Mcqueenen
JF-Expert Member
- Nov 2, 2019
- 6,843
- 11,702
- Thread starter
- #161
Enhee hata wanaosema Mungu yupo kwasababu ulimwengu umepangiliwa inabidi uwaonyesge hii.Unapingana na ukweli kwani jiji la dar lina mpangilio gani? Wakati vurugu tupuu... Sasa wewe hueleweki Mara unasema hayupo Mara yupo Mara hujui ndo nn sasa
Mimi naona dar imepangiliwa kwasababu nikitaka kupanda daladala najua ni wapi pa kwenda na nikitaka kwenda sokoni najua ni kariakoo.,nikitaka kucheza mziki au kula malaya najua ni wapi pa kwenda kupata hiyo huduma kwakuwa kuna mpangilio fulani wa hizo huduma..Lakini weee unaona hamna mpangilio kwasababu ukiona mafuriko yanavyosomba watu, barabara zisivyopangiliwa,huduma kiwa mbali mbali na usafiri kuwa wa tabu.
Hata watu wanaosema ulimwengu umepangiliwa kwasababu kila kitu kina kazi yake kama kazi ya mti ilivyo kuzaa matunda,hawajui kuna sehemu kubwa tu ya ulimwengu ni chaos tu isiyo na mpangilio, kuna blackholes, kuna Mafuriko, kuna vimbunga,matetemeko,Tsunami,Volcanoes,Vita,Machafuko na vitu vingi random tu ambavyo havina mpangilio wowote na havina kazi yoyote.
Hata wewe ukiamka ukaenda kazini.,je watu unaokutana nao kuanzia konda wa daladala mpaka Muuza duka uliponunulia vocha,,vitu unavyofanya je vimepangiliwa au ni randomly tu na vinabafilika kila siku bila mpangilio wowote???
Jibu ni ndiyo na hapana.
Inaonyesha kuwa mpangilio sio fundamental na wala sio ishu kubwa ya kuthibitisha uwepo wa uumbaji/muumbaji