Uchaguzi 2020 Azimio: Bunge la Marekani laisihi Serikali ya Tanzania na wahusika wote kuhakikisha Uchaguzi utakuwa Huru na wa Haki

Uchaguzi 2020 Azimio: Bunge la Marekani laisihi Serikali ya Tanzania na wahusika wote kuhakikisha Uchaguzi utakuwa Huru na wa Haki

Magufuli aliwaambia wakurugenzi.

"Nimekupa kazi.
Ninakupa mshahara.
Nakupa posho.
Nakupa Nyumba
Nakupa Gari.

Bado unaenda kumtangaza mpinzani"
 
Ukiona wanakufuatilia juwa uko kwenye target yao.

Bunge la Amerika kukaa pamoja na kuweka azimio juu ya uchaguzi wa Tanzania ni habari ya kujivunia mkuu, inaonesha tuko ligi kubwa. Au wewe unachukulia vipi bunge la Amerika kuacha shughuli zake na kukaa kujadili na kuweka azimio juu ya uchaguzi wa Tanzania?..Eti unaonaje hiyo hali mkuu? levol ya nchi yako iko juu sana ama vipi?
 
Uchaguzi huu unawezi kutufanya tuwe kama Zimbabwe au tubakie kama Tanzania
 
Azimio la bunge la Marekani liliotolewa tarehe 17/09/2020 lenye jina la "Urging the Government of Tanzania and all parties to respect human rights and constitutional rights and ensure free and fair elections in October 2020, and recognizing the importance of multi-party democracy in Tanzania."

Limepitishwa nchini Marekani kusihi serikali ya Tanzania na wadau wote wanaohusika kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 nchini Tanzania kufuata haki za binadamu, katiba ili kuhakikisha uchaguzi utakuwa wa huru na haki hapo mwezi Oktoba 2020. Tamko hilo limeonekana kukemea baadhi ya vitendo vya Serikali ya Tanzania tangu mwaka 2015 vyenye viashiria vya kuvunja haki za wananchi wa Tanzania.

Moja ya madai ya azimio hilo ni kwamba:
1. Serikali ya Tanzania imezuia ukusanyaji huru wa takwimu, utoaji wa takwimu
2. Serikali ama watendaji wa serikali wamekuwa wakitishia, kushambulia na kukamata wanahabari na kutokujali wanahabari waliopotea.
3. Serikali imezuia wanasiasa kufanya shughuli zao za kisiasa kuanzia mwaka 2016 mpaka 2019 kinyume na katiba ya nchi.
4. Serikali imedhibiti uhusiano wa taasisi zisizo za serikali NGO na taasisi nyingine zilizopo nje ya nchi kwa mujibu wa sheria iliyopitishwa mnamo September 2019.
5. Viongozi wa vyama vya upinzani wamekuwa wakipotea vitisho, kushambuliwa na serikali kushindwa kuwakamata watenda makosa.

View attachment 1573603

Soma zaidi:
Tanzania yaihakikishia Marekani uchaguzi utakuwa huru | DW | 09.09.2020
Ubalozi wa Marekani nchini wasikitishwa na Uminyaji demokrasia na ukamataji wa Viongozi wa Upinzani nchini
Ubalozi wa Marekani: Mbowe ameshambuliwa kikatili, wakumbushia pia shambulio la Tundu Lissu huku kukiwa hakuna hatua zilizochukuliwa
Takataka hii, wapambane na hali zao, hakuna kibaraka watakae msimika nchi hiii, narudia hayupo!
 
Kwani wametupa pesa ya kugharamia uchaguzi situmegharamia wenyewe kwa 100% wao waombe wasiombe sisi ni lazima magufuli awe rais kwisha habari yao walizoea wanatoa vipesa vya uchaguzi alafu na maelekezo mengi.
 
It's not. About the size of a dog in the fight.. But the size of the fight in the dog.

Ukija kiboya na mawazo kama haya utaishia kupewa mrahaba wa asilimia 3 na mali ni yako.. na kupangiwa matumizi juu..

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
Magufuli aliwaambia wakurugenzi.

"Nimekupa kazi.
Ninakupa mshahara.
Nakupa posho.
Nakupa Nyumba
Nakupa Gari.

Bado unaenda kumtangaza mpinzani"
Hivi kauli yake hii ya kishetani haitoshi kumpeleka the Hague kweli....?? 😒😒🤔🤔
 
Uchaguzi huu unawezi kutufanya tuwe kama Zimbabwe au tubakie kama Tanzania
Uzuri wa Tanzania mvua ni nyingi wao hutegemea kutumia njaa kama silaha na sisi hatuna njaa zimbabwe na sisi ni vitu tofauti kabisa kule kuna njaa,hawana bahari ,hawana maziwa,hawana vitu ambavyo ni muhimu,sisi tunategemewa na nchi 07 kupitisha bidhaa zao,sisi tuna mazao mengi na hatutegemei chakul kutoka nje.
 
Tanzania haiongozwi na Bunge la Marekani, mara 100 wangekua Waganda au Wakenya kwa kuwa la jirani ni lakwako
 
Wanaona matendo yenu yalivyo ndio maana mnakemewa upumbavu uwatoke, la sivyo wawachukulie hatua nyingine sababu nyinyi ni kama kenge! Hamsikii mpaka damu iwatoke kwenye masikio.
Upumbavu utoke kwenu uende Kwa Nani tena mkuu, kawaambie na hao waume zenu kwamba, Mbeligiji hatafikisha hata Kura milioni moja
 
Bunge la Amerika kukaa pamoja na kuweka azimio juu ya uchaguzi wa Tanzania ni habari ya kujivunia mkuu, inaonesha tuko ligi kubwa. Au wewe unachukulia vipi bunge la Amerika kuacha shughuli zake na kukaa kujadili na kuweka azimio juu ya uchaguzi wa Tanzania?..Eti unaonaje hiyo hali mkuu? levol ya nchi yako iko juu sana ama vipi?
Endelea kuwapa moyo vilaza wa lumumba! Yajayo yanafurahisha
 
Magufuli alishalisemea hili muda mrefu na akarudia na kusisitiza kuwa uchaguzi utakuwa huru na haki. Sasa marekani Wana Nini kipya?
Wanatamani wasimamie uchaguzi huu kumsaidia mchumba wao ashinde.
 
Only a colonised mind will cheer for such things. Kwao wakisema na mwangwi ukasikika kutoka kwa watu weusi wa taifa hili..ni ushindi mkubwa sana.

Wanaendelea kujua kuwa kati ya hao mamilioni walioko Tanzania kuna mifugo yao. Huwezi kushangilia jirani kujipangia ujisimamieje.

Wewe umeshindwa kujisimamia!? Unaona umekanyagwa unaumia ..kwann usisimame useme naumia.. sitaki.!? Mpaka uanze kumwambia jirani akusemee!??

Pathetic.

Kwani kusema wanataka uchaguzi uwe huru na haki kuna kosa gani. Ni sawa na CHADEMA wakisema wakishinda halafu wasitangazwe wataingia barabarani utasikia mtu anasema wanataka kuteta fujo hivi anayeleta fujo anayekataa kutangaza mgombea aliyeshinda au yule anayedai kwanini hata gazeti.

Hivi kwanini hii awamu serikali ni kama imejiyoa ufahamu na kutunga sheria nyingi sana za kuminya demokrasia ili iweje mbona watawala waliotangulia hawakufanya hayo ya kujaribu kujijengea himaya ya kutoguswa? Ngoja tuendelee kuvutugsna na hayo mataifa makubwa kumlinda dikteta hadi tuwe Zimbabwe nyingine.
 
US wanamsemo wao kwamba "the only language dictactors can understand is strength and power"
Kabisa...... Kimsingi tunawakaribisha watusaidie kumuondoa beberu na kupe ccm aliyenyonya nchi kwa miaka 60 sasa
 
Hawa mabeberu wamepewa na nani mamlaka ya kuwa viranja wa dunia nzima?

Mbona sisi tunakua kimya wao wanapowaziba pumzi watu weusi mpaka wanawaua kila kukicha?

Mbona tunakua kimya wanapowaua maelfu ya watu wasio na hatia kule Afghan na Iraq na hata Libya?

Anayeshabikia mambo haya bado ni nyani aliye kwenye zama za ujima
 
Hivi kauli yake hii ya kishetani haitoshi kumpeleka the Hague kweli....?? [emoji19][emoji19][emoji848][emoji848]
Na wao kwa nini hawakuwapeleka the likes of Henry Kissinger huko the Hague!?

Don't be fooled by the dramatized world order ...it's just an illusion painted to do one thing in reality doing the other. Ref. To Corona "The Pandemic Outbreak"

Hiki US inafanya sio kulinda haki zako wewe kabwela Nanjilinji huko . Is use you for the american conglomerates to make money.. Just that.

You can either be a fool and bend over.. or take it the high road and be a man about it. narudia hivi sio vigeni , alifanya Carl Peters na machief miaka ya 1800 na sasa collaborators are floating like bad beans repeating the same thing paving the road for colonialism.. once again.

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Kuna mgombea nimeona video kazidisha muda kakataa kushuka jukwaani na eti linajigamba lipo tayari kwa lolote

Kwani wewe hiyo kanuni ya kumshusha mgombea kwenye jukwaa umeona imeandikwa wapi kwa mujibu wa kanuni mgombea anapokiuka kanuni ni yule aliyeathirika na ukiukwaji huo kwenda kulalamika kwa msimamizi wa uchaguzi. Kulingana na kanuni jeshi la polisi haliwezi kuathirika kwakuwa wao siyo wagombea.
 
Back
Top Bottom