Baada ya bandari kubinafisishwa kwa miaka 100, ninamuomba radhi chifu Mangungo

Baada ya bandari kubinafisishwa kwa miaka 100, ninamuomba radhi chifu Mangungo

Madhara ya waarabu kuja kututawala.maana yeye anaasili ya huko uarabuni.ameamua kuwauzia waarabu wenzake ili siku akimaliza urithi wake arudi kwa waarabu wenzake na sisi kutuachia madhara ya huu mkataba wa kipumbavu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Na vp kuhusu wachina wanaotaka kupewa bagamoyo?!!! Na vp kuhusu waingereza waliopewa migodi mvalimvali enzi na enzi?!!!!

Acha udini na chuki haviwasaidii zaid8 ya kuwapa baraka tu mnaowachukia na kuwazushia hao huku nyie na udini wenu mkitakiwa kuolewa tu na hao mabwana zenu wa kizungu.

Unfeweza kujenga hoja yako bila kujngiza udini wako uliopandikizwa.
 
Kweli mama anaupiga mwingi kuifilisi nchi.

Huo mkataba hata ukivunjwa tutalipa pesa nyingi vizazi na vizazi.
 
Haya yatakuwa maajabu ya Karne, yaani majuzi tumegomea $12 billion za Bagamoyo kama awataki mkataba wa miaka 33 tena port wajenge wenyewe.

Halafu leo nchi isaink mkataba wa miaka 100 kwa uwekezaji wa $500m, tena kwa bandari ambazo zipo tayari.

Kama kuna ukweli ata huyo bwana godi atatususa, maana atubebeki ni gunia la misumari.
Hili ni Dili la bandari ya bagamoyo wamelileta kinyumenyume
 
Hili ni Dili la bandari ya bagamoyo wamelileta kinyumenyume
Kakoko alikuwa mtu sahihi, wa kuongoza bandari. Angeweza dadavua huo mkataba kinaga ubaga; tija ipo wapi.

Fair to current management ya TPA wamejaribu kuita waandishi wa habari kuelezea upande wao kwanini wanahitaji uwekezaji. Shida ni kwamba TBC, Azam na vyombo vingine ambavyo avijali cheap shorts awakuona umuhimu wa kuhudhuria.

Personal sijapenda vipande vya habari ambavyo Global TV na Millard Ayo vimeamua ku cover; based on what on what they thought it was important content.

Naelewa kwa upande wao, muhimu ni kuweka vitu wanavyodhani jamii inataka kusikia kwa uelewa wa uwezo wetu wa data usage na kukata mengine. But then if you are deeper you feel awakumtendea haki mkurugenzi na wasikilizaji kwa kutoa full interview.

That is why you need TBC involvement au taasisi husika kuwa wana channel zao kuhakikisha full interview is heard.

Not that ni wazalendo; mimi binafsi naamini Kakoko was the best.
 
Kakoko alikuwa mtu sahihi, wa kuongoza bandari. Angeweza dadavua huo mkataba kinaga ubaga; tija ipo wapi.

Fair to current management ya TPA wamejaribu kuita waandishi wa habari kuelezea upande wao kwanini wanahitaji uwekezaji. Shida ni kwamba TBC, Azam na vyombo vingine ambavyo avijali cheap shorts awakuona umuhimu wa kuhudhuria.

Personal sijapenda vipande vya habari ambavyo Global TV na Millard Ayo vimeamua ku cover; based on what on what they thought it was important content.

Naelewa kwa upande wao, muhimu ni kuweka vitu wanavyodhani jamii inataka kusikia kwa uelewa wa uwezo wetu wa data usage na kukata mengine. But then if you are deeper you feel awakumtendea haki mkurugenzi na wasikilizaji kwa kutoa full interview.

That is why you need TBC involvement au taasisi husika kuwa wana channel zao kuhakikisha full interview is heard.

Not that ni wazalendo; mimi binafsi naamini Kakoko was the best.
Umeongea kweli
 
Walichokitaka wamekifanikisha.

Dar ndio lango kuu la nchi nane.

Ukoloni ni Rasmi Sasa.

Samia anaingia kwenye historia ya Rais aliyeamua kuturejesha utumwani.
Maoni na Ushauri wa Wataalam wa Bunge ulikuwa ni huu - Je ulizingatiwa? Ndio ni kweli Bandari yetu ina shida kubwa hasa ya uzembe, kuendeshwa kwa hasara na upigaji - Je swala la kubinafsisha ni lini ilifanyika Mjadala wa Kitaifa watu watoe maoni- Uwekezaji ni mzuri ila ni hatari sana usipopelekwa kwa umakini na uzalendo. Kwanini miaka 100
Wataalam a wa bunge wanasemaje? Kutokana na uchambuzi tuliofanya hapo juu, ni maoni na ushauri wetu kuwa, Bunge lipate ufafanuzi kutoka Serikalini katika maeneo machache yafuatayo:-

19 a. Ibara ya 25 (1) inaeleza kuwa kuna shughuli za awali za mradi (Early Project Activities) zitaanza kufanyika mapema baada ya kusainiwa Mkataba. Shughuli za awali za mradi zitafanyika kabla ya Bunge kuridhia Mkataba na kabla ya Mkataba kuanza kutumika rasmi kwa mabadilishano ya Hati za Uridhiaji kati ya Serikali zote mbili.
Shughuli za awali za mradi zimetafsiriwa katika Ibara ya 1 kuwa ni kufanya upembuzi yakinifu pamoja na kufanya tathmini ya kimazingira na kijamii ya mradi huu (environmental and social due diligence), kujenga barabara za muda kuwezesha kufika eneo la mradi, n.k.
Tunashauri Serikali itoe ufafanuzi katika eneo hili, ambapo shughuli za Mradi zinaanza kabla ya Mkataba kuridhiwa na Bunge.

b. Ibara ya 20 kuhusu usuluhishi wa migogoro kufanyika Afrika Kusini na kwa kutumia Sheria za Usuluhishi za Kamisheni ya Umoja wa Mataifa juu ya Sheria zinazohusika na Biashara za Kimataifa (UNICITRAL Arbitration Rules), ni kinyume na maelekezo ya kifungu cha 11 cha Sheria ya Mamlaka ya Nchi kuhusiana na Umiliki wa Rasilimali na Maliasili ya Mwaka 2017 (The Natural Wealth and Resources [Permanent Sovereignty] Act, 2017).
Sheria tajwa inaelekeza kuwa mgogoro wowote unaotokana na matumizi ya rasilimali na maliasili za nchi hautatatuliwa katika mahakama na mabaraza ya nchi za nje, bali utatatuliwa na vyombo vya sheria vya Tanzania na kwa kutumia sheria za Tanzania.
c. Ibara ya 23 (4) kuhusu kusitisha Mkataba, inaeleza bayana kuwa Serikali husika katika Mkataba hazitakuwa na haki ya kuvunja Mkataba (denounce), kujitoa (withdraw from), kuahirisha (suspend) au kusitisha (terminate) Mkataba katika mazingira yoyote, ikiwa ni pamoja na mazingira ya uvunjaji mkubwa wa masharti ya Mkataba huu (material breach), mabadiliko ya msingi katika mazingira ya utekelezaji Mkataba (fundamental change of circumstances), mgogoro mkubwa wa kidiplomasia (severance of diplomatic or consular relations), au sabau zozote zile zinazotambulika katika sheria za kimataifa.
Masharti ya Ibara hii yanatakiwa kufafanuliwa na Serikali.

d. Muda wa utekelezaji Mkataba huu haujawekwa bayana, bali Ibara ya 23 1) inasema kuwa ukomo wa Mkataba huu ni mpaka hapo shughuli za mradi huu zitakapokuwa zimekamilika. Serikali iombwe kutoa ufafanuzi kuhusu jambo hili la ukomo wa Mkataba.

e. Ibara ya 27 inaweka masharti kwamba, pale ambapo Mkataba huu utaanza kutumika rasmi, Serikali yeyote katika Mkataba huu haitaingia au kuwa sehemu ya makubaliano ya ndani ya nchi au ya kimataifa wakati wa utekelezaji wa Mkataba.
Serikali iombwe kutoa ufafanuzi wa Ibara hii. Mkataba huu haujaweka muda wa ukomo, hivyo Serikali haitakuwa na nafasi ya kuingia makubaliano mengine kuhusu kuendeleza au kuboresha na kuendesha bandari zake.
f. Ibara ya 30 inaweka masharti ya kuwa na uthabiti, uimara na uhakika wa kutoyumbisha Mkataba huu (Stabilization). Eneo hili lipate ufafanuzi wa Serikali. Kwa kuzingatia kuwa Mkataba huu hauna muda wa ukomo. Hivyo, kuna mazingira sheria zitahitaji kufanyiwa mabadiliko kulingana na wakati, ambapo mabadiliko hayo yanaweza kuathiri masharti ya Mkataba huu na kuchukuliwa kuwa ni kuyumbisha Mkataba huu.

g. Kwa upande wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mamlaka ya kusaini mMkataba huu yametolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, hata hivyo, kwa upande wa Serikali ya Dubai haijawekwa wazi. Tunashauri Serikali itoe ufafanuzi kuhusu mamlaka ya kusaini Mkataba huu kwa upande wa Serikali ya Dubai
Imeandaliwa na Sekretariati ya Bunge

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Haya maandiko yananiacha na sonona. Mbaya zaidi we have no one to turn to. Hatuna bunge , serikali imejipachika ulanguzi. Hivi Mungu tumemkosea nini sisi watanzania
Uafrika hasa utanzania ni LAANA.

Wale Raia 66 walio ukana Uraia na raia wengine wengi waliokimbia hii nchi na hili bara wako sahihi kabisa na wamefanya jambo sahihi kabisa la kuvua Laana na kujitakasa kutoka kwenye Laana.
 
Onesheni palipoandikwa kuwa watamiliki kwa miaka 100
 

Attachments

  • Screenshot_20230606-234324.png
    Screenshot_20230606-234324.png
    138.6 KB · Views: 1
migodi tumeshindwa , mbuga za wanyama tumeshindwa, reli tumeshindwa, hub ya uchumi ambayo ni bandari nayo eti tunaelekea kushindwa, mwisho hata ikulu tutaambiwa tumeshindwa tu.

Wazanzibar tuliwapa ardhi ya bagamoyo wafuge ng'ombe , wakashindwa. yaani kila mahali tunashindwa,

Nyie akina kabudi na lukuvi si mpo ikulu , ndo ushauri huu mnaompa mama!? auze bandari kuu ya uchumi wetu kwa miaka 100,are we serious , mwigulu huu mkataba mabavu ukipita ,sidhani Kama utakuwa na amani moyoni maisha yako yote , kwa kuiuza Tanzania!!
 
Back
Top Bottom