Hongereni sana team ya JF kwa kuendesha shindano na hatimaye kuibuka na washindi ambao mabandiko yao/mada walizoandika zitaleta chachu ya mabadiliko kwenye jamii baada ya kusomwa, kuchambuliwa na kufanyiwa kazi na wawakilishi wa serikali na hatimaye kumgusa mwananchi mmoja mmoja pale alipo.
Mfano bandiko kuhusu ukusanyaji wa kodi, kwenye upande wa mrengo chanya serikali ikifanikiwa kukusanya kodi kutokana na uwiano wa mapato (GDP) na ikatumika ipasavyo kuleta maendeleo kwa jamii haswa kuwaua maadau wakuu watatu (Umasikini, Ujinga na Elimu) na ndugu zake walioongezeka; kila mwananchi atanufaika na maendeleo yatayofanyika (uboreshwaji katika sekta ya elimu utaofua maarifa ya wananchi kujitengenezea namna ya kujimudu kimaisha badala ya kusubiri ajira kutoka serikalini na mashirika makubwa, sekta ya afya, upatikanaji wa maji safi na salama kwa wananchi wote, kukuza uchumi haswa ujengwaji wa viwanda vidogo vidogo na vikubwa, kuboresha na kukuza mifumo ya teknolojia kuendana na kasi ya dunia n.k.).
Pia, mada zote zilizoshinda hata ambazo hazijashinda, sio tuu ziachwe kufanyiwa kazi na serikali pekee la hasha, bali hata sekta binafsi, mashirika yasiyo ya kifaida na mtu mmoja mmoja kwa namna yake anaweza akaona fursa ambayo anaweza ifanyia kazi na kuweza kumkwamua kiuchumi.
Kuna msemo unasema akili ni mtu, na mwingine unasema watu hufa na utajiri wao, maana kila mmoja huwa ananamna yake ya kutafakuri na kuchambua jambo na kuleta suluhisho kwake binafsi, kwa familia na jamii kwa ujumla.
Ingekuwaje watu wengi wangekufa na mawazo yao ambayo yameleta maendeleo makubwa kwa jamii bila kuyaweka wazi mawazo hayo aidha wakayafanyia kazi wao au wengine wakayaboresha na kuyafanyia kazi...🤔
Oohoooo nimeanza kuandika mada badala ya kuchangia mada 😁, my bad.
Hongereni sana bodi ya wakurugenzi, waanzilishi wenzake na Bw. Max, mgeni rasmi, mabalozi na wote waliowezesha na kusherehesha shughuli nzima.
Mwisho wa yote, hongereni sana wafanyakazi wote wa JF kwa ujumla kwa kujitoa na kujituma kwenu kazi yenu imeonekana na binafsi nimetambua huduma yenu. Naamini nje ya mshahara kuna bahasha zinawajia kutoka kwa Bosi, kama hakuwa amewaza hili basi akisoma hili wazo anaweza akafanya kitu 😊.
Shukrani kubwa zifike kwa Muanzilishi wa JF Mr. Maxence (always humble), kongole nyingi kwako na 💐 maua yako teleee 😊.
Wasalaaam, Bi. Kasinde 🙂.