Audio: Alichosema Askofu Dkt. Josephat Gwajima kwa Kardinali Pengo

Kaaibisha ukristo na Kanisa Katoliki! Kanisa lenye heshima lililotulea lenye maadili mema!
Apigweeeeeeeeeeee malaika wamshughulikie Pengo arudi kundini

maadili ya kufumbia macho ulawiti wa watoto :what: kwa kuwaamisha makasisi waliotenda uovu huo na kuwapeleka kwenye parish nyingine badala ya kuwafikisha kwenye vyombo vya kisheria :what:
kweli dini ni kama brain virus😡😡
 

Hata asiposoma, za uso amekula aisee. Kilaini lazma ampe salamu.
 
Daimaa!!! mhashamu pengo kakosea njia m naona ni haki yake kutkanwa hvo

Nihaki yake kutukanwa! Sisi hatumuabudu Pengo, na mimi pia namtukana .........

Mi ni mkatoloki. Pengo kakosea acha anyooshwe tu. Hamna jinsi.

Pengo ameonyesha unafiki

Acha apate baakora

mhhhh!!! Mleta mada pole. ila palipo na ukweli usemwe tu bila kugichaficha ila sio kwa matusi. nawatakieni jioni njema. Tumsifuni Yesu Kristu.

Mtoa mada unaanzisha vuguvugu la kidini ili iweje? Kwa kiongozi wa kanisa akipotoka hasahihishwi? Tafadhali sana, call spade a spade- not a big spoon!!!

Mleta mada nina shaka kama u-Mkatoliki. Wakatoliki wanajua Mwadhama Kardinali Pengo si Kiongozi wa Wakatoliki Tanzania. Jipange upya.

Kaaibisha ukristo na Kanisa Katoliki! Kanisa lenye heshima lililotulea lenye maadili mema!
Apigweeeeeeeeeeee malaika wamshughulikie Pengo arudi kundini
Kwa msimamo wangu sikubaliani na msimamo wa Kadinali Pengo, ila siungi mkono matusi yaliyoelekezwa kwake na Ngwajima.

Kati yenu wote hapa ni nani msafi hadi mmulaumu Pengo ambaye ni binadamu kama wewe.?

Tusisukumwe na mihemuko ya kidunia kwa hukumu za Mungu.!

Asante Watu8 ujumbe wako ni mfupi ila unamajibu yote ya kibiblia na kidunia.!

Kama una muda wa kuomba ni bora uiombee nchi yako, Pengo na Gwajima watapita lakini si Tanzania
 
Last edited by a moderator:
Kikubwa ni kusamehe tu, mi nadhani watanzania Mungu ametupa utashi tunakoipeleka tz ni chaguo letu wenyewe
 
Katiba hiyo ni haramu,haitoki kwa wananchi,taratibu zilikiukwa,rasimu halali ya tume ikaachwa.Hivyo kura yake ni moja tu,HAPANA.Kupiga kura ya NDIO ni kuhalalisha kitu haramu.Pengo amehalalisha kitu haramu kwa kuheshimu mchakato haramu uliotumika.Alipaswa kukataa katiba hii.
 

Pengo hajapewa jukumu la usemaji katika kanisa la Tanzania, hata sheria na wajibu wa makardinali kwenye sheria mama ya Canon Low haijadokeza hilo, bali ni mshauri kwenye halmashauri ya Pope. Msemaji wa Kanisa Tanzania na ambaye anatambuliwa na Vatican ni Mwenyekiti wa Baraza la Maaskofu Pengo akiwa mjumbe mmojawapo katika jopo la Maaskofu Katoliki Tanzania mjumbe kama walivyo wajumbe wengine.

Kama kuna jambo ambalo Pengo anaona kwa dhamiri yake haliendi sawa na anahitaji lifanyiwe kazi, anachotakiwa ni kupeleka mapendekezo yake kwa balozi wa Vatican nchini ambaye atafikisha Vatikan na kupima kisha kushauri, na ushauri wa Vatican hautaenda kwa Pengo ila balozi wa Vatican atafikisha suala hilo kwa ofisi za baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania ambao ndio wenye wajibu na jukumu kitaifa.

Kwanza tuelewe maana ya msamiati wa neno "college" licha ya maana ya chuo (mafunzo), kuna maana nyingine pana kadiri ilivyoainishwa kwenye
Context of Catholic Cano Law.
College:
"as well as an educational institution, the term can also refer, following its etymology, to any formal group of colleagues set up under statute or regulation; often under a Royal Charter. Examples are an
electoral college, the College of Arms, a college of canons, and the College of Cardinals. Other collegiate bodies include professional associations, particularly in medicine and allied professions. In the UK these include the Royal College of Nursing and the Royal College of Physicians. Examples in the United States include the American College of Physicians, the American College of Surgeons, and the American College of Dentists. An example in Australia is the Royal Australian College of General Practitioners."
​

Hivyo college maana ilivyo tumika katika context of Canon Law inamaanisha jopo kwa kiswahili, kama jopo la mahakimu wakishakaa na kukubaliana kutoa hukumu, kati ya watatu au wanne moja akiwa kinyume haina nguvu na hawezi kujenga utetezi sababu ya uwajibikaji wa pamoja.

Hali kadhalika baraza la Mawaziri wakishakaa pamoja kama ilivyotokea wiki iliyopita na kuamua kusitisha baadhi ya safari za shirika la Ndege la Kenya hata kama kuna waliopinga, ikishaamuliwa kwa wingi katika kikao wote wanawajibika. Mrema alitimuliwa uwaziri na Mzee Ruksa sababu ya kiburi cha kutotaka kuwajibika kwa pamoja na mawaziri wenzake.

Mfumo wa kanisa Katoliki ndio kabisa uwajibikaji wa pamoja na ndio maana kanisa limeandaa vikao vya pamoja si kila mmoja kukurupuka na kuropoka ovyo ovyo. Hata ungejenga utetezi kwa nguvu zote Pengo hana mamlaka ya kutoa matamko ila tamko litokanalo na vikao vya pamoja, na kama hakuridhika basi anawajibika sababu ya taratibu za uamuzi wa wengi. Ameteleza na kanisa linamvumilia kwa udhaifu huo na anaakiwa ajirekebishe.

Tazama Pengo ameshaonyesha udhaifu wa kumeguka kutoka makubaliano ya pamoja si wakatoliki tu, ila umoja wa makanisa Tanzania. Pengo kajidhalilisha, kalidhalilisha kanisa na ameshangaza waumini kutoa tamko lililo kinyume na waraka rasmi toka Uongozi wa Kanisa nchini. Tamko lake linapingana na barua inayotoka kwenye ofisi ambayo Pengo ni mjumbe katika kikao kilichoamua waraka huo kwa waumini. Matatizo yake angeyaeleza kwenye vikao kuliko kunyamaza halafu atatoa kauli za kukanganya na kuchanganya waamini.

Nakushauri usifikiri kilichoko kichwani mwako ndicho kinachotakiwa ila angalia sheria na maelekezo ya Vatican kwa watumishi wa kanisa kwa sheria za kanisa na maelekezo ya taratibu ya uchungaji yalivyo.
 
Hadi tuipate katiba mpya,tutashuhudia sarakasi za kila aina
 
Kwa uelewa wangu mdogo naona pande zote tatu zimekosea,
Tuanze na maaskofu,dhamira yao ilikua nzuri kulingana na jinzi katiba yenyewe ilivyopatikana na ule waraka wa kichungali tuliosomewa haukua mbaya isipokua ulipotutaka tupige kura ya hapana hapo ndio kosa kwani siwote wanaina katiba hii sio nzuri, kweli hali haikua nzuri kupatikana kwa katiba hiina vitu vingi vya msingi viliondolewa na jinsi ya kuikataa nikupiga kura ya hapana, sasa maaskofu wetu wanajua wazi serikali inapiga kampeni ya ndio, wao wanakuja na kuwashawishi waumini na hapana na wakati wanajua wazi MWENYEZI MUNGU ametuagiza kitii mamlaka yoyote ya kiserikali kwani yeye ndio kaiweka hijalishi ni ya namna gani,kwa namna hio hapa maaskofu wanaipinga serikali hadharani, badala yake wangefanya kama siku za uchaguzi kuwa "tumuombe MUNGU atuongoze kwa ROHO wake mtakatifu tuwachague viongozi bora" na walitusisitizia tuombe mwongozo wa MUNGU katika kupiga kura na si tumchague nani. Sasa iweje hapa watuambie chakufanya na si kuomba kwa MUNGU?
 
maadili ya kufumbia macho ulawiti wa watoto :what: kwa kuwaamisha makasisi waliotenda uovu huo na kuwapeleka kwenye parish nyingine badala ya kuwafikisha kwenye vyombo vya kisheria :what:
kweli dini ni kama brain virus😡😡

Ndugu yangu funika kombe basi mwanaharamu apite.Hili tutaonyana kanisani ila wakristo tunawasupport maaskofu wetu na waraka ule! Mi ni mprotestant nitautafuta...... umebeba maudhui mujarabu kabisa!
 
Gwajima ni muhuni angalia zungumza yake mi napataga shida kuwaelewa hawa wanaojiita wachungaji wenye makanisa binafsi.Ifike point tuwakimbie hawa watu stress zetu za maisha ndio mitaji yao.
 
Huwa inatokea, Rais mstaafu Mzee Mwinyi aliwahi kutandikwa kofi na bwana mdogo kwa kile kilichaaminika kuwa kaenda kinyume na wenzake. Hiki ndicho kilichompata Pengo japo siungi mkono kauli aliyotumia Gwajima. Pengo aliwasaliti wenzake, haiwezekani mkubaliane kitu na mkitie sahini kisha baadaye uongee kinyume na yale mliyokubaliana.
 
Daimaa!!! mhashamu pengo kakosea njia m naona ni haki yake kutkanwa hvo

binafsi nasema pengo kakosea lakini haku stahili matusi kama alivyo fanya gwajima....una muita kiongozi mwenzako wa kiroho "mpuuzi","mjinga"...that means na wote wanao muamini yani waumini wa kanisa analo liongoza ni wapuuzi na wajinga....
 
Pengo sawa sawa tu alivyotukanwa...nam naongezea......
 
Pengo siku nyingine bora akae kimya maana kuongea ovyoovyo kuna mshushia he shima na gwajima apunge matusi
 
Gwajima ni muhuni angalia zungumza yake mi napataga shida kuwaelewa hawa wanaojiita wachungaji wenye makanisa binafsi.Ifike point tuwakimbie hawa watu stress zetu za maisha ndio mitaji yao.

Uko sahihi mkuu binafsi kwa mahubiri yake siwezi kuvumilia hata dakika kumi.

Ajabu mpaka viongozi wakubwa wa kisiasa wanamsikiliza mahubiri ya kipuuzi kabisa

Nakubaliana na wewe shida zetu ndio mtaji wao.

Nakubaliana na FaizaFoxy watanzania wengi shuleni wanafundishwa Ujinga.!
 
Last edited by a moderator:
maadili ya kufumbia macho ulawiti wa watoto :what: kwa kuwaamisha makasisi waliotenda uovu huo na kuwapeleka kwenye parish nyingine badala ya kuwafikisha kwenye vyombo vya kisheria :what:
kweli dini ni kama brain virus😡😡

huu uzi haukuhusu ndugu yangu!
 
Unapoteza muda wewe, pengo kapotoka kanunuliwa yule au iq yake ina utata
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…