Baada ya Dr.Kigwangala, Mwigulu, sasa ni zamu ya Makonda kuhusu jina, hii inaweza kuwa kweli au?

Baada ya Dr.Kigwangala, Mwigulu, sasa ni zamu ya Makonda kuhusu jina, hii inaweza kuwa kweli au?

Makonda ni mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam na katika mkoa wake kuna watu wanaishi kwa imani tofauti hivyo wanayo haki ya kumwita na kumuombea. Mie naona heri avae shuka kuliko yule anae mwita binadamu mwenzie mungu wakati kishasema yeye sio mungu
 
Ziko jinai za aina mbili, public offences na private offences. Public offense ni makosa ya uvunjifu wa sheria za public laws kama mikosanyiko, maandamano, uharibifu wa malí ya umma or makosa yoyote against the public.

Personal/private crimes ni makosa ya jinai yanayofanywa na individual dhidi ya individual or individual ndidi ya entities be it public or private.

Kosa la theft, forgery, fraud, bodily injuries, sexual offences other than incest or sodomy, hata rape, beating, Polisi haiwezi kuinitiate uchunguzi hadi mtu au taasisi ipeleke malalamiko kufungua RB. Hakuna mtu yoyote au taasisi yoyote iliyopeleka malalamiko yoyote kuitisha uchunguzi. Waliochunguza ni wale "jamaa zetu" tuu. Hivyo hakuna lalamiko lolote dhidi ya Mkuu wetu wa mkoa Mhe. Sana Daudi Albert Bashite AKA Paul Makonda.

Hata kama unaishi jirani na Kamanda Siro na akashuhudia mke anapokea kisago, mke huyo asipolia kuomba msaada, Siro haji kuingilia.

Au mtu akiibiwa na mwizi akakatwa red-handed Siro hawezi kunfungulia mashitaka kama wewe hujakwenda kulalamika.

Paskali
acha kutulisha matango pori ewe uliyeamua kudharau taaluma yako na kugeuka mchumia tumbo
emphasis on Section 14(a) (extracted from the Criminal Procedure Code Cap 20 Revised edition 2002)
14. Arrest by police officer without warrant
A police officer may without a warrant arrest–
(a) any person who commits a breach of the peace in his presence;

sasa wewe unatudanganya hapa eti, "Hata kama unaishi jirani na Kamanda Siro na akashuhudia mke anapokea kisago, mke huyo asipolia kuomba msaada, Siro haji kuingilia."

kama umetenda kosa la jinai katika uwepo wake na akashuhudia ana wajibu chini ya kifungu 14(a) cha Sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai kukukamata kwa hilo kosa alilolishuhudia.

wajibu huu pia upo kwa watu binafsi kifungu 16(1) cha Sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai ya 2002
16. Arrest by private persons
(1) Any private person may arrest any person who in his presence commits any of the offences referred to in section 14.


na pia kwa mahakimu kifungu 18 cha Sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai ya 2002
18. Magistrate may arrest person for an offence committed in his presence
When any offence is committed in the presence of a magistrate within the local limits of his jurisdiction he may himself arrest or order any person to arrest the offender and may, subject to the provisions of this Act relating to the granting of bail, commit the offender to custody.


NAWASILISHA.
 
halafu huwa siwapendi watu kama nyie ndo mnafanya taifa linaangamia hv unafurahia makonda kutumia cheti cha mtu hawezi kufanya kaz kwa weledi sababu ni mbumbumbu halafu ww li mtu lizima hebu kuwa na akili shule ni muhimu ktk utendaji ukimsemea mwigulu huyo hajawahi kufeli alitumia jina la mtu kusoma cheti ni chake
lkn makonda ametumia cheti cha mtu kichwan empty
Tuwekee hicho cheti cha mtu wewe mwenye akili timamu .
 
Ukimgusa Mbowe ni kama umegusa kidonda kibichi kwa msumari wa moto ni wakali kuliko maelezo. Sabbu huyo ndio mtoa riziki wao muabudiwa wao he is OK all the tym.
Ukiuliza kuhusu Makonda as long as alimgusa mtoa riziki wao he is more like a monster kwao.!
Alinunua cheti alieuza cheti je ni nani ? Yuko wapi? Je muuzaji hana hatia? Alinunua kwa tsh ngapi? Kulikuwa na makubaliano gani baina yao ? Je kulikuwa na ushahidi wa kuuziana baina yao?
Je elimu aliyo nayo makonda ni ya chuo kikuu au ya darasa la saba? Je alie muuzia cheti ana elimu ipi kwa sasa? Na yuko wapi?
[HASHTAG]#Makonda[/HASHTAG] you are my Hero#
Maswali hayo yatajibiwa pale Bashite aka Makonda atakapojitokeza kukanusha!
 
Sasa Sirro ana ushahidi kuhusi vyeti vya Makonda?

Sirro tangu lini akaweza kuhakiki vyeti vya watu?
Kuna mambo yanahitaji mamlaka husika(Necta, Wizara ya elimu) kutoa miongozo kwa vyombo vya sheria kufanya kazi juu ya jambo flani.
Otherwise Sirro hawezi kwenda kichwa kichwa hapo na je ushahidi ukikosekana?
Nani kati yenu anaweza kutoa ushahidi kuhusu vyeti vya Makonda?

Hapa tunaongea maneno mengi tu hakuna Mwenye ushahidi na hilo
 
Nitashangaa sana kama hatashitakiwa na kama ataachwa kuhudumu kama mkuu wa mkoa, JPM itabidi na yeye achunguzwe PhD yake au aachie ngazi kwa hiari hatuwezi kukubali kuendelea kuongozwa na watu wasio na sifa yaani wasio wakweli, wajanja wajanja
Peleka lalamiko kwenye vyombo vya sheria na uwe tayari kutoa ushahidi mkuu, itakua vizuri ukitusaidia kusema yaliyochini ya kapeti
 
halafu huwa siwapendi watu kama nyie ndo mnafanya taifa linaangamia hv unafurahia makonda kutumia cheti cha mtu hawezi kufanya kaz kwa weledi sababu ni mbumbumbu halafu ww li mtu lizima hebu kuwa na akili shule ni muhimu ktk utendaji ukimsemea mwigulu huyo hajawahi kufeli alitumia jina la mtu kusoma cheti ni chake
lkn makonda ametumia cheti cha mtu kichwan empty
Cheti cha Mwigulu na jina si lake. Usiwe na selective AMNESIA.
 
Historia ya Ndg RC Mhe. Paul Makonda.

Nitangulize kuomba radhi kwa ndg Makonda kwa sababu hajanipa ridhaa yake ya kuelezea Historia yake.
Nimelazimika kutoa historia hii ili kuondoa upotoshaji unaoendelea ktk mitandao ya kijamii na mitaani.
Kwa hiyo kosa langu kubwa litakuwa ni hilo

Kwa ufupi Mhe. Makonda ni mhitimu wa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi ndiko alikokupatia Digrii ya uchumi na maendeleo ya jamii.
Hata hivyo safari yake ya kitaaluma ilikuwa ngumu kutokana na hali ya kipato.
Kabla hajaenda Chuo Moshi, alipita ktk shule ya msingi Kolomje na amesoma pia ktk Chuo cha uvuvi Mbegani Bagamoyo ambako alisoma hadi ngazi ya Diploma ktk masuala ya uvuvi.

Safari ya Makonda ya kisiasa ilianzia Chuoni Moshi akiwa waziri mkuu wa Serikali ya wanafunzi.
Amekuwa kiongozi pia ktk Jumuiya ya Vijana CCM kama makamu Mwenyeki taifa nk.
Hakuna asiyejua misukosuko na minyukano ya kisiasa ndani ya CCM vijana walivyokuwa wanagawika kutokana na wanasiasa mafisadi kuwagawa vijana wa UVCCM.
Makonda alikipigania chama kutokana na misimamo yake lakini alienda mbali zaidi na kuwataja wanasiasa waliokuwa wanawagawa vijana wa CCM kwa rushwa na hila,-jambo ambalo halikuwa rahisi kwa wakati huo.
Hatimaye Rais Kikwete akamteua kuwa Mkuu wa wilaya ya Kinondoni.

Makonda ni mwana CCM ambaye hajapitia mafunzo ya kiitikadi kama wengine lakini siasa za Makonda ni zile zinazoendana na wakati husika na zinawavutia watu wengi lakini pia zinawaumiza vichwa vya wana siasa wengine ndani na nje ya CCM, kiasi kwamba wanamuonea wivu na kutaka kumkwamisha kwa kila namna ili asifanikiwe kwa sababu wanaamini mafanikio yake yatampa umaarufu.
Hili ndilo linalokwamisha maendeleo ya kijamii kutokana na wanasiasa kukwamishana wala hawana huruma na watanzania.

Makonda ni mbunifu, kwani yeye ndiye mwanzilishi wa mashindano kama lile la "Kinondoni Talent Seach" lililopelekea hata baadhi ya wakuu na wabunge mbalimbali nao kuanzisha mashindano ya ligi za mpira wakiziita ligi hizo mara nini nini cup, clab, jock kwa majina yao nk.
Bahati mbaya hawakufanikiwa zaidi ya kutafuta sifa, si hawakujua mwenzao alilenga nini!.

Kwa nini Makonda, kwa nini vyeti na kwa nini utajiri wa Makonda?

Kabla ya Makonda kuibua vita ya biashara ya madawa ya kulevya mambo yaliyozuka hivi sasa ya utajiri, vyeti na mara viongozi wanasema hazingatii sheria. sababu ni...

Kwanza wanaosema Makonda hafuati sheria ni wapumbavu na si wazalendo wa taifa hili na ni wanafiki wakubwa.
Kwa sababu kama hoja ni sheria, sheria zilitungwa tangu lini na hapakuwa na wasimamizi wa sheria wala wauza madawa ya kulevya?.
Na je kwa nini hazikufanya kazi kwa kiwango ambacho amekifikia Makonda?.
Je tatizo ni sheria au tatizo ni watu?.

Pili ni wapi kunachuo cha u-DC na u-RC mpaka watu wahoji elimu ya Makonda?.
Kwani kuendesha vita ya madawa ya kulevya ni kuvunja katiba ya Nchi? au kuendesha vita hii hadi uwe na Digrii au Phd?
Si vita ya kila watanzania wote?.

Tatu suala la utajiri wa Makonda kuhoji kwa wakati huu wa sakata la madawa ya kulevya linawafanya wanaohoji kutudhihirishia kwamba wao ni watetezi wa wafanyabiashara hiyo kwa sababu, watanzania haituingii akilini kabisa;
Yaani kuona mtu ameanzisha mapambano ya madawa ya kulevya halafu mjinga mmoja au kikundi cha watu fulani kinaibuka na swali ambalo halihusiani na agenda ya vita husika.
Vita ya madawa ya kulevya inaingilianaje na utajiri wa mtu?,
Kama waliona kuna haja ya kuhoji kuhusu utajiri wa Makonda kwa nini wakae kimya muda wote huo hadi Makonda aanzishe vita ya madawa ya kulevya?.

Mwisho.
Siri ya mafanikio ya Makonda kisiasa itawachukua muda wanasiasa wengine kuijua kwa sababu wanasiasa wengi wanatamaa ya kupenda sifa na kufanya kila jambo waonekane ni lao au wamelianzisha wao huku lengo lao kuu wasifiwe, lakini pia kung'ang'ana sifa hizo zibaki kwao kwa vyovyote vile.
Kwa Makonda ni tofauti, Makonda yeye anatabia ya kuwatanguliza mbele viongozi wakubwa au walio juu ya mamlaka yake.
Siri nyingine ya Makonda ni jasiri na ana msimamo.
Asanteni.

Haya wanaobisha leteni ujinga mwingine.

Msisahau kutuletea cv ya elimu ya Mbowe, aliyewashikia akili zenu na kubaki mazuzu.

hoja binafsi.asanteni

Ni Makonda yupi unayemzungumzia? Kama ni Bashite rudi kwenye desktop yako uanze upya!
 
Mwigulu kanunua jina tu la mtu, makonda kanunua jina na elimu ya mtu.
Hatutaki RC mwenye elimu ya mtu mwingine lakini kichwani hamna kitu.

Amezungusha yani...yule bwanaaa.

Yule kiumbeee...amezungusha yani.

Yule bwana
 
Kitendo cha kamanda SIRO Kumuacha Makonda akitamalaki na vyeti Feki hapa Dasalaam inaonyesha kiongozi wa kanda Maalum anapwaya.

Makonda aliwahi kuhoji utendajikazi wa kamanda Siro kuwa haukizi viwango. nimeanza kuamini,kelele zetu zote hizi na inteligensia zake ameshindwa kufungua jarada la uchunguzi dhidi ya Daudi Bashite! only in Tanzania.

forgery is a criminal offence in the eyes of the law Kamanda Siro!
Mbona wewe ndio unapwaya hata ujui kazi za Kamanda Sirro.
 
Malaika wa bwana wamenishukia...wacha sasa nidownload material sasa

Wacha mimi niwashe moto sasa...yani yule kiumbe alitaga yani
 
Kitendo cha kamanda SIRO Kumuacha Makonda akitamalaki na vyeti Feki hapa Dasalaam inaonyesha kiongozi wa kanda Maalum anapwaya.

Makonda aliwahi kuhoji utendajikazi wa kamanda Siro kuwa haukizi viwango. nimeanza kuamini,kelele zetu zote hizi na inteligensia zake ameshindwa kufungua jarada la uchunguzi dhidi ya Daudi Bashite! only in Tanzania.

forgery is a criminal offence in the eyes of the law Kamanda Siro!
Kuna uwezekano yeye mwenyewe akawa Hanna vyeti staili vya kuweza kufahamu hayo,unajua tumefikia wakati hata kwenye wadhifa wa sirro Kuwe na cheti staili cha kuifikia nyadhifa hiyo,Ni gyro vinavyohusiana na sheria,ndio maana hata akakubali kuongozwa na Daudi basheti,Huu Ni utawala wa wagagagigikoko.
 
Back
Top Bottom