Baada ya bandari kubinafisishwa kwa miaka 100, ninamuomba radhi chifu Mangungo

Athari yake ni nchi kutumia niuz nyingine kupata mapato, mfano ni kuintroduce Kodi sehemu nyingi. Leo ukipata mita mpya ya umeme utapaswa kulipa Deni la tokea 2021
 
Mbona Serikali inatuchanganya? Which is which? Who when why?

Mkataba wa Mwaka au Jiti? Faida ya Trilioni 14 zinaatikanaje kwa huo mwaka? Maana ufafanuzi unasema Waarabu wataongeza mapato kutoka 7T mpaka 21T kwa mwaka.
Common sense tu wala huitaji utafute mganga, uwekezaji mkubwa kama huo unawezaje kuwa wa mwaka mmoja? Serikali wanajua baada ya mwaka mtazoea tu na hakuna wa kuulizia tena, atayeuliza ataambiwa kuna vitu havijakamilika wanatakkwa kuendelea

Tabu ni baadae raisi atayekuja na kulalamika hili wote watapiga u-turn
 
Wameonaa tunapiga kelele miak 100 wameonaa wapunguzee miaka ila bado nina maswaliu mengi sana yani kwenye hay matrilion ya msaada hatuwezi kuleta kampuni ikajengaa miundo mbinu mizuri ya bandari na kuweka system za kuoperate mpaka tubinafsishe bandari? hatari sanaaa hili limedhihirishaa VIONGOZI WETU HAWAJITAMBUI KABISAA yani hili suala kulijadili bungeni ni matusi makubwa mnooooo...mnooo bora wajadili USHOGA KAMA HAWANA KAZI.
 
Bandari ilishajengwa na tbc juzijuzi wakasifiaa kasi ya upanuaji bandari, kila sifa ikamwagwa. Huyu mwarabu kajiokotea dodo, kakuta tayari uwekezaji mkubwa ushafanyika

Alafu walivyo wasahaulifu, wamesema bandari ya dar imefikia kikomo ndio maana wanataka bandari bagamoyo, hapohapo wanasema mwarabu atafanya uwekezaji mkubwa wa kupanua hii bandari
 
yani kwanza mkataba wa bagamoyoo Magu alisema wazi ni mkataba wa ovyoo na kiwendawazimu ila kwa kuwa hayupo wameamua waufufue upya.. Unajenga bandari kwa mkataba wa ovyoo kama uleee bado bandari kuu ya dar unampa MWARABU???? ila aisee ni vile tu hii nchi ina amani ila something must be done.... kuna ujinga mwingi sana unaendelea.
 
Hauhitaji kumuomba radhi Mangungo kwa mkataba ambao bado haujasainiwa.
 
Hauhitaji kumuomba radhi Mangungo kwa mkataba ambao bado haujasainiwa.
hapana mpaka bunge kuleta ule mswada hadharani sidhani kama haujasainiwaa ila wanafanya hivii ili kesho ukikutaa hata makuli ni waarabu pale bandari usishangae... yani kubinafsisha bandari ni UTAHIRAAAAAAAAAAA hakuna namna nyingine unaweza lisema hili.
 
Kwanza hakuna huo mkataba na barua ya kukanusha ipo. Pili nitajie menejimenti moja iliyopewa bandari na ikafanya kazi kwa ufanisi mkubwa. Masuala ya bandari inayokutanisha wadau wa mataifa mengi kwa wakati mmoja sio ya kuendeshwa na watu wasio na uzoefu wa kutosha kwa maana ya kuwa wataalam wa uchumi waliobobea.

Kila rais anakuja na team yake pale bandarini na inaishia kuwa ya wezi na wapigaji, kwanini tusijaribu kuja na menejimenti nyingine?. Cha muhimu ni kuwa na taratibu za kazi zenye kueleweka kila upande.

Tunapiga makelele humu JF tukipewa jukumu la kuendesha bandari unakuwa ni utumbo ule ule wa kila siku.
 
Kinara wa kusifu na kuabudu umeamua kubadili mtazamo ni vizuri nadhani umejifunza kitu.
 
Kumbe barua ipo, kama unayo tuwekee hapa.
 
Yani umeonaa tulivyolaaniwaa... wew unaamini Mwarabu au Mgeni anaweza kusimamia bandari kiusahihi kuliko mwafrika??? hapa shida unaweka watu kwa kujuana na kuamini aliesoma ndo ana uwezo mzuri wa kuongoza.. yule mkurugenzi aliiba akakutwa na mamilion kibao mwisho wa siku akarudishwaaaa... Hivi shida ni usimamizi au shida ni miundo mbinu???? tunajishusha sana na tunafanya kazi kwa kujuana na mazoeaa.
 
Mkuu mwafrika ni mwizi tu, kila report ya CAG ni madudu kwa kwenda mbele. Hatuna kipya chochote cha maana, ni mwendo wa urasimu ili mteja achukie atoe rushwa, bullshit kwa kifupi.

Waswahili hatuna uchungu na chetu, unajenga mazingira ya kuuchelewesha mzigo usitoke ili uibe ukisahau kuwa wanaousubiri mzigo huo ni watanzania kama wewe!, Taifa la kipumbavu sana hili.

Aje DP World, aje mwekezaji yoyote mwenye uwezo akabidhiwe bandarini, ilimradi mkataba uandikwe kwa umakini mkubwa ili maslahi yetu yalindwe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…