kuhanda kawili
Senior Member
- Sep 19, 2014
- 164
- 33
Labda nimesahau kwa hoja ya kura, ni wapi viongozi wa dini hupigiwa kura na waumini wao? Cku zote maamuzi yao cc huwa tunaunga mkono tu!
Hili swali sijui nilikuuliza wewe..?Upumbavu hauna jina jingine zaidi ya kuitwa ni upumbavu, alichokifanya pengo ni upumbavu hivyo lazima tuukate kwa lugha zote bila kulemba.
Asante sana Nabii wa kweli na mpaka mafuta Gwajma.
Sikupendi Gwajima ila kwenye hili umenisaidia kumwambia kiongozi wangu mtukufu, potelea pote lugha aliyotumia ujumbe umefika,.....Naukimbilia ulinzi wako, mzazi mtakatifu wa Mungu, usitunyime tukiomba katika shida zetu,utuokoe siku zote kila tuingiapo hatarini, Ee Bikira mtukufu, Amina.

Tatizo watu wametekwa na siasa, hawataki kuambiwa ukweli hata kidogo. Mahaba ya siasa ndio yanayowafanya wamtukane Pengo na kuona kakosea alichokisema. Pengo kama mkuu wa kanisa katoliki Tanzania hawezi kuona mambo yanaenda kinyume halafu akakaa kimya, haiwezekani.
Kanisa halijafikia hatua ya kufanya maamuzi kwa niaba ya waumini wake, kanisa halijafikia hatua ya kulamisha watu katika suala linalohitaji haki na uhuru wa mtu. Kumwambia mtu lazima akapige kura ya hapana hiyo si sawa hata kidogo, na hata kumwambia mtu lazima akapige kura ya ndiyo nayo si sawa hata kidogo.
Mtu anapaswa kupiga kura kwa mujibu wa maamuzi na matakwa yake binafsi na si kulazimishwa. Ni sahaihi kuwaelimisha watu manzuri na mabaya ya katiba pendekezwa lakini si sahihi kuwapangia watu kura ya kupiga.

Teh Teh.
Kwa hiyo una kubaliana na mhuni Ngwajima kumwambia pengo anavishwa pampasi? Kwa hiyo Mungu wenu huwa anawaelekeza mkitofaitiana basi ni kuporomosheana matusi?
sasa wewe WAPI KATIKA BIBLE PAMEAGIZA TUMUOMBE MUNGU KWA KUPITIA MARIA. Bible imeainisha wazi YESU alivyosema yeye ni njia na uzima. sasa unataka kupitisha maombi yako kwa BIKIRA( Maria!) au Canon law ndio inaagiza hivyo. FUNGUKA
hajaikumbusha serikali kuacha kuwaambia watu wapige kura ya ndio? pengo angeitaka serikali iwashawishi watu wapige kura bila kuwataka wapige NDIO AU HAPANA, watu wajichagulie wenyewe
Teh Teh hii thread ina vichekesho sana..kwa sababu ya siasa leo hii wanao jiita wakristo wana bariki Pengo kutukanwa matusi yale na anaye jiita mchungaji mfufuaji..
Lakini kuna siku niliona hapa thread kuna mchungaji alisema kuwa wasio kwenda kuswali ni mafala..watu wali laumu sana na kusema mchungaji yule hana hekima lakini leo Mhuni mwingine kama yule ana mtukana mwenzie wana mshangilia...
Gwajima unajaribiwa,kaza kamba mtumishi...:canada:
Hiyo audio nimeisikiliza ila nimechoka.Vile vichambo vimetolewa na mchungaji? Hatari hii.
Teh Teh kumbe kutukanana ndio utumishi?
Pengo hakuwepo kwenye huo mkutano ni vizuri ukasoma vizuri hili sakata kabla ya kumlaumu na alichokisema alitanguliza kabisa kuwa ni maoni yake binafsi hivi kusema waumini wanayo akili ya kujua wapige kura ipi bila maelekezo ya kanisa ni kosa? Na kama ni kosa je unataka kusema waumini ni mambumbu hadi waelekezwe?