John Wickzer Mulholland
JF-Expert Member
- Apr 13, 2023
- 6,656
- 14,403
Tatizo mnaandika kirahisi kanakwamba kuna batan ya kubonyeza tu ajira ziwepo.
Huko Arabuni walikoharibu nchi zao kwa kisingizio cha ukosefu wa ajira wamepata hizo ajira au ndio hali imezidi kuwa ngumu?
Sisi wananchi tujitambue kwanza hasa kwenye mtandao kama huu wa jamiiforums tuwe tunaandika hoja za msingi mara kwa mara, kwa uwingi na kwa staha hii itapelekea viongozi wenye dhamana kuvutwa na nguvu chanya kitu kitakachopelekea wao na sisi tukae tuamue jambo moja lenye manufaa kwa wote.
Tatizo sisi wananchi hatujui tunachotaka au tunajua lakini hatuheshimu muda wa kukiumba.
Unaweza kufika mwisho wa uvumilivu ukajikuta unajidhuru mwenyewe au unadhuru njia njema maishani mwako
Tatizo la ukosefu wa AJIRA kwa Vijana ni kubwa sana, zinahitajika nguvu za pamoja Kati ya Serikali na Wananchi wote ili kukabiliana na tatizo hili.
Kwenye hiyo comment yangu hapo nwishoni nimejaribu kueleza Nini kifanyike ili kutatua tatizo hili