Mbona mnaleta dharau nyie wagalatia, povu la nini na vitu vipo wazi. Hauhitaji kuwa na shahada ya chuo kikuu kuona namna nchi kadhaa zinavyojipanga kuiporomosha Saudia kiuchumi na kiusalama? ikiwemo Iran?
Mkuu jaribu kufatilia kwa karibu nyenendo za watawala wa Saudia, ukoo wa kifalme wa Saudia ndio wana finance Ugaidi mashariki ya kati na Africa kaskazini, ku advocate regime change kwenye mataifa ambayo wanafikiri ni tishio kwa Ufalme wao mfano Syria,Yemen,Iraq, Iran yaani utawala huo wa Kifalme huko in bad terms na nchi za Mashariki ya kati save Uturuki, Israel, Quatar nk
Wanachochea mifarakano ya kidini kati ya Washia na Sunni nk, Ufalme wa Saudia ni madikteita hawaruhusu Taifa hilo liwe na Demokrasia ya kweli wananyanyasa sana wanawake wa Taifa hilo na wanao toka nje kuja kufanya kazi za Uyaya.
Ufalme huo hauna goodtrack record ya kuheshimu binadamu wenzao save Wafalme wenzao au watawala wa nchi za magharibi, wana dhalau sana na viburi, dhalau zao hazijalishi kama wewe ni mwislaam au mkristo - chukulia mfano wa waumini kuangukiwa na crane/ukuta huko Mecca, hawakuonyesha kujali hata kidogo kazi ni kulahumu Wafrica kwamba ndio walihusika na stampede iliyo changia watu wengi kufa! Miaka ya nyuma moto uliwahi kuua waumini wengi, Ufalme huo bila aibu wakasingizia Waafrica kwamba ndio walisababisha moto kwa kuwa hawajui kutumia majiko ya gesi!!!!
Misaada mingi wanayo toa niya kisiasa zaidi wanaitumia kama PR ya kuzuga Dunia ili waendelee kubaki madarakani milele, nataka nieleweke kwamba raia wa Saudia na Waislaam karibu wote hawana tatizo lolote wenye matatizo ni Ukoo wa Kifalme ni wanafiki sana, kama si busara na hekima za Obama Ufalme wa Saudia na Uturuki walikuwa wanachochea vita ya tatu ya Dunia kuanzishwa nchini Syria - hawatumii busara hata kidogo.
Kwa nini nasema ni wanafiki? Huko Saudia ukikamatwa unakunywa pombe au una relationship na mwanamke out of wedlock unaweza kuhukumiwa a captial punishment!
Nilikuwa naona wana wa kifalme wakija mjini London wanajirusha kwenye ma night club, wanakunywa Pombe kali kama kawa na company ya akina mama wa barabarani wanawaganda kama luba maana wanajua wanazo!!! Wakati fulani kuna call girl aliwahi kueleza kwenye tabloid newspaper (The SUN) kwamba mwana wa Mfalme alimununulia nyumba ya kifahari za "inner London!!"
Uwezi kuamini kwamba Ukoo wa Kifalme wa Saudia unao jifanya una maadili ya hali ya juu ukiwa nchini mwao, wakitoka nje ya nchi yao wanafanya mambo ya kishenzi kweli kweli niliyo ya eleza hapo juu.
Ni ukoo unao tawala Saudia with iron fist, element ya u sadism waliyo nao ndio maana upendelea kutumia majambia kukata shingo za petty thieves/wahuni lakini linapokuja suala la ukoo wao kufanya mambo ya kudhalilisha Taifa lao wakiwa nje ya nchi, hao hawachukulii hatua yoyote wanaedelea kuwaonea raia masikini kwa kuwahukumu adhabu za kinyama wanavamia nchi masikini kama Yemen na kuua raia ovyo!
Juzi juzi hapa imekamatwa a private jet yao katika uwanja wa ndege wa Gatwick au Luton sikumbuki vizuri, wapelelezi/polisi walikuta mzigo wa COCAINE ndani ya ndege - mi sikushangazwa kwa ugunduzi huo, nakumbuka miaka ya zamani kuna mwana wa Mfalme wa Saudia alikutwa amefariki kwenye Hoteli mojawapo ya kifahari mjini Dar-Es-Salaam kifo chake kilisababishwa na overdose ya Cocaine.
Mwisho niseme kwamba binafsi nahafiki kwa mapendekezo ya marehemu Gaddafi - Mecca na Medina ziwe nje ya utawala wa Kifalme wa Kisaudia, Taifa hilo li emulate Vatican na Taifa la Italy ili kunusuru sehemu hizo takatifu zisidhulike na adventures hatarishi za Ufalme wa Saudia, mambo wanayo yafanya ya kuchochea ugaidi na kutaka kupindua Serikali za majirani zao yatakuja kuwagehuka muda si mrefu kuanzia sasa - mimi siyo mtume wala nabii lakini sioni kama utawala wa Kifalme wa Saudia utadumu zaidi ya miaka kumi ijayo,mapinduzi yatafanywa na raia wa Saudia wakisaidiwa na watu wa nje - kwanza hata Marekani imekwisha wachoka - they won't be sorry see them go.