Azam Media Kutopeleka Vifaa vya matangazo tarehe 15.06.2025

Azam Media Kutopeleka Vifaa vya matangazo tarehe 15.06.2025

Inasemekana wameandaa barua kuidai fidia bodi ya ligi kwa hasara waliyopata tarehe 8 na endapo bodi itashindwa kulipa fidia ndani ya siku 7 basi mechi namba 184 kati ya Yanga na Simba haitarushwa.
Ligi ilikuwepo kabla yao, kwanza kutakuwa na mvua so haina shida sana maana wao na mvua ni maji na mafuta
 
Hakuna hio kitu kama Yanga wangekua na makosa wasingepata kiburi cha kukataa kucheza mechi , subiri utaona hii kitu inaondoka na mtu
Hakuna mpuuzi yeyote wa kuingilia mpira, ila kwakuwa nyie wenye akili wawili tu ndio mnapenda kukubali kila mnachoambiwa, rudi kwa BM3, Kagoma ndio utajua utopolo ni majinga
 
Hizi ni propaganda tu za Yanga. Azam haiwezi kususa kurusha matangazo kisa walileta vifaa uwanjani halafu mechi haikuchezwa.

Hata hiyo hoja ya usumbufu kwa wateja wao siyo nzito kihivyo maana hawauzi kifurushi cha mechi moja, na watu walinunua vifurushi na hawakuwarudishia. Ile barua ilikuwa tu kuonyesha wanawajali wateja wao ila kibiashara Azam hawajaumia kabisa.
Akili kubwa
 
Yaaaan Azam huyu agomeee?? Wewe unafikiri tukiotoa ligi azam anabaki na nini?
 
Unafikiri ni jambo jepesi kma unavyochuchuma kuharisha!
Punguza kuwaza mambo ya ajabu,ile ni biashara watu wakishindana mkataba unavunjwa Kwa hela tu,kampuni nyengine inaingia kazini,nakuhakikishia hata leo hii azam tukimvunjia mkataba hatumalizi week anapatikana mtu mwengine wa kurusha mechi kama kawaida
 
Mashabiki wa mpira mna nongwa sana, mwamba unaandika as if na wewe una cheo bodi ya ligi 😆😆, kwamba azam akizingua chap mnavunja mkataba mnampa mwingine.

Kama mwenye nyumba kuhamisha mpangaji wake na kumpata mwingine chap kupitia madalali.
Mkuu sihusiani na bodi ya league nahusiana na wapanga bajeti na mikataba ya kimichezo,nakuhakikishia azam ananufaika zaid na hayupo tayari Hilo litokee,ni sauti Moja anarusha mechi live
 
DSTV huyu huyu aliye hati hati kung'atuka na kuwaacha Canal au unajitekenya na kucheka mwenyewe?

Ubinadamu ni kazi/The humanity is work.
Canal anadeal na nchi zinazoongea kifaransa
Dstv sub sahara ikiwemo hizo juu
Be in sport kwa nchi za uarabuni wakimo na rt
24sports kwa uingereza na nyingine nyingi
 
Mkuu hata kama Tanzania ni nchi maskini lakini hatujafkia huko,eti kushindwa hata kulipia hata DStv,mpira hii nchi unapendwa
Dstv madai yao sio pitch tu hata majukwaa ya kusetia camera ni issue kwa viwanja vya bongo otherwise ikae moja ama tatu tu
 
Mkuu sihusiani na bodi ya league nahusiana na wapanga bajeti na mikataba ya kimichezo,nakuhakikishia azam ananufaika zaid na hayupo tayari Hilo litokee,ni sauti Moja anarusha mechi live
Sawa, maana hata kuitangaza hajaanza bado. Ngoja tusubiri.

Yaani utadhani huyo azam mnamlipa na yeye haweki kitu.
 
Inasemekana wameandaa barua kuidai fidia bodi ya ligi kwa hasara waliyopata tarehe 8 na endapo bodi itashindwa kulipa fidia ndani ya siku 7 basi mechi namba 184 kati ya Yanga na Simba haitarushwa.
Umeanza na neno INASEMEKANA

NYAMBAFFF KABISA
 
Hana hiyo jeuri, huduma yake anawezapigwa chini vizuri tu tukampa mkataba DStv aonyeshe ligi ya ndani halafu tuone nani atapata hasara zaidi
Hiyo ndio maana halisi ya UBAYA UBWELA ajichanganye aone
 
Punguza kuwaza mambo ya ajabu,ile ni biashara watu wakishindana mkataba unavunjwa Kwa hela tu,kampuni nyengine inaingia kazini,nakuhakikishia hata leo hii azam tukimvunjia mkataba hatumalizi week anapatikana mtu mwengine wa kurusha mechi kama kawaida
Unavyoongea kama ni rahisi sana.... Unajua thamani ya mkataba wa Azam ulivyo? Unajua gharama ya kuvunja mkataba huo?. Tff wanazo hizo pesa?, acha kurahisisha vitu kwa kutype tu.
 
Back
Top Bottom