favor of targeting the United States. He called on the other delegates to nationalizeAmerican businesses in the Arab world, to impose a total oil embargo on the United States and on all other nations friendly to Israel, and to withdraw Arab funds from every American bank. He pointed out that Arab bank accounts were substantial and that this action could result in a panic not unlike that of 1929.

Other Arab ministers were reluctant to agree to such a radical plan, but on October 17 they did decide to move forward with a more limited embargo, which would begin with a 5 percent cut in production and then impose an additional 5 percent reduction every month until their political objectives were met. They agreed that the United States should be punished for its pro-Israeli stance and should therefore have the most severe embargo levied against it. Several of the countries attending the meeting announced that they would implement cutbacks of 10 percent, rather than 5 percent.

On October 19, President Nixon asked Congress for $2.2 billion in aid to Israel. The next day, Saudi Arabia and other Arab producers imposed a total embargo on oil shipments to the United States.1

The oil embargo ended on March 18, 1974. Its duration was short, its impact immense. The selling
 
sisi waislam wenye chuki na marekani (saudia ni pro US) ambao tunapenda sisi na vizazi vyetu vijavyo kwenda kuhijj pale saudia inatuwia ngumu kuchangia hii mada.
Napata shida kuelewa mantiki ya hii mada ni nini?
 
hivi unajua yale mahoteli makubwa saudia ni soko kubwa sana la pombe na kitimoto yaani hiyo misaada unayochekelea ni kodi za wauza nguruwe na pombe so uwe mpole kidogo.
 
Utakuta jitu lipo IKWIRIRI huko linapiga miayo tu halafu linakandia taifa teule lenye miji mitakatifu miwili MECCA na MADINA . Takbiiiir
 
Dunia ya ajabu sana hii.

Familia ya Saudi inayotawala Saudi Arabia kwa msimamo mkali sana wa kidini usioruhusu kabisa ibada ya Kikristo nchini humo ni MARAFIKI WAKUU wa wahafidhina wa USA wenye msimamo mkali sana wa Kikristo wenye kuchukia Uislamu.

Saudi Arabia wanafahamika kwa kufadhili vikundi hatari vya kigaidi duniani kudhuru Washia na nchi wanazotawala. Huku ikiwa nadra sana siku hizi (hasa baada ya enzi za Al Qaeda) kusikia wakitishia usalama wa Israel na Marekani. Ulaya ndio inabebeshwa zigo la Marekani.
 
Sina maana ya kuuunga mkono maudhui ya mada ila kuhusu suala la misaada tuweke rikodi sawa, kua:-

-Saudia ni moja nchi zinazochangia Bajeti ya SMT kwa miaka mingi sasa.

-Chuo kikuu "Zanzibar University" kimeanzishwa na kinaendeshwa na taasisi ya Saudia.
Vijana wengi wa visiwani, bara na Africa mashariki na kati wame/wanasoma katika chuo hichi.

-taasisi ndogo ndogo za Saudi zinafadhili miradi mingi ya Jamii, elimu, afya, maji n.k mfano King Feisal Hospital iliyopo Tabata (kama sikosei)
Hii hospital ya Tabata, ni waOman kama siyo wakuwait
 
Mbona mnaleta dharau nyie wagalatia, povu la nini na vitu vipo wazi. Hauhitaji kuwa na shahada ya chuo kikuu kuona namna nchi kadhaa zinavyojipanga kuiporomosha Saudia kiuchumi na kiusalama? ikiwemo Iran?

Mkuu jaribu kufatilia kwa karibu nyenendo za watawala wa Saudia, ukoo wa kifalme wa Saudia ndio wana finance Ugaidi mashariki ya kati na Africa kaskazini, ku advocate regime change kwenye mataifa ambayo wanafikiri ni tishio kwa Ufalme wao mfano Syria,Yemen,Iraq, Iran yaani utawala huo wa Kifalme huko in bad terms na nchi za Mashariki ya kati save Uturuki, Israel, Quatar nk

Wanachochea mifarakano ya kidini kati ya Washia na Sunni nk, Ufalme wa Saudia ni madikteita hawaruhusu Taifa hilo liwe na Demokrasia ya kweli wananyanyasa sana wanawake wa Taifa hilo na wanao toka nje kuja kufanya kazi za Uyaya.

Ufalme huo hauna goodtrack record ya kuheshimu binadamu wenzao save Wafalme wenzao au watawala wa nchi za magharibi, wana dhalau sana na viburi, dhalau zao hazijalishi kama wewe ni mwislaam au mkristo - chukulia mfano wa waumini kuangukiwa na crane/ukuta huko Mecca, hawakuonyesha kujali hata kidogo kazi ni kulahumu Wafrica kwamba ndio walihusika na stampede iliyo changia watu wengi kufa! Miaka ya nyuma moto uliwahi kuua waumini wengi, Ufalme huo bila aibu wakasingizia Waafrica kwamba ndio walisababisha moto kwa kuwa hawajui kutumia majiko ya gesi!!!!

Misaada mingi wanayo toa niya kisiasa zaidi wanaitumia kama PR ya kuzuga Dunia ili waendelee kubaki madarakani milele, nataka nieleweke kwamba raia wa Saudia na Waislaam karibu wote hawana tatizo lolote wenye matatizo ni Ukoo wa Kifalme ni wanafiki sana, kama si busara na hekima za Obama Ufalme wa Saudia na Uturuki walikuwa wanachochea vita ya tatu ya Dunia kuanzishwa nchini Syria - hawatumii busara hata kidogo.

Kwa nini nasema ni wanafiki? Huko Saudia ukikamatwa unakunywa pombe au una relationship na mwanamke out of wedlock unaweza kuhukumiwa a captial punishment!

Nilikuwa naona wana wa kifalme wakija mjini London wanajirusha kwenye ma night club, wanakunywa Pombe kali kama kawa na company ya akina mama wa barabarani wanawaganda kama luba maana wanajua wanazo!!! Wakati fulani kuna call girl aliwahi kueleza kwenye tabloid newspaper (The SUN) kwamba mwana wa Mfalme alimununulia nyumba ya kifahari za "inner London!!"

Uwezi kuamini kwamba Ukoo wa Kifalme wa Saudia unao jifanya una maadili ya hali ya juu ukiwa nchini mwao, wakitoka nje ya nchi yao wanafanya mambo ya kishenzi kweli kweli niliyo ya eleza hapo juu.

Ni ukoo unao tawala Saudia with iron fist, element ya u sadism waliyo nao ndio maana upendelea kutumia majambia kukata shingo za petty thieves/wahuni lakini linapokuja suala la ukoo wao kufanya mambo ya kudhalilisha Taifa lao wakiwa nje ya nchi, hao hawachukulii hatua yoyote wanaedelea kuwaonea raia masikini kwa kuwahukumu adhabu za kinyama wanavamia nchi masikini kama Yemen na kuua raia ovyo!

Juzi juzi hapa imekamatwa a private jet yao katika uwanja wa ndege wa Gatwick au Luton sikumbuki vizuri, wapelelezi/polisi walikuta mzigo wa COCAINE ndani ya ndege - mi sikushangazwa kwa ugunduzi huo, nakumbuka miaka ya zamani kuna mwana wa Mfalme wa Saudia alikutwa amefariki kwenye Hoteli mojawapo ya kifahari mjini Dar-Es-Salaam kifo chake kilisababishwa na overdose ya Cocaine.

Mwisho niseme kwamba binafsi nahafiki kwa mapendekezo ya marehemu Gaddafi - Mecca na Medina ziwe nje ya utawala wa Kifalme wa Kisaudia, Taifa hilo li emulate Vatican na Taifa la Italy ili kunusuru sehemu hizo takatifu zisidhulike na adventures hatarishi za Ufalme wa Saudia, mambo wanayo yafanya ya kuchochea ugaidi na kutaka kupindua Serikali za majirani zao yatakuja kuwagehuka muda si mrefu kuanzia sasa - mimi siyo mtume wala nabii lakini sioni kama utawala wa Kifalme wa Saudia utadumu zaidi ya miaka kumi ijayo,mapinduzi yatafanywa na raia wa Saudia wakisaidiwa na watu wa nje - kwanza hata Marekani imekwisha wachoka - they won't be sorry see them go.
 
Tunaelewa Wanafiki wanatumia Iran kama chambo lakini tunawahakikishia kuwa hakuna atakayeliweza taifa Teule SAudi Arabia katika vita vitakatifu. Marekani mwenyewe anamkubali Msaudia itakuwa nyie mbilikimo msio na shukrani?
Wasyria wamekimbilia Ulaya badala ya Saudia nchi tajiri na takatifu kwa imani yao
 
Back
Top Bottom