Audio: Alichosema Askofu Dkt. Josephat Gwajima kwa Kardinali Pengo

Luka 13:32 Yesu akasema, Nendeni mkamwaambie yule mbweha, leo na Kesho natoa mapepo na kuponya wagonjwa, halafu siku ya tatu nakamilisha

Mkuu hilo fungu uliloandika hapo ndivyo linavyosema kweli?
 
Goooooooooooooood Gwajima,sasa ni wakati mwafaka wa kumpa cheo cha unabii askofu Gwajima. Sasa anatakiwa kuitwa BABA MTUKUFU ASKOFU DOKTA NABII GWAJIMA. Gwajima amekua kama manabii wa zamani waliokua wanakemea uovu laivu.

Gwajima umenisaidia kumwambia Pengo sasa hata mimi hasira niliokua nayo dhidi ya pengo imeisha. Huwezi kua na akili timamu ukamuunga mkono pengo,unahitakji kua zezeta kumuunga mkono pengo.
 

Kila nikisikiliza hii Audio najiuliza huyu ni mchungaji au mtu wa vigodoro? Huu ni uthibitisho kuwa Ngwajima ni tapeli..
 
His Eminence Cardinal Pengo Elected in A Pope committee of Three Cardinals to Probe Bank Vatican

Benedict also moved to beef up a panel of cardinals tasked with scrutinizing the "organizational and economic problems of the Holy See," the Vatican said. He appointed to the panel three cardinals: Polycarp Pengo, an archbishop from Tanzania; and two Asians, Telesphore Toppo, from India, and John Tong Hong, the Hong Kong prelate who was elevated to the rank of cardinal earlier this year by the pontiff.

Kazi Zingine Anazofanya Vatican Nje Ya majukumu yake Tanzania ni :-

He has the following Curial Memberships: Evangelization of the Peoples, Doctrine of Faith (congregations). Interreligious Dialogue, Culture (councils), family and chairperson of Catholic Episcopal Conferences of Africa and Madagascar (CECAM).

Interreligious Dialogue ...ni Kamati maalum ya Papa ya kuweka mahusiano mema na mawasiliano au majadialiano na dini Nyingine Duniani Kama ..Waislamu ,buthist ,Hindu ....na hata Dini Za ASILI ....na pia Madhehebu mengine ya Kikiristo na Wayahudi
 
wee Hamis, mwache Gwajima...Mungu wake ndio atamuhukumu...halafu mbona umeishupalia hii topic km sio kutaka kuhakikisha mchungaji wa watu anazama? au unalipwa na Mbasha?

Teh Teh kwa hiyo Ngwajima kakosea au hajakosea?
 

Katika hayo majukumu aliyonayo, ndiyo maana hakuweza kudiriki kukaa kimya pindi alipoona misingi ya kanisa inataka kupotoshwa au kupindishwa. Yeye kama mshauri wa Pope, yeye kama mjumbe wa Kanisa Katoliki Tanzania katika vikao vya Vatican, yeye kama candidate wa upope hawezi kukaa kimya pindi anapoona Kanisa linakanyaga misingi yake. Na ndio maana kwenye michango yangu nimesema, Pengo ameongea kufuatana na majukumu anayopewa na Canon Law. Lakini pia katika baadhi ya michango yangu ukisoma page namba mbili nadhani kuna sehemu nimesema wazi kwamba Pengo hayupo juu ya TEC na ndio maana hakuwa na mamlaka ya kuzuia waraka usisomwe makanisani hasa katika jimbo kuu la Dar es salaam analoliongoza. Lakini kutokuwa na madaraka hayo, hakumyimi uhuru wa yeye kama Kardinali kuwakumbusha waumini na wachungaji wa Kanisa misingi ya Kanisa Katoliki. Mimi sioni kosa la Kardinali Pengo, labda uniambie kwamba alipaswa kwanza kwenda kwa Pope akamueleze hili jambo halafu ndio Pope atoe muongozo, kitu ambacho sidhani kama kinahitaji tufike huko.
 
Pengo kama mkuu wa kanisa katoliki Tanzania hawezi kuona mambo yanaenda .

Kuweka mambo sawa,Mwadhama Polycarp Kardinal Pengo sio mkuu wa kanisa Katoliki,usichanganye cheo cha ukadinary na ukuu wa Kanisa.Nchi kama Brazil,USA na hata Nigeria zina Makaldinary zaidi ya mmoja na kuna Nchi hazina kabisa Kardinali.Baraza la Maaskofu kama (TEC kwa Tanzania) ndio chombo pekee kikubwa kinachoongoza Kanisa chini ya Rais wa baraza.Hayo mengine nakubaliana na wewe.
 
Asante Gwajma nabii wa bwana, hakika we ni mtumishi kwel unayesimamia haki, kuanzia jumapili ijayo nitaanza rasmi kusali kanisani kwako maana nimeamini hapo upo utikufu mkubwa na nguvu za bwana,
 
Akili za kushikiwa mbaya sana, yani Pengo kusema wakristo wana akili timamu na wanajua nini cha kufanya waachwe waamue wenyewe kura ya kupiga ni kosa. Tatizo wengi wanakurupuka tu kushabikia bila kusoma alichosema Pengo ni kipi hasa

Bado nawashangaa wanao jiita wakristo kubariki matusi kama haya....
 
sijui amekula maharagwe yule.....ayo ni baadhi ya michambo
 

Ahsante mkuu kwa ufafanuzi. Ila nilishalitolea maelezo hilo katika michango yangu iliyofuata tangu jana. Sijafanya editing ya hiyo sehemu kwa sababu tayari watu wengi walishaqoute, hivyo kwa ajili ya kutunza kumbukumbu za JF niliona ni vyema niache kama palivyo.
 
Hahahaaa, nimechoka aisee. Eti nimempa vipande vyake, tena sijamkopesha!
[emoji23] [emoji23] [emoji23]

Teh Teh kama yuko kwenye kigodoro vile halafu huyu wanamuita Mtumishi
 
Mapendo!

kwa wale wakristo wakatoliki wenye imani thabiti tuungane kwa pamoja kumuomba mwenyezi Mungu amlipe kwa matendo yake anaye jiita mchungaji Gwajima kwa kumtusi kiongozi wetu wa kanisa katoliki Tanzania kadinali Pengo.

Kwa pamoja tuseme neno!
 
Luka 13:32 Yesu akasema, Nendeni mkamwaambie yule mbweha, leo na Kesho natoa mapepo na kuponya wagonjwa, halafu siku ya tatu nakamilisha

Kwikwikwi..naomba kwa hiyo unajaribu kusema matusi ya msanii Ngwajima yamebarikiwa? Duu wewe utakuwa una sali pale...
 
Daimaa!!! mhashamu pengo kakosea njia m naona ni haki yake kutkanwa hvo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…