Audio: Alichosema Askofu Dkt. Josephat Gwajima kwa Kardinali Pengo

Kuna siku alimchamba CAG Assad watu wakashangilia humu, cag akasema huyu ni mwehu...naona leo kibao kimemgeukia baba askofu...hatari sana.
Siku hizi umejificha wapi we bibie? Uje kule chemba tuongee basi kidogo. Mwenzio nimekumiso ati (In bambo's voice)
 

Msaliti anapewa za uso ili iwe fundisho kwa wengine. vumilia ukweli mchungu hasa baba yako anapopewa za uso hadharani. NANI ANGEMFUNGA PAKA KENGELE KWA SAKATA HILI.
 
Yesu aliwahi mwita mfalme wa nyakati zake mbweha. Maaskofu wa Catholic hawawezi kumrudi pengo maana ni mwajiri wao. Hivo Mungu huinua aliye juu yake kumwadibisha

Hamna akili nyie wote na vizazi vyenu na laana i mbele yenu nyote mnaoamini Gwajima yuko sahihi. Bwana wa Majeshu ajua fimbo ya kuwacharaza siku si nyingi usoni. Mtasambaratika kama wajenzi wa mnara wa babeli
 
akasikilize wapi; wewe mtetea hoja weka clip ya Pengo hapa tuangalie pumba na mchele

Inakuwaje hali hii kumbe hujamsikiliza. Ntajitahidi kwa faida yako na wengine niiweke hiyo clip. Ni vema tukajifunza kutafakari pindi zitolewapo kauli nzito.
 
Pumbavu,demokrasia ya wapi inasema uwaambie watu jinsi ya kupiga kura?

Du kumbe nchi yetu ina hatar kubwa namna hii ya wasio jua,
Sasa kumbe haina haja ya kupga kampen kwa maana yake kupga kampen n kumjulisha mwananchi apge vip kura na ampigie nani.
Msiwe wanafiki hapa wala tusipotezeane mda ktk nchi hii ni sawa kwa watawala kuwaambia watu wafanye nini ila ikija upande wa pili viongoz wa din wakisema mfanye hvi tayar tatizo dt machafuko. HAKUNA NCHI AMBAYO NI YA KIDEMOKRASIA HAIWAAMBII WATU WAKE JINSI YA KUPIGA KURA usidanganye raia hapa
 
Hamna akili nyie wote na vizazi vyenu na laana i mbele yenu nyote mnaoamini Gwajima yuko sahihi. Bwana wa Majeshu ajua fimbo ya kuwacharaza siku si nyingi usoni. Mtasambaratika kama wajenzi wa mnara wa babeli

Tatizo wakatolik mmezoea kuona maaskofu wenu kama malaika. sasa hapa mmoja kawasaliti wenzake HAKUNA WA KUMFUNGA PAKA KENGERE. God kainua mtumishi wake mwingine kakemea kwa 100% nyie mnaona malaika wenu kachafuliwa. MAPOVU yanawatoka. FUNGUKENI hakuna malaika anaeitwa mwanadamu chini ya jua.
 
Nami baada ya kusoma uzi huu na maoni ya wadau nimejipa tena fursa ya kuzisikiliza hotuba zote mbili za Askofu Kardinal Pengo na Askofu Gwajima.

1. Nianze kwa kusema katika hotuba yake Askofu Pengo amekili kuipokea na kuikubali barua ya kichungaji(maazimio) ya Maaskofu wenzake wa Katoliki na madhehebu mengine.
​
Sasa kitendo cha kukubaliana anapokuwa na maaskofu wenzake alafu akitoka nje kwa waumini anapinga kile alichokubaliana na maaskofu wenzake kiitenjwe hiki kitendo kama siyo unafiki na kuwadhalilisha wenzake??​
Hapa alichokifanya Gwajima ni kumweleza ukweli Askofu mwenzie Pengo kuwa anafanya UNAFIKI. Kitendo alichofanya Gwajima ni sawa sawa kabisa na kitendo alichokifanya Mtume Paulo pale alipomkemea Mtume mwenzake Petro(ambaye alikuwa mkuu wa mitume) hadharani kwa unafiki wake wa kujionesha anakubaliana na desturi za mataifa mengine ila wakitokea wayahudi wenzake Petro alikuwa anajitenga kabisa na wakristo wa mataifa mengine. Katika hili Paulo wala hakumkopesha Petro, alimpa makavu tena hadharani. Na hapa Gwajima kampa Pengo makavu hadharani.


​
2. Askofu Pengo anasema maaskofu hawana mamlaka ya kuwaelekeza waumini wao kupiga kura ya hapana kwa katiba inayopendekezwa. Tena Askofu pengo anasema watu waachwe waamue kwa dhamili zao wenyewe. Lakini askofu Pengo hasemi ukweli kuwa kwa muujibu wa biblia lililokubaliwa na maaskofu(viongozi) wote wa kanisa ni sawa na amri ya kanisa na waumini wanapaswa waambiwe kuitii hiyo amri; ingawa kutii au kutokutii ni uamuzi wa mtu binafsi na asiyetii anakuwa kafanya dhambi.​
Lakini tena askofu Pengo haendi mbele zaidi na kukemea tabia ya viongozi wa serikali kutaka watu wapige kura ya ndiyo kwa hii katiba pendekezwa. Hili kimsingi Pengo anajua ni kosa ila kaamua tu kulifumbia macho.​
Kitendo hiki cha Pengo kulalia upande mmoja kwa makusudi ni UPUUZI na USALITI wa wazi kabisa na ulipaswa kukemewa. Gwajima hili aliliona na akaamua kulikemea hadharani.
Neno MPUUZI, MSALITI au MPUMBAVU siyo tusi na Biblia imewataja watu wengi tu kama walikuwa wapuuzi, wasaliti na wapumbavu kutokana na matendo yao. Mfano ni Yuda Eskariote, Nabali na yule tajiri aliyetajwa na Yesu kuwa alikufa akaenda motoni akamwona Lazaro kufuani mwa Ibrahim.


​
3. Wote wanaosema Gwajima katukana hawataji wazi wazi tusi lipi alilotukana Gwajima zaidi ya kutoa tuhuma za jumla jumla tu. Ni kweli Gwajima katumia maneno makali sana kufikisha ujumbe wake kwa Askofu mwenzake lakini maneno hayo hayajabeba chembe yeyote ya tusi.​
Yesu aliwahi kumwita Petro SHETANI pale Petro alipojifanya ana huruma sana juu ya Yesu na kumtaka Yesu asiongelee habari ya kuteswa, kufa na kufufuka kwake; Je Yesu hapo alimtukana Petro??​
Yesu pia aliwahi kumfananisha mtoto wa mama mmoja ambaye siyo myahudi kuwa ni MBWA baada ya yule mama kumsihi Yesu amponye mwanaye; Je Yesu hapo alitukana watu wasio wayahudi??

​

Jambo moja lipo wazi. Askofu Pengo tangu mwanzo alionekana kuiunga mkono hii katiba pendekezwa, sasa kitendo cha maaskofu wenzake wote nchi nzima kukubaliana kwa kauli moja kuikataa kimemvuruga na sasa kaamuwa kutoka kivyake kwa kutoa tamko ambalo linapingana kabisa na BARUA YA KICHUNGAJI inayotaka katiba mpya ipigiwe kura ya HAPANA kama maoni yao yatapuuzwa. Hili Pengo kalifanya hadharani na hakuna anayeweza kubisha.
Kitendo alichokitenda Askofu Pengo alistahili kabisa majibu aliyopewa na Askofu Gwajima.
 
Hivi kweli kosa la Kardinali Pengo mpaka Gwajima amtukane kiasi hicho nini hasa?!!!

Mnaonaje kama Kardinali naye angekuwa mwendawazimu kama Gwajima na kujibu matusi aliyotukanwa?

Ndugu fazili unaweza kuyataja hayo matusi unayoyasema hapa??
Ni kitabu gani katika biblia au kitabu chochote kinachoyatambua maneno hayo kuwa ni mwatusi????
 
Last edited by a moderator:

Umeona sasa hapo!!!! Kwa nini Pengo anaona ni makosa maaskofu wenzake kuwashawishi waumini kuipigia kura ya hapana katiba wakati huo huo hakukemea serikali inayowataka watu wapige kura ya ndio? Huyu kwa lugha nyepesi amejitokeza kuwa kama mnafiki.

Tiba
 
Kardinali Pengo amekuwa siku zote mwiba kwa serikali na hana haja hata kidogo ya kujipendekeza kwa watu waliopo chini yake.

Kwa hiyo wewe unakubaliana na kulazimishwa upige kura ya hapana na unafurahi tu kwa jinsi ulivofilisika kiuelewa wa mambo

Wewe Fazili sasa unapindisha mambo. Hakuna mwenye uwezo wa kumlazimisha mwenzake linapokuja suala la kupiga kura kwani kwa kawaida kupiga kura ni siri ya mtu. Kwa uelewa wangu mdogo maaskofu hawajawalazimisha waumini wao kupiga kura ya hapana ila wamewashawishi waumini kupiga kura ya hapana kama serikali inavyowashawishi watu wapige kura ya ndio. Hakuna suala la kulazimishana hapa.

Tiba
 
Pengo amevuna alichopanda. Wakatoliki wengi wamechelewa kumjua mnafiki mkubwa huyu.
 
kosa hasa la Pengo ni lipi?halafu nakushauri irudie hiyo audio,halafu huyatafakari hayo maneno ungekuwa unatamkiwa wewe,sijui kama ungetoa hoja hii

Nikwenda kinyume na makubaliano walioafikiana, kazi ya viongozi wa dini ni kuonyesha njia impasayo mtu kufuata na sikumpa option ya kufuata black is black and red is red na ndicho anachokizungumzia Gwajima.

Tatizo la pengo ni mnafiki sana unakumbuka issue ya mlipuko wa bomu arusha alichokisema?
 
Audio ya pengo amesema

mimi ni nani mpaka kulipinga tamko la maaskofu.. Ila hakuna mtu mwenye mamlaka ya kuwaambia watu wakapige kura ya hapana..mungu mwenyewe ametuacha huru.. Kuwaambia wakristo wote kuwa wakapige kura ya hapana ni kuwafanya kama watoto hawajui kitu

Pengo hajakosea Maana Anajua Demokrasia.. Kuna Wakristo Ni Die hard wa Ukawa na Kuna Wakristo ni Die hard wa CCM ... Sasa kuwashurutisha Wakristo wote wakapige kura ya Hapana Ni kuweka Utengano wa kitaifa na Kidini.....

Watu waachwe Huru kama Mungu Mwenyewe alivyotuacha Huru bila kutushututisha na tunachagua tupendavyo....

Mwenye Hekima Atamuelewa Pengo Kasemaje wenye Mihemko Hawataelewa chochote..... OVER
 
Mwenye bongo iliyekwenda shule atakuelewa mpuuzi kama Pengo hatakuelewa nimependa ulivyodadavua...
 

Umechanganya madesa kazi ya kiongozi wa dini ni kuonyesha njia mpasayo mtu kuifuata si option ya kuchagua ila mmlaka ya kuchagua njia gani aifuate ipo katika mtu mwenyewe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…