Ahahahaha.Wakikupa Hilo basi namimi wanipe andiko linalosemwa lazima uzikwe kidini. Ni kwa wakristo kutumia biblia.
Wakuu kwema,
Kuna laki moja hapa nataka nimpe mtu akale na wana wake. Ili uipate nahitaji uniwekee aya, mstari au sura ndani ya Quran au Biblia inayoonesha mke na mume walifungishwa ndoa na kiongozi wao wa dini au walifungishwa ndoa na Mtume, nabii au Kuhani?
Sihitaji Hadithi au andiko lisiloonyesha ninachokizungumza moja kwa moja.
Nimesema nukuu itoke kwenye Biblia au Quran si kwamba siheshimu dini zingine hapana, hivi vitabu ndivyo navifahamu.
Asante.
Andiko kama halipo watu wanatumia dini kuwa control watu kama kulikuwa na ulazima mungu angesema
Yesu alikuwa anapenda sana kwenda katika harusi kuna harusi moja alikwenda kama ingekuwa lazima viongozi wa dini kuwafungisha watu ndoa ndio mungu akubali basi siku ile Yesu angefungisha lakini alifanya jambo alilopenda mwenyewe walimuuliza mama ake aliwaambia atakalofanya msikilizeni basi akageuza maji kuwa pombe hapa inaonyesha jamaa kwenye mambo ya pombe yupo poa na itakuwa alikunywa tu
Muhamad alimuoa Khadija mwanamke tajiri kama Leo tunasema zali la mental kwa maana muhamad alikuwa kapuku hana hata hela unaambiwa iyo hela ya mahari katoa khadija je huyo aliefungisha ndoa yake alikuwa sheikh gani?
Ukija kuangalia hayo matukio utakuja kugundua hakuna ya haja ya mchungaji au sheikh au padri au kiongozi yoyote wa dini kuwafungisha watu ndio maana Yesu mwenyewe kaenda katika harusi hakufungisha watu ndoa sana sana kageuza maji kuwa pombe na Muhamad kama mwenyewe kiongozi hajafungishwa na sheikh hakuna ulazima wa sheikh kutaka kufungisha watu ndo nyie wakristo na waislam mumepata wapi huo utaratibu ?
Naongeza laki moja mkuu, iwe laki mbili.
Yes hakualikwa kwenye ndoa, Kana ilikuwa harusi. Ambayo ni sherehe baada ya ndoa (lugha inayotumika siku hizi). Hiyo ndoa ya hao maharusi ilifungwa? Ilifungwa na kiongozi was dini au Yesu? Taratibu za kufunga ndoa zilikuwaje?Mimi najua tu ile tu ya Kana ambapo Bwana Yesu alialikwa na kutengeneza mvinyo
Swali la mtoa mada ni kwamba, hiyo ndoa ya kidini msingi wake ni andiko lipi kwenye biblia?Siyo kweli, mnaweza kutambulika kama mme, na mke, ila siyo wana ndoa, Ndoa ina misingi yake.
Serikali inatambua aina tatu kama siyo nne za ndoa.
1. Ndoa kidini
2. Ndoa ya kiserikali
3. Ndoa ya kimila
Sasa ukiangalia hapo utaona hakuna ndoa ya mme na mke ya kuishi mda mrefu, na ukienda kuomba cheti serikalini hutapewa mpaka mfungoshwe ndoa.
Naona wewe ndio unaleta siasa.Nimeshaisoma Biblia Yote ya vitabu 66 na Ile ya 72 zote hakuna kitu kama hicho.
Hayo ni Mapokeo tuu.
Mbinu za dini kuteka waumini wapya watakaozaliwa kwenye Ndoa
Naona wewe ndio unaleta siasa.
Kasome Mathayo 18:18 na Marko 10:9.
Hamuezi kujiendeshea mambo kama mbuzi ilhali mna utashi.
Sawa nimekuelewa ROBERT HERIEL
Lakini hoja yangu ni kwamba kutokana na vifungu hivyo. Kama kuna utaratibu wa kufanya na ufuatwe.
Ndio maana hao viongozi wako. Kwa mantiki hio basi hakuna haja ya kwenda nyumba za ibada ikiwa mambo yanafanyika inavyotupendeza.
Aki nashindwa kuwasilisha hoja. Ila nielewe kama nilivyoandika. Wewe piah uko sahihi. Mimi hoja yangu iko kuhusianisha maana hayo mapokeo yamekuwa derived kutoka vitabu vya dini, na ndio msingi wake. Ingekuwa hakuna pahala pa kutolea hata hayo mapokeo. May be ingekuwa ni batili kweli.
Basi kwa mantiki hio, hakuna kifungu ambacho moja kwa moja kinaelekeza hayo.
Ila kwa swala la ndoa kwamba wanandoa ambao hawajafungia ndoa kanisani ni wanazini, ndio nasikia kwako.
ROBERT HERIEL
Mimi nimeelewa. Shukurani.
Basi kwa mantiki hio, hakuna kifungu ambacho moja kwa moja kinaelekeza hayo.
Ila kwa swala la ndoa kwamba wanandoa ambao hawajafungia ndoa kanisani ni wanazini, ndio nasikia kwako.
ROBERT HERIEL
Mimi nimeelewa. Shukurani.
Mimi nljua unamzungumzia ndoa inayotambulika ni ya Kikristo Hapo ningesema sio.Shukrani Sana.
Hujasikia majina wanayopewa Watu walioamua kuishi kindoa?
"Wamesogezana"
"Sogea tuishi"
" Wanaishi kiharamu bila ya ndoa"
" Wanafanya zinaa, mpaka Wabariki ndoa"
Mwanamke na Mwanaume hawawezi ishi pamoja kama hawajafunga ndoa, yaani hawajakubaliana kuishi pamoja.
Tofautisha na wale wanaonunua Makahaba, hiyo inajulikana.
Lakini Biblia yenyewe imeandika, yaliyomo humu sio matukio yote yaloweza kutokea kipindi, bali yale tu yalionekana kuwa yafaa. huenda ilikuwa hivyo sema waandishi hawakuona umuhimu wa kuandika hayo.Sio tuu kifungu kinachoelekeza hayo.
Bali pia hakuna hata kisa kimoja cha manabii au makuhani au walioandikwa kwenye Biblia ambao ndoa zao zilifungishwa na Makuhani au viongozi wa Dini.
Hii inamaanisha sio sheria/sio lazima.
Ila kama MTU atapenda kufanya afanye lakini akae akijua haina tofauti na ambaye hajafanya
Kuna laki mbili kwa atakayeleta fungu la biblia linatuambia Yesu alizaliwa tarehe 25/12Wakuu kwema,
Kuna laki moja hapa nataka nimpe mtu akale na wana wake. Ili uipate nahitaji uniwekee aya, mstari au sura ndani ya Quran au Biblia inayoonesha mke na mume walifungishwa ndoa na kiongozi wao wa dini au walifungishwa ndoa na Mtume, nabii au Kuhani?
Sihitaji Hadithi au andiko lisiloonyesha ninachokizungumza moja kwa moja.
Nimesema nukuu itoke kwenye Biblia au Quran si kwamba siheshimu dini zingine hapana, hivi vitabu ndivyo navifahamu.
Asante.
Mimi nljua unamzungumzia ndoa inayotambulika ni ya Kikristo Hapo ningesema sio.
Ila hao sogea tuishi ni kweli wanazini, maana utaratibu haujafuatwa. Na kumbuka kwenda kinyume na utaratibu mliojiwekea ni ukosefu wa nidhamu, simply ni dhambi. kama lengo lao ni ndoa kwa nini wasifuate utaratibu? Watambulishane kwa jamaa na ndugu vinginevyo ni sawa na kula chakula cha wizi ndio hutaki wengind wafahamu.