Audio: Alichosema Askofu Dkt. Josephat Gwajima kwa Kardinali Pengo

Audio: Alichosema Askofu Dkt. Josephat Gwajima kwa Kardinali Pengo

Kubali kuwa Pengo ni Mnafiki na Msaliti kwa kuweka mbele mahaba yake na CCM badala ya kusimamia Matamko na mambo yenye tija na kanisa.

Hilo la unafiki, usaliti na mahaba kwa ccm sina utaalamu nalo kwa kweli, inategemea unaliangalia kwa mrengo gani na tunaweza kuwa na maoni tofauti...na binafsi sioni vibaya kuwa na maoni tofauti katika hilo...Lakini hili la kauli za gwajima ni HAKIKA ni matusi, ni kashfa...ni ushetani..Ni kukosa hekima na udhalilishaji kwa binadamu mwenzake...Ni jambo linalopaswa kupigwa vita na wote wenye akili, wenye kujitambua.. wenye kutafakari mema...wenye kuitakia mema nchi hii.
 
Uzi huu unazungumzia alichoongea gwajima kwa askofu Pengo. Na hoja ya msingi hapa ni endapo kauli alizotoa gwajima dhidi ya askofu Pengo ni matusi au sio matusi. Wewe ndio unataka kunitoa nje ya mada ndio maana nakushauri uweke bayana msimamo wako katika hili kabla hatujatoka nje ya mada. na swali lako ni jepesi sana ukipenda unaweza hata kufungua uzi mpya tukaongea kiundani kuhusu ujinga, upumbavu, kashfa, kejeli, matusi. n.k. kwa sasa tuutendee haki uzi huu. Niko makini mkuu

Nilishaweka huko nyuma mkuu kuhusu matamshi ya Gwajima. sikutaka kukutoa ila nilitaka tufikiri nje kidogo ya mtazamo wa kawaida kama alichokisema gwajima ni matusi au la kwa kuangalia matamshi yaliyowahi kutamkwa na watu muhimi katika maisha yetu na tuseme kama pia ni matusi au la.
 
Hilo la unafiki, usaliti na mahaba kwa ccm sina utaalamu nalo kwa kweli, inategemea unaliangalia kwa mrengo gani na tunaweza kuwa na maoni tofauti...na binafsi sioni vibaya kuwa na maoni tofauti katika hilo...Lakini hili la kauli za gwajima ni HAKIKA ni matusi, ni kashfa...ni ushetani..Ni kukosa hekima na udhalilishaji kwa binadamu mwenzake...Ni jambo linalopaswa kupigwa vita na wote wenye akili, wenye kujitambua.. wenye kutafakari mema...wenye kuitakia mema nchi hii.

Kijana umeshakosa mwelekeo tayari.
Mwenye kuitakia nchi hii mema lazima awe mkali kukalipia kwa watu au kikundi chochote kinachotaka kupitisha masuala binafsi ya kidini kuingia katika sheria za nchi hii.

Tanzania ni Secular state HAPANA dini wala taratibu za ibada kuingia katika sheria na katiba ya nchi hii.

Na Pengo kwakua ameonyesha kutokua na msimamo alichoambiwa ni sahihi kabisa, sasa kama wewe unatafsiri ni matusi basi alianza kutukanwa Herode kwa upuuzi kama huu. Yesu alimtukana Herode na Herode alikua mkuu wa Jimbo la Nazareth itakua Pengo?

Labda kabla hujamtetea ukamuulize aliyoyafanya alifanya kwa faida ya nani? Na nani aliyemtuma?

Watu wajinga na wasaliti hawaambiwi kwa kuchekewa na kubembelezwa ni kuambiwa maneno magumu yatakayofanya wajutie maamuzi yao wanayoyafanya.
 
Jamaa anasaka sadaka kwa kick ya Pengo :smile-big:

Ni kweli kabisa...gwajima anatafuta umaarufu kupitia mgongo wa askofu Pengo..Maaskofu waliotoa tamko wameskia alichosema askofu Pengo lakini wametulia.Mwenye hekima hutulia na kutafakari jambo kabla ya kulitolea majibu. Huyu na kiherehere chake kakurupuka kama mwendawazimu na kuanza kumwaga matusi. Naona ameona hiyo ndio njia yake ya kurudisha washabiki baada ya kudhalilika kwa kashfa ya kutembea na mke wa mtu na madawa ya kulevya..hajui kuwa ndio anazidi kujidhalilisha. Hizi njaa hizi!... mtu anajichetua na kuwa kama mwehu kusaka sadaka za watanzania maskini. Shame!
 
Nilishaweka huko nyuma mkuu kuhusu matamshi ya Gwajima. sikutaka kukutoa ila nilitaka tufikiri nje kidogo ya mtazamo wa kawaida kama alichokisema gwajima ni matusi au la kwa kuangalia matamshi yaliyowahi kutamkwa na watu muhimi katika maisha yetu na tuseme kama pia ni matusi au la.

Kama ulishaweka ni vizuri ukarudia mkuu au quote. Ni wazi sijaona uzi wako kuhusu hilo
 
MAMBO MUHIMU YA KUJIULIZA KUHUSU SUALA HILI;

1. Je ni kweli Bishop Pengo alikuwa kwenye kikao cha maaskofu na alisaini hiyo hati (waraka) wa maaskofu kuhusu maoni ya katiba kadri ya madai ya "Pastor" Gwajima?
2. Je kama alisaini hiyo hati je ilikuwa ni halali au sahihi kwa yeye tena kuja kutoa msimamo wake binafsi unaopingana na msimamo wa pamoja wa maaskofu kwenye vyombo vya habari?
3. Je kama kweli hakuwepo kwenye hicho kikao lakini kikao hicho kiliwakilishwa na maaskofu katoliki je hawakuwa wanaliwakilisha kanisa ambalo yeye ndio kiongozi wake? hakuwatuma?
4. Je Pastor Gwajima alikuwa na uhalali wa kumdhalilisha kiongozi mwenzie wa dini jukwaani kwa kiwango hicho hata kama Pengo alikosea?

Asanteni.
 
Kijana umeshakosa mwelekeo tayari.
Mwenye kuitakia nchi hii mema lazima awe mkali kukalipia kwa watu au kikundi chochote kinachotaka kupitisha masuala binafsi ya kidini kuingia katika sheria za nchi hii.

Tanzania ni Secular state HAPANA dini wala taratibu za ibada kuingia katika sheria na katiba ya nchi hii.

Na Pengo kwakua ameonyesha kutokua na msimamo alichoambiwa ni sahihi kabisa, sasa kama wewe unatafsiri ni matusi basi alianza kutukanwa Herode kwa upuuzi kama huu. Yesu alimtukana Herode na Herode alikua mkuu wa Jimbo la Nazareth itakua Pengo?

Labda kabla hujamtetea ukamuulize aliyoyafanya alifanya kwa faida ya nani? Na nani aliyemtuma?

Watu wajinga na wasaliti hawaambiwi kwa kuchekewa na kubembelezwa ni kuambiwa maneno magumu yatakayofanya wajutie maamuzi yao wanayoyafanya.[/QUOTE]

Kwahiyo unasupport matusi! wewe ni Mkristu? Hivi mfano askofu Pengo akijibu kwa style ya gwajima na maaskofu wengine wakaingilia wakawa wanajibizana kwa mipasho na matusi..kuna mtu ataendelea kwenda kwenye nyumba za ibada? Biblia inatufundisha kumrejesha aliyepotea kwa upole..Hizi lugha zingine zinafaa kuachiwa wanasiasa. Kama gwajima ana uchungu sana mbona hamtukani Raisi aliyewaambia wananchi wapige kura ya ndio? Mbona anachagua wa kumtukana? gwajima ni mnafiki.
 
Kama Oil chafu imeisha mwagwa na mnahisi gari liko vizur sasa ya nini kila mara mnazungumzia tena Oil hiyo, Zito c kashawaachieni chama chenu sasa ya nn maneno?
 
kumbe kardinali PENGO alielekezwa na Mizengo PINDA Kutoa Tamko lake.

Wadau

Kuna mambo yanatimka na kuendelea huku Maofisini kwetu, yanakera, yanachefua na si ya kizalendo hata kidogo, na kila mpenda haki na amani lazima ayapinge kwa nguvu zake zote. Nimeona niyachomoe yaende hewani hivi hivi.

Jana Kumekuwa na Vikao vya ‘wakubwa selikalini ’ Kujadili tamko la Gwajima kwa Pengo, waziwazi wakubwa hao wametueleza kwamba wameelekezwa na Mizengo Pinda wamfuatilie Gwajima, kuanzia Usajili wa kanisa lake na sijui wamepanga nini zaidi. Maafisa Polisi wameagizwa kuanza ‘kazi’ ambayo hatujaijua bado kuhusu Gwajima, na maelekezi Yote yametoka kwa waziri Mkuu, Mh Peter Kayanza Pinda

Chanzo cha karibu kabisa na nyumbani kwa Pinda kinasema Pinda na Kardinali Pengo ni marafiki, na wamesoma Seminary pamoja, na wote ni wafipa. Chanzo kimesema bila kuogopa kwamba kumekuwa na kutembeleana kwa Pinda na Pengo kwa Mazungumzo, na chanzo kimetema wazi kwamba ni Pinda ndie aliye muelekeza Kardinali Pengo kwenda kinyume na matamko ya maaskofu Wote kwenye waraka ambao hata yeye Pengo aliusaini na kuukubali.

Chanzo kinasema pia kwamba Ni Pinda aliye mshawishi Pengo awaasi maaskofu wenzake na watu wa makanisa Yote. Chanzo kinadai binafsi kilikasirishwa sana na Kitendo cha Waziri mkuu kumnajisi kardinali pengo ambaye alikuwa na sifa kubwa ndani na nje ya nchi yetu.

Taarifa hizi ambazo zimesambaa kwa maaskofu wote wa Kanisa Katoliki wamemlaani sana Pinda, kitendo cha Pinda kumuharibu Pengo, na Kumfanya Pengo kama mtoto wa kuasi maamuzi yake mwenyewe kimewakera sana.

Baraza la maaskofu wa Katoliki linangoja kumuuliza Pengo, Ni kitu gani huyu Mfipa mwenzake alimlewesha kiasi cha kuropoka maneno hatari. Tamko la Gwajima kumrarua Pengo lilikuwa kumrarua Pinda ambae amekuwa mtoa maelekezo yale, sasa Pinda amekuwa Mbogo, ameanza kama chizi Kumsakama Gwajima, na Kutuharibia utaratibu wa kazi zetu za kila siku serikalini.

Baadhi ya maofisa wetu kwenye kikao walimjibu Pinda kwamba Askofu Pengo kashambuliwa na Askofu Gwajima waachwe maaskofu wapambane wao kwa wao bila kuweka mkono wa serikali kwenye mambo ya dini. Matamshi hayo yalionekana kumkera sana Pinda aliyemtishia nafasi yake.

Kuna chanzo kingine cha karibu sana ambacho kilirekodi kikao cha Pinda na Pengo. Kadiri ya sakata linavyoendelea kaeni mkao wa kuona Mengi. Kanisa la Gwajima jiandaeni kupokea ‘mambo’ kutoka kwa Pinda.
Natuma kama nilivyopata.
 
Hapana...Huyu amejidhalilisha mwenyewe..na kanisa lake analolisimamia. ni mfano hai wa wachungaji feki.. Kwa style hii.. Sidhani kama Flora alisalimika.

Huyu jamaa sjui kasomea wapi hamna kitu kichwani mwake, anakurupuka kelele nyingii..akelee mtoto na flora ndo anachokiweza dini hamna pale ni mwanamziki wa taarabu tuu.
 
sikupenda jinsi gwajima alivyowasilisha ujumbe kwa pengo,lakini pengo naye anapenda publicity yeye aliona shida gan kutoa mawazo yake akiwa na wenzie hko kwny vikao TEC? hii inanifanya niamin kwa sasa inaonekana hana saut mbele ya maaskofu wenzie wa kikatoliki,ndo mana akaamua kutoa maon yake binafsi hadharani.

Hakuwepo kwenye Vikao Hivyo... hii inadhihirisha Umekurupuka Tu kucomment bila Kusikiliza Audio ya Pengoo...

Acheni Mihemko muwe mnafuatilia hata Alichoongea.. Si mtu anaanzisha mada Tu unakomment
 
Wewe umeanza kuzungumza UTUMBO, UPUUZI NA UTAAHIRA!

Wakatoliki wanaingia sehemu gani hapo? Kosa la Pengo sio la wakatoliki ndio mana maaskofu wengine wa kikatoliki walikubaliana na kuweka saini katika Tamko lao.

Acha kuleta mambo ambayo hayapo, hii ni issue binafsi ya unafiki wa Pengo na sio wakatoliki.

Bila Pengo kuruhusu Hilo Tamko kwenda Katika Majimbo Lisingeenda... Tatizo Hamjamuelewa Pengo
 
MAMBO MUHIMU YA KUJIULIZA KUHUSU SUALA HILI;

1. Je ni kweli Bishop Pengo alikuwa kwenye kikao cha maaskofu na alisaini hiyo hati (waraka) wa maaskofu kuhusu maoni ya katiba kadri ya madai ya "Pastor" Gwajima?
2. Je kama alisaini hiyo hati je ilikuwa ni halali au sahihi kwa yeye tena kuja kutoa msimamo wake binafsi unaopingana na msimamo wa pamoja wa maaskofu kwenye vyombo vya habari?
3. Je kama kweli hakuwepo kwenye hicho kikao lakini kikao hicho kiliwakilishwa na maaskofu katoliki je hawakuwa wanaliwakilisha kanisa ambalo yeye ndio kiongozi wake? hakuwatuma?
4. Je Pastor Gwajima alikuwa na uhalali wa kumdhalilisha kiongozi mwenzie wa dini jukwaani kwa kiwango hicho hata kama Pengo alikosea?

Asanteni.

Umesikiliza Audio yake?
 
Pengo alistahili kubabuliwa tena Gwajima amemstahi sana!! Mnafiki anaambiwa mnafiki hali kadhalika mpuuzi!
Hatuwezi kulea maradhi ya wanafiki eti tumwambie pengo chumbani kakosea!
Anababuliwa hadharani kama alivyochemka hadharani!

Haya Amelipwa nini huyo Gwajima........ Anatofauti Gani na Redio inayopiga Tarabuu na kutumbuiza Jukwaani
 
Hata kama alikosea Gwajima hakuwa na haki ya kumtukana;
Je, hivyo ndivyo kuongoza roho za watu ili wafike mbinguni?

Gwajima ni mhuni tu.
 
Gwajima kumtukana Pengo kwa ajiri ya Katiba mnaona sawa! kusema kwamba watu watumie utambuzi wao mnaona kakosea! Upumbavu wa akina Mbowe! Mbatia na Lipumba kukimbia BMK hamuuoni? hii ni hatari na ni upumvavu wa hali ya juu kabisa yaani walevi, wazinzi na wauza madawa ya kulevya ndiyo wenye thamani katika ulimwengu wenu? Dunia iko mwisho.
 
Ufahamu wako ni very much below average ndo maana unawatukana viongozi wa upinzani. Ebu rudia tena post yako. Sidhani hata kama utaielewa.
 
.....Pengo ni mnafki sana, kama analijua hili kwanini asingegoma kusign ktk huo mkataba baada yake akasign kisha akaja kusema pembeni mambo ambayo no tofauti na mkataba.
.....Viongozi wa kiroho (Maaskofu) siku zotr huwa wanatutakia mema, mimi binafsi kwa taifa letu lilipofikia naona ni vema kwa wao kuungana na kupiga kura ya HAPANA.
.....Na ifahamike kwamba, Wakristo wengi au Watanzania wengi hawajaisoma Katiba Ipasavyo, kama wao wameiosoma na wameona haitafaa kwa Maslahi ya Watanzania ila ni kwa maslahi ya CCM ni vema wakatuambia ukweli na tuikatae.
.....Pengo najua ameona madhaifu ya KATIBA na yeye kama kiongozi alipaswa kusimama wima na kupinga vikali juu ya hiyo katiba, sio kuanza kuwa na maamuzi mepesi mepesi wakati ikipita Maisha ya Watanzania yatakuwa mabaya zaidi.
.....Asilimia kubwa ya maoni ya Watanzania yametupwa nje, sasa hiyo ndo Katiba ambayo tunaitaka? Mimi nasema kwamba Hakuna Mtanzania mwenye uchungu na nchi yake ambae ataikubali hii Katiba, hata mimi ninhekuwa na uwezo wa kupita kila mahali na kusema watu waikatae katiba mpya basi ningefanya hivyo.
.....Pia tutambue kuwa waliomuona Pengo ni mpuuzi sio Gwajima tuu, Chama cha Maaskofu Tanzania kipo na watu wengi, nadhank wote wamemshangaa Pengo na wakaamua kuwa na maneno ya pembeni, heri Gwajima katoa yake ya Moyoni.
.....Naungana na Gwajima kuwa Pengo ni mbweha tuu.

Chama cha Maaskofu kinaitwaje mkuu, ni vema tukayajua na haya ili mjadala uende vizuri. Karibu.
 
Back
Top Bottom