Azzan Zungu ataka mazungumzo Bandari ya Bagamoyo kunusuru tatizo la ajira

Kwa maoni yako "Mwenye aliye nacho aongezewe zaidi"?

Bagamoyo ni sehemu nzuri ya kuwepo kwa bandari ya nguvu; lakini kwa sababu tunataka maendeleo yaenee nchi nzima, ni bora tuweke jitihada za ziada kuwekeza na huko kwingine, ili nako mchango wao kwa taifa uonekane.

Ukiangalia tu hata ramani, pakiwepo bandari yenye uwezo mzuri Tanga, na miundombinu (iliyopo) kama reli na barabara ikaimarishwa, bandari hii itakuwa na umuhimu wa kipekee sana kwenye eneo lote la kaskazini hadi kuelekea kwenye ukanda wa Ziwa, hadi Uganda, DRC na kwingineko.
Hii itakuwa ni bandari muhimu inayofanya kazi kwa pamoja na hii ya Dar.

Tukiimarisha bandari hiyo, sehemu hizo zinazonyemelewa sana sana sasa hivi na bandari ya Mombasa, hawatakuwa na usumbufu tena wa kusubiri mizigo toka Dar.
Usafiri wa ndani ya Ziwa Victoria utawafanya waganda wengi kutegemea bandari hii. Kifupi ni kuwa itaweka ushindani mzuri sana kwa Mombasa.

Sasa hivi Mombasa wanategemea kushika sehemu zote hizo bila ushindani - Kilimanjaro, Arusha, Manyara, na hata sehemu za ukanda wa ziwa, maeneo haya hatimaye yatashikwa na Mombasa, na hakuna atakayezuia hilo lisitokee.
 
Bandari tunazungumzia sekta binafsi kuwekeza kwenye taasisi za uma mahali ambapo Serikali haina uwezo wa kuwekeza
Hapana kwani PPP inafanyeje kazi? Kuna hospitali za Rufaa zinamilikiwa na taasisi binafsi kwa ushirikiano na serikali. Hata kuna shule ya serikali ya viziwi ila inaendeshwa na benki fulani!! Yaani wao wanaweka majengo serikali inatafuta walimu n.k

Kwenye karne ya 21 biashara zinafunguka zaidi so ushiriki wa serikali unabaki kwenye udhibiti tu sio mpaka ishiriki moja kwa moja kwenye kuendeleza bandari/viwanda n.k

Ndio maana kuna kampuni za ulinzi ilihali kuna polisi, kuna private investigators ilihali kuna TISS n.k so sio vibaya serikali ika focus kwenye kuweka mazingira wezeshi kma miundombinu alafu ikaachia mambo mengine sekta binafsi yenyewe isubiri kodi tu na mapato ya wananchi wake wanaopata ajira.
 
Sasa hapo upigaji wake uko wapi?

Umasikini ni mbaya sana
NSSF wangewalipa Wananchi wenye maene yao vizuri, sema Manji akaja akawanyanganya Tonge la mdomoni kwa ujanjajanja, halafu yeye Manji akavuta Mkwanja mrefu sana kutoka NSSF!! Hapo huoni Kama Muhindi kawapiga Watanzania wenzako wasiokuwa na uelewa wa Mambo yanavyokwenda huko ndani!? Wewe unadhani Kama kweli Wananchi wangeambiwa mapema kuna mradi unakuja na watalipwa, unadhani wangekubali kumuuzia Manji maeneo yao!?

Tujifunze kuwapa Wanyonge haki zao hata Kama tunaona akili zao zimelala na wala hata hawajui kuwa wana haki zao!! Manji aliwapiga kwa kuwa hawana information za kutosha!! Au wewe unadhani bila huo Mradi Manji angethubuti kununua hayo maeneo kwa wakati huo!? Viongozi ndiyo walitakiwa wawape information raia wao, lakini information wamempelekea Manji kimyakimya!!
 
Hiyo hela haitatosha
Pale inatakiwa zaidi ya trillion 20
 
Uchumi wa Singapore na Malaysia wanategemea bandari mkuu,kwa hiyo bandari ni mojawapo ya vyanzo vya mapato kwa asilimia kubwa vyenye uhakika kwa mwaka
Sawa kwan hizi zilizopo hatuwez kuboresha ili kuongeza mapato??

Acheni kuuza nchi wajukuu wenu watakuja kuwalaani
 
Manji ni mfanya biashara. Angewatapeli hayo maeneo bila kuwalipa, ningekuunga mkono kuwa aliwapiga. Lakini waliuza kaa hiari yao wenyewe.

Tuache hizi mambo za kutaka kuonewa huruma kwenye ulimwengu wa ukweli
 
Duuuh kumbe Hawa watu ni wahuni hivi?? Daaah
 
Uchumi wa Singapore na Malaysia wanategemea bandari mkuu,kwa hiyo bandari ni mojawapo ya vyanzo vya mapato kwa asilimia kubwa vyenye uhakika kwa mwaka
Unaweza kulinganisha akili ya Malaysia na Singapore na akili ya Bongo ya hivi karibuni? Hatuwezi kuiga ujenzi wa bandari Singapore peke yake bila kuyawwza mwngine madogo tu, kwa mfano; kuchaguana na kupeana madaraka kwa misingi ya sifa zinazofaa! Tunashindwa!
 
Ni kweli mwenda zake baadhi ya mambo yake yalikuwa ya kuumiza watu, ila kwa swala bandari ya Bagamoyo mkataba ule ni ng'ombe pekee anayeweza kuukubali sababu hana utashi wa kujua jema au baya, sasa baadhi ya wabunge wanaibuka wakati huu bila kufiria hata jinsi ya kurekebisha mkataba wenyewe 10% inawabana kama kuku anayetafuta pa kutagia.
 
zungu hafai hata kuwa mwenyekiti wa mtaa ni waovyoo sana ilala haina barabara za maana magufuli alimchagua kuwa waziri wa mifuko ya nailoni rais alijuta kupa uwaziri
 
Mradi wa bandari ya bagamoyo ni muhimu kwa ukuaji wa uchumi wa nchi yetu na utaleta ongezeko kubwa la ajira na uzalishaji wa bidhaa kutokana na eneo mwambata la industrial area.Unafaida nyingi huu mradi kuliko hasara nashauri serikali isaini utejelezaji wa mradi kwa kuzingatia win-win situation #mh Rais na watendaji wako tafadhalini tumewapa dhamana msisite kufanya maamuzi magumu yenye tija.Mradi wa ges Lindi tafadhali harakisheni utekelezaji wake nchi inufaike na rasilimali hizi
 

..Je, watanzania tunajua kilichomo ktk mikataba ya ujenzi wa sgr au stieglers gorge?
 
Wabunge wetu ni mbumbu, how we vote for imbeciles, I just can’t understand. Funga bunge na Pima akili zao, 99% ni vichaa, they have serious mental issues!
Hapana siyo vichaa, wanajuwa watakacho, its all about 10% in dollars...
 
Bandari ya Bagamoyo haiwezi kujengwa pasipo kuzuia utendaji wa bandari zingine, ni sharti la lazima linasemwa kuwepo ndani ya mkataba. Huwezi kupata vyote.
 
Umuhimu wa bandari sio tatizo, tatizo ni mapato yatokanayo na bandari yanamnufaisha nani? Hata hiyo Dar Port, container terminal kwa undani anaefaidika ni TICTS siyo TPA sababu ya mikataba mibovu.

Iwe kupanua bandari za Mtwara, Dar na Tanga au Kujenga bandari upya kama Bagamoyo, Kilwa n.k, tusiwabebeshe wananchi mzigo mzito wa madeni wakati mfaidika au wafaidika ni watu wachache.

Mkataba wa ujenzi wa Bagamoyo uwekwe wazi ili umma ujue mazuri na mabaya yaliomo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…