Awamu ya Rais Samia ndiyo awamu iliyofeli kuliko awamu zote na kufanya wananchi kujutia zaidi uongozi huu

Miradi gani "mingi" ya kimkakati iliyoanzishwa..?
 
Unajua kipimo cha CT SCAN ni shilingi ngapi!?
Na hospitali ngapi zina huduma hiyo maana ulivo punga umejikita kusini tu.

Chawa promax hebu tupe na hospital zingine zenye hiyo huduma na ni bei gani kwa kipimo.
Kabla ya Rais Samia ulikuwa unaijua hata CT Scan wewe?

Samia kafunga CT Scan hospital zote za Mikoa ambapo kabla hazikuwepo isipokuwa hospital za Kanda tuu.

Swala la gharama ni issue nyingine ila wahitaji wanapata Huduma

View: https://twitter.com/wizara_afyatz/status/1702728608739910044?t=cpVnWoih_vZTFHSDgM-1hQ&s=19
 
Mnashindwa kuelewa kuwa awamu hii ya sita imeingia madarakani kipindi dunia ikiwa inahangaika na madhara ya vita kati ya Russia na nchi za NATO huko Ukraine. Hivyo mambo ya bei za bidhaa kuendelea kupaa, umeme kukatika katika, dollar kuadimika, maji kukatika katika na kadhalika, ni matokeo ya hiyo vita ya dunia inayoendelea hadi sasa. Pia mabadiliko ya tabia nchi.

Kila awamu ilikuwa kwenye mazingira tofauti, hivyo huwezi kuzilinganisha kirahisi namna hiyo. Mazingira ya awamu hii ni magumu kuliko ya awamu zote. Imepambana na kufanikiwa kwa kiwango kikubwa ukilinganisha na hali ilivyo kwa nchi zingine za Afrika hususani majirani zetu Kenya. Inawezekana kuwarudisha baadhi ya vijana kama Nape na January kumsaidia katika mapambano haya ya kiuchumi na kuwaondoa baadhi ya wazee kama Kabudi na Lukuvi halikuwa jambo sahihi sana, lakini yeye ndiye anajua na amekuwa akifanya mabadiliko ya mara kwa mara. Tuko vizuri, nchi imetulia, ajira za kumwaga, demokrasia imeshamiri, miundombinu inajengwa, viwanda vinajengwa, siasa zinaendeshwa kistaarabu isipokuwa wachache kama TL wanakiuka kidogo na kurudishwa msitarini etc.
 
Unapoteza mda wako bure
 
Duuuh umesahau na ajira hakuna. Yani mifumo ya kutengeneza ajira imekufa yote while vigogo wananeemeka kwa kununua mavitu ya thaman kama magar, mabasi na mengineyo
 
Duuuh umesahau na ajira hakuna. Yani mifumo ya kutengeneza ajira imekufa yote while vigogo wananeemeka kwa kununua mavitu ya thaman kama magar, mabasi na mengineyo
Labda mna laana sio bure.Ila sio mbaya maana mtu atahukumiwa na ulimi wake.

Hakuna awamu watu wamepata Ajira kama awamu ya 6 za government na private sector.

Yaani uchumi unavyokua hivi harafu unasema hakuna Ajira? Uko Tanznaia au Burundi?

Mwisho usipopata kazi awamu ya 6 hutokuja kupata kamwe,shika hiyo itakusaidia.
 
Kama haujui me ni medical personel, ndo maana nikakuuliza wewe chawa wa mama unafahamu bei ya kipimo cha CT SCAN!?

Je hiyo bei ya kipimo ni afordable kwa mtanzania!?.
 
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚Chawa kama chawa. Kila post ambayo iko against j serikali yako umo
 
Kama haujui me ni medical personel, ndo maana nikakuuliza wewe chawa wa mama unafahamu bei ya kipimo cha CT SCAN!?

Je hiyo bei ya kipimo ni afordable kwa mtanzania!?.
Kwani kuwa medical personnel kunafanya wewe usiwe hater?

Hoja sio gharama za CT scan hoja ni kwamba CT scan kabla zilikuwepo?

Hata gharama za kusafisha Damu kwani hujui kwamba zimepunguzwa by half?
 

View:
Kwani kuwa medical personnel kunafanya wewe usiwe hater?

Hoja sio gharama za CT scan hoja ni kwamba CT scan kabla zilikuwepo?

Hata gharama za kusafisha Damu kwani hujui kwamba zimepunguzwa by half?
Mjinga haujui lolote lala mbele huko, nyokooo.
Kaa kimya you know nothing, kazi kusifia tu kumbe haujui hata unachosifia kina umuhimu gani kwa raia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…