Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hamia startimesKama walionesha maudhui ya namna hiyo hawakufanya jambo sahihi na kama nyinyi wenye Imani yenu mlikaa kimya basi mna ujinga sana
Sawa mkuuHujui maana ya ukweli pia hujui maana ya haki?
Basi una safari ndefu
Karibu mwaya kila siku wanamapocho pochoNakuja mama hiki kisimbuzi chao nakiweka sokoni nilinunua kwa ajili ya ligi kuu lengo kubwa
sasa nitaangalia bandani tu
Achana na tamthilia tazama vipindi vingineJana nimerudi nimechoka nikafikia kujitupa tu kwenye kiti hakukuwa na mtu sebuleni ila TV ilikuwa inaonesha chaneli ya Azam 2
Macho yangu yakaona kipande kimoja kwenye tamthilia ya kituruki bila shaka inaitwa Alpasalani nadhani, Sasa Kuna Binti alikuwa Yuko kwenye mtego na viongozi wa utawala mwingine inaonesha huo utawala una Ukristu maana askari wake wana misalaba kwenye mavazi yao.
Sasa hawa askari aisee ni midebwedo vibaya mno yaani mwanamke moja anaua infidels (humo wanaita wadhalimu) zaidi ya 20 mbele ya kiongozi wao halafu Yuko pekeake na bado anaendelea kusurvive!? Duuuh ina maana hao ni wanyonge kiasi hiko? Halafu mule inaonesha waislamu ni watu wema sana na wakristu ni watu wenye Roho mbaya mno na hii chanel secular ila inabagua Imani moja na kuipendelea ingine.
Ututuki ni nchi ambayo raia wake wengi ni waislamu hivyo ni sawa kuwa na maudhui kama Yale, Sasa Tanzania hii ni multi religion county huwezi kuwa na maudhui hayo hayo tu kila siku ya kukandamiza Imani moja na kuipendelea ingine kulikuwa na;
Zote hizi maudhui ni yaleyale.
- Ertugrul
- Ottoman
- Barbarossa na Sasa ni hii
- Alpasalani
Azam tv badilikeni, hela tunalipa sisi lakini mnatutibua nyingi makusudi kabisa.
Na huu mwezi nitaacha kulipia hiki kisimbuzi kama ni ligi kuu nitaangalia bandani na kisimbuzi nitanunua cha startimes.
Azam tv mjifunze kwa wenzenu, mbona wao wanajua mipaka yao.
Mnakera bwana aah!
Leo sasa nimeamin 100 mshangazi ni libazaziUnaweza kusafisha mtaro?
Leo sasa nimeamin 100 mshangazi ni libazazi
Wakristo wengi tu wanapenda hzo tamthilia na mara nying huwa upande wa waislamu(steering)Mm n mkristo lakin nilikuwa naipenda sana ottoman mpaka Leo napenda kufatilia mana n story ya kweli
Mods wameedit andiko langu ndio maana hujanielewa.Hueleweki
Unamaanisha crusaders sio? Waliua pia wakristo, na ile ni historia ya kweli, crusader ni kama unavyoona Nazi, Fascists ama Zionism ni movement tu za watu weupe ambao walikua wakijiona superior na wana haki ya kutawala dunia, na wengine si viumbe vikamilifu.Shida sio kuwa na maudhui ya kidini naomba unielewe ndugu yangu katika Imani
Shida ni kupambanisha Imani za watu, moja kuichora kama Imani safi na nyingine kuwaita wadhalimu hii si sawa, na tena wanatumia hadi nyenzo takatifu za Imani nyingine kudhihaki
Mbona bongo movie zipo movie nyingi tu ambazo huegemea desturi za kiislamu lakini bila kukashifi Imani ingine? Movie za madebe na hata Mohamed nurdin nyingi tu ziko hivyo