Baada ya bomu la vijana wasiyo na ajira naona mgomo mwingine kutoka kwa kundi la vijana lililorudishwa nyumbani kutoka JKT

Kwamba Tanzania yenyewe imeshushwa toka sayari ya Mars ? Haah

Matukio tu mengi yametokea Tanzania hii hii teka mengine hayana hata miaka mingi iliyopita
 
Watapigwa hadi waonekane kama wamepata ajali
Unajidanganya Sana ndugu.

Duniani kote kabisa uzoefu unaonyesha kwamba Umma haujawahi kushindwa jambo lolote lile pale umma huo unapoamua kwa dhati kabisa ya mioyo yao kutekeleza jambo hilo.

Rejea yale machafuko yaliyotokea katika nchi za kiArab kati ya Mwaka 2011 hadi 2015 kule Tunisia, Libya, Misri, n.k.
Mlipuko wa Vuguvugu lile hatari ulianzia nchini Tunisia, sababu zikiwa ni UKOSEFU WA AJIRA KWA VIJANA.
Rejea pia kule nchini Bangladesh, Mwaka jana wa 2024 Waziri Mkuu wa nchi hiyo Hasinna lilimkuta jambo huko nchini Bangladesh hadi akalazimika kuokoa nafsi na kukimbilia nchini India, hadi leo hii tunapojadili suala hili bado yupo huko India. Sababu ya yote haya ni UKOSEFU WA AJIRA KWA VIJANA.

Aidha, hata mlipuko wa Generation Z kwa majirani zetu wa hapo Kenya, sababu ni UKOSEFU WA AJIRA KWA VIJANA

Hivyo Basi, suala hili la Ukosefu wa Ajira kwa Vijana MUST BE HANDLED WITH GREAT CARE!
The Regime of this country Must be very careful in dealing with this Problem of the Youth Unemployment.
Matumizi ya nguvu kubwa hayana nafasi kwenye suala la Utatuzi wa tatizo hili, badala yake AKILI KUBWA, HEKIMA na BUSARA ndiyo silaha sahihi zinazopaswa kutumika katika kutatua Mgogoro huu.
 
Reactions: Ame
Upo sahihi ila kwa watanzania utasubiri sana..
 
Hili sasa ndilo nililokua nalisubiri hatimae limefika sasa polisi huko walipo wanajiandaa kuwakamata sababu wanataka kuwajambisha wale waliokuwa wamekaa kwenye viti vya juu,
P

polisi.
Utawapiga wangapi? Would it make a different kumpiga wewe na jinsi anavyopigwa na maisha? Tusiombee mabaya nchi yetu, bali tukubali kuwajibika
Naona kabisa hii ni trend tu ya mtandaoni. Ngoja tuone.

Ukosefu wa ajira kwa Vijana ni tatizo kubwa ambalo lipo kiuhalisia.

Duniani kote kabisa uzoefu unaonyesha kwamba Umma haujawahi kushindwa jambo lolote lile pale umma huo unapoamua kwa dhati kabisa ya mioyo yao kutekeleza jambo hilo.

Rejea yale machafuko yaliyotokea katika nchi za kiArab kati ya Mwaka 2011 hadi 2015 kule Tunisia, Libya, Misri, n.k.
Mlipuko wa Vuguvugu lile hatari ulianzia nchini Tunisia, sababu zikiwa ni UKOSEFU WA AJIRA KWA VIJANA.
Rejea pia kule nchini Bangladesh, Mwaka jana wa 2024 Waziri Mkuu wa nchi hiyo Hasinna lilimkuta jambo huko nchini Bangladesh hadi akalazimika kuokoa nafsi na kukimbilia nchini India, hadi leo hii tunapojadili suala hili bado yupo huko India. Sababu ya yote haya ni UKOSEFU WA AJIRA KWA VIJANA.

Aidha, hata mlipuko wa Generation Z kwa majirani zetu wa hapo Kenya, sababu ni UKOSEFU WA AJIRA KWA VIJANA

Hivyo Basi, suala hili la Ukosefu wa Ajira kwa Vijana MUST BE HANDLED WITH GREAT CARE!
The Regime of this country Must be very careful in dealing with this Problem of the Youth Unemployment.
Matumizi ya nguvu kubwa hayana nafasi kwenye suala la Utatuzi wa tatizo hili, badala yake AKILI KUBWA, HEKIMA na BUSARA ndiyo silaha sahihi zinazopaswa kutumika katika kutatua Mgogoro huu.
 
Kama tukiipata kiongozi mzuri na mwenye maadili ya kifedha na uchungu wa nchi yetu Tanzania hakuna sababu yakuwa na Tatizo la ajira na pia tunaweza kuawaajiri na vijana wengi wa nchi jirani. Muhimu tu nikuhakikisha kuwa tunaweka kipambele kwenye kuzalisha ajira, Tunauwezo wakuzalisha ajira nyingi sana kwa Mda mfupi sana. Ajira ya kwanza ambayo inaitaji mtaji ni Bahari na maziwa uwezekano wakuwakopesha vijana vifaa vya uvuvi na kuendeleza na kupandikiza samaki wengi kwenye maziwa yetu tunaweza kuzalisha ajira direct milioni mbili na indirrect milioni mbili nyingine, Kilimo kama vile iliki, kahawa korosho, pamba na tumbaku hapa tunaweza kuzalisha direct ajira milioni 2 na indirect milioni moja, uwekezaji wa viwanda vya kuchakata mazao ya mashambani kama vile, Pamba, kahawa, korosho, tumbaku nakadharika pamoja na mnyororo mzima wa kuonheza thamani yaaani ni ajira za kumwaga kiasi vijana watanzania peke yake hawatazimudu hizo kazi, Kuimarisha kilimo cha umwagiliaji na usindikaji wa mazo mbali mbali, Badala ya nyanya kuozea mashambani kunatengenezwa viwanda vikubwa vya usindikaji mazao kama nyanya na matunda menginevkama zabibu. Tatizo hatuna viongozi ambao wapo tayari kuhakikisha watanzania tunapiga hatuwa tunawekeza fedha kibao kwenye bunge na magari ya washawasha ili kuwadhibiti vijana wasilete vurugu wakati vijana wakiwa busy hakuna hata mmoja utamwambia aandamane akakubali ila kwa sasa hali jinsi ilivyo ni kama nchi imemwagiwa petrol inasubiri tu kuwashwa moto.
 
Reactions: Ame
Upo sahihi ila kwa watanzania utasubiri sana..
Siyo kweli hata kidogo, kumbuka hao vijana baadhi yao Wana wazazi wao, ndugu zao, jamaa zao ambao wapo huko huko Serikalini. Athari wanazopitia hao vijana na hao ndugu zao nao pia wanazipitia, tatizo hili linawaumiza Watu wengine wote katika Jamii.
Kumbuka kwamba uvumilivu huwa una Mwisho wake.
 
Reactions: Ame
Shida yenu nyie msio na mafunzo ya kijasusi chama chenu kikikua mnaanza kuunga mkono juhudi kama chama cha walimu, malengo mazuri ila end of the day mnageuka chawa wa kisiasa.

For me naona hao jamaa wana mwanzo mzuri.
 
Tatizo mnaandika kirahisi kanakwamba kuna batan ya kubonyeza tu ajira ziwepo.
Huko Arabuni walikoharibu nchi zao kwa kisingizio cha ukosefu wa ajira wamepata hizo ajira au ndio hali imezidi kuwa ngumu?

Sisi wananchi tujitambue kwanza hasa kwenye mtandao kama huu wa jamiiforums tuwe tunaandika hoja za msingi mara kwa mara, kwa uwingi na kwa staha hii itapelekea viongozi wenye dhamana kuvutwa na nguvu chanya kitu kitakachopelekea wao na sisi tukae tuamue jambo moja lenye manufaa kwa wote.
Tatizo sisi wananchi hatujui tunachotaka au tunajua lakini hatuheshimu muda wa kukiumba.

Pia tuelewe maisha hayajakamilika!
 
Unaweza kufika mwisho wa uvumilivu ukajikuta unajidhuru mwenyewe au unadhuru njia njema maishani mwako
 
Jkt si wamefundishwa kilimo waandamane ya nini sasa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…