Kididimo
JF-Expert Member
- Sep 20, 2016
- 4,153
- 3,800
Mashirika yetu hayauwawi na wala hayakuuwawa na CEOs. Yanauwawa na Viongozi wetu tuliowachagua. Fedha za mashirika zinachukuliwa kuimarisha chama, kuhonga uchaguzi, posho, kuinvest kwenye miradi ya kifisadi, ufisadi nk. Ilitakiwa nchi yetu ibadilishwe katiba ili mwizi wa fedha za Umma hasa viongozi wa juu kuanzia Rais,mawaziri nk wapigwe risasi hadharani kama hukumu.Kuwawachia Watanzania waendeshe nashirika hayo makubwa ni ujinga uliokithiri.
Hivi hatuelewi mashirika hayo yaliuliwa na kina nani mpaka kuwa chali?
Tumeona mwendokasi imetushinda kuendesha na sio kwa mara ya kwanza.
ATC tuliiuwa na sasa ipo njiani kuuliwa tena.
Reli ya kati na TAZARA hatujajifunza tu? Sasa tunarudia makosa yaleyale, tunawakabidhi SGR wauwaji.
Hivi lini tutapata akili?
Tumechoka na uwongo huu.
Ukitaka kujua ninachosema, nenda Namibia na Botswana ukutane na MaCEOs wa Kitanzania walivyo waaminifu na wapiga kazi!!
Kila Kiongozi anayeingia madarakani ananunua media kumsifia ananunua makunfi ya watu kupiga sound siku hizi wanaitwa chawa nk. Ila uhalisia kiasi tunauona kwenye ripoti za kina Kichere na wengine.
Kuna mtu anaitwa Kadogosa alituaminisha alichokuwa akisema Dr. Magufuli kuwa tunajenga SGR yetu kwa fedha zetu na tutaiendesha wenyewe. Ameingia Mama yetu Samia,hoja zimegeuka kuwa ni mikopo. Na isitoshe majuzi hapa kaanda kongamano kutafuta ushauri namna ya kuiendesha SGR. Leo nasikia Mwarabu kapatikana wa kuiendesha. Kadogosa aliyetudanganya bado yupo na anadunda!!!.