Baada ya Dr.Kigwangala, Mwigulu, sasa ni zamu ya Makonda kuhusu jina, hii inaweza kuwa kweli au?

Baada ya Dr.Kigwangala, Mwigulu, sasa ni zamu ya Makonda kuhusu jina, hii inaweza kuwa kweli au?

Kwanza wanaosema Makonda hafuati sheria ni wapumbavu na si wazalendo wa taifa hili na ni wanafiki wakubwa.
Kwa sababu kama hoja ni sheria, sheria zilitungwa tangu lini na hapakuwa na wasimamizi wa sheria wala wauza madawa ya kulevya?
Kwaio kama sheria zilitungwa zamani kisha zikawa hazifuatwi na yeye ndio asifuate? Si basi na yeye angewaachia wauza madawa kama hapo zamani?
Na je kwa nini hazikufanya kazi kwa kiwango ambacho amekifikia Makonda?.
Naomba uniambie kiwango gani kimefikia hadi sasa? Au ndio kapoteza kabisa hii vita? hivi unamwambia muuza unga nakuja kwako kusearch kesho kama una unga nikukamate nae muuza unga atakaa nao tu?
Pili ni wapi kunachuo cha u-DC na u-RC mpaka watu wahoji elimu ya Makonda?.
Kwani kuendesha vita ya madawa ya kulevya ni kuvunja katiba ya Nchi? au kuendesha vita hii hadi uwe na Digrii au Phd?
Ishu hapa sio kama vyeti vyake vinafit na kazi anayofanya, ishu ni kama vyeti feki awajibishwe kama walivyowajibishwa vengine, watu hawahoji elimu yake, wanahoji vyeti vyake.
Siri nyingine ya Makonda ni jasiri na ana msimamo.
Jasiri awamu ya tatu hawakuwataja majina, au kuna vigogo au amekuwa coward?
 
kinachozungumzwa ni wizi aka kugushi vyeti...ujambazi wa taaluma.hutaki majambazi yajadiliwe kwa ujambazi wao kisa wanatoa msaada ya kujenga misikiti na makanisa au kutoa mafungu manono kwa yatima?ujambazi utatukuzwa kwa njia hiyo ya kuficha maovu yao ?je hiyo ni halali ?tuubomoe huu ujambazi bila kujali mchango wa mhusika katika jamii.!
Leta ushahidi wako hapa wa ujambazi wa taaluma
 
Umeuuliza jambo jema.

Makonda kagusa ngome ya madawa ya kulevya, ndivyo inaonyesha nchi hii wengi wanategemea pesa kupitia madawa hayo. Inasikitisha, watajaribu sana ila wananchi wengine tunajua ni blah blah kumchafua tu.
Usihusishe madawa na vyeti fake ndugu vipi?
Jana kuna mdada muuguzi kala mvua 28 kwa kosa kama la Makonda.
There is no double standard on this.
 
Ishu sio kufeli wala kutokuwa na elimu ya kiwango tunachodhani kinatakiwa, ishu hapa ni matumizi ya vyeti/cheti visivyokuwa vya mhusika na kumfikisha katika nafasi ambayo asingeweza kwa kutumia vyeti vyake halisi.

Ni rahisi sana kutumia labels, nyumbu etc lakini jua ya kwamba hoja inafaa kujibiwa na hoja!
Weka ushahidi wa hivyo vyeti visivyokuwa vyake hapo tuone uthibitisho wa comment yako
 
Historia ya Ndg RC Mhe. Paul Makonda.

Nitangulize kuomba radhi kwa ndg Makonda kwa sababu hajanipa ridhaa yake ya kuelezea Historia yake.
Nimelazimika kutoa historia hii ili kuondoa upotoshaji unaoendelea ktk mitandao ya kijamii na mitaani.
Kwa hiyo kosa langu kubwa litakuwa ni hilo

Kwa ufupi Mhe. Makonda ni mhitimu wa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi ndiko alikokupatia Digrii ya uchumi na maendeleo ya jamii.
Hata hivyo safari yake ya kitaaluma ilikuwa ngumu kutokana na hali ya kipato.
Kabla hajaenda Chuo Moshi, alipita ktk shule ya msingi Kolomje na amesoma pia ktk Chuo cha uvuvi Mbegani Bagamoyo ambako alisoma hadi ngazi ya Diploma ktk masuala ya uvuvi.

Safari ya Makonda ya kisiasa ilianzia Chuoni Moshi akiwa waziri mkuu wa Serikali ya wanafunzi.
Amekuwa kiongozi pia ktk Jumuiya ya Vijana CCM kama makamu Mwenyeki taifa nk.
Hakuna asiyejua misukosuko na minyukano ya kisiasa ndani ya CCM vijana walivyokuwa wanagawika kutokana na wanasiasa mafisadi kuwagawa vijana wa UVCCM.
Makonda alikipigania chama kutokana na misimamo yake lakini alienda mbali zaidi na kuwataja wanasiasa waliokuwa wanawagawa vijana wa CCM kwa rushwa na hila,-jambo ambalo halikuwa rahisi kwa wakati huo.
Hatimaye Rais Kikwete akamteua kuwa Mkuu wa wilaya ya Kinondoni.

Makonda ni mwana CCM ambaye hajapitia mafunzo ya kiitikadi kama wengine lakini siasa za Makonda ni zile zinazoendana na wakati husika na zinawavutia watu wengi lakini pia zinawaumiza vichwa vya wana siasa wengine ndani na nje ya CCM, kiasi kwamba wanamuonea wivu na kutaka kumkwamisha kwa kila namna ili asifanikiwe kwa sababu wanaamini mafanikio yake yatampa umaarufu.
Hili ndilo linalokwamisha maendeleo ya kijamii kutokana na wanasiasa kukwamishana wala hawana huruma na watanzania.

Makonda ni mbunifu, kwani yeye ndiye mwanzilishi wa mashindano kama lile la "Kinondoni Talent Seach" lililopelekea hata baadhi ya wakuu na wabunge mbalimbali nao kuanzisha mashindano ya ligi za mpira wakiziita ligi hizo mara nini nini cup, clab, jock kwa majina yao nk.
Bahati mbaya hawakufanikiwa zaidi ya kutafuta sifa, si hawakujua mwenzao alilenga nini!.

Kwa nini Makonda, kwa nini vyeti na kwa nini utajiri wa Makonda?

Kabla ya Makonda kuibua vita ya biashara ya madawa ya kulevya mambo yaliyozuka hivi sasa ya utajiri, vyeti na mara viongozi wanasema hazingatii sheria. sababu ni...

Kwanza wanaosema Makonda hafuati sheria ni wapumbavu na si wazalendo wa taifa hili na ni wanafiki wakubwa.
Kwa sababu kama hoja ni sheria, sheria zilitungwa tangu lini na hapakuwa na wasimamizi wa sheria wala wauza madawa ya kulevya?.
Na je kwa nini hazikufanya kazi kwa kiwango ambacho amekifikia Makonda?.
Je tatizo ni sheria au tatizo ni watu?.

Pili ni wapi kunachuo cha u-DC na u-RC mpaka watu wahoji elimu ya Makonda?.
Kwani kuendesha vita ya madawa ya kulevya ni kuvunja katiba ya Nchi? au kuendesha vita hii hadi uwe na Digrii au Phd?
Si vita ya kila watanzania wote?.

Tatu suala la utajiri wa Makonda kuhoji kwa wakati huu wa sakata la madawa ya kulevya linawafanya wanaohoji kutudhihirishia kwamba wao ni watetezi wa wafanyabiashara hiyo kwa sababu, watanzania haituingii akilini kabisa;
Yaani kuona mtu ameanzisha mapambano ya madawa ya kulevya halafu mjinga mmoja au kikundi cha watu fulani kinaibuka na swali ambalo halihusiani na agenda ya vita husika.
Vita ya madawa ya kulevya inaingilianaje na utajiri wa mtu?,
Kama waliona kuna haja ya kuhoji kuhusu utajiri wa Makonda kwa nini wakae kimya muda wote huo hadi Makonda aanzishe vita ya madawa ya kulevya?.

Mwisho.
Siri ya mafanikio ya Makonda kisiasa itawachukua muda wanasiasa wengine kuijua kwa sababu wanasiasa wengi wanatamaa ya kupenda sifa na kufanya kila jambo waonekane ni lao au wamelianzisha wao huku lengo lao kuu wasifiwe, lakini pia kung'ang'ana sifa hizo zibaki kwao kwa vyovyote vile.
Kwa Makonda ni tofauti, Makonda yeye anatabia ya kuwatanguliza mbele viongozi wakubwa au walio juu ya mamlaka yake.
Siri nyingine ya Makonda ni jasiri na ana msimamo.
Asanteni.

Haya wanaobisha leteni ujinga mwingine.

Msisahau kutuletea cv ya elimu ya Mbowe, aliyewashikia akili zenu na kubaki mazuzu.

hoja binafsi.asanteni

Hahahaha, kamuulize jina lake nani??Mwizi wa vyeti ,hivi unajua ni kosa la jinai??Halafu Muulize mahusiano yake na Masogange na GSM.Ukiniuliza Inawezekana anamisimamo kwenye kuficha wafanyabiashara wa madawa maana alimpangishia nyumba Masogange,ni mtakatishaji pesa maarufu ndiyo sababu yuko bega kwa bega na watakatishaji pesa wa GSM.

Mwisho kama amekutuma mweleze Watanzania wa juzi siyo wa Jana,Leo wala kesho.
 
Eti leteni vyeti vya mbowe!!! Aisee wewe ni mzigo hadi kwa familia yako.Halafu sijui wanaume wengine wanapata wapi ujasiri wa kulamba wenzao hadi makalio ili tu wakumbukwe. Hizi tabia mikoa kama MARA huzi kuzikuta. Hakuna anayeweza kuhalalisha hii haramu ya makonda kwa kumuingiza mbowe. Hata kama mbowe ana dv sifuri ya four six but still hana kosa, kufeli siyo jinai brother ila kuchukua cheti cha mtu awe mzima au mfu kwa lengo la kuzitumia na kudanganya umma ni jinai kubwa.
 
Mkuu sisi watz ni watu wa Maneno siku zote kila siku mnataka vyeti vya Makonda vyenu mbona hamuweki tuvione..
Na hata akiwaonesha nyie itawasaidia nn kwann msifatilie vyeti vya watoto wenu bongo kweli badala mfanye kazi mnabaki kumfatilia mtu daaah Tanzania nchi yangu ila basi tu...

nyie ndio mizigo ya nchi hata wewe nazani una zero kwa jinsi unavyoonokana
 
Huu ni upoporombo,ni lini mwigulu alitumia cheti c chake?tunahitaji makonda alete vyeti vyake aache porojo,uongozi ni pamoja na skonga upstair
Makonda hana shida ila wewe unayelalamika na ushahidi unao weka hapa turidhike na comment yako tuache maneno matupu
 
Mwigulu alifanya papers zote kuanzia standard seven wakati bwana Daudi Bashite yeye alikuwa mzee wa mbonji tu na akaibuka na vyeti kwenye level za diploma. Hizi ni case mbili tofauti kabisa.
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] akipita hapa makonda analia
 
Mwigulu hakufeli bali aliacha shule kwenda kuchunga mbuzi, kisha akarudi shule kwa jina hilo, alisoma yeye mwenyewe, akafaulu, akasoma shule ya vipaji Ilboru, akatoka na Div one kali, akaenda chuo kikuu akatoka na 1st Class akaajiriwa BOT.

Daudi Albert Bashite alisoma kijijini akafeli, akaenda kurudia mjini, akafeli, akapiga dili kuchukua nafasi ya mtu aliyepasi hivyo akasoma shule ya serikali kwa jina jingine, akapata Div 0. Ndipo mrembo Christina akampa cheti cha kaka yake Paul Christian alichowasilisha kusomea chuo.

Makonda amefoji jina na kufoji cheti, Mwigulu amesomea jina la mtu mwingine.
Uthibitisho: Mwigulu Nchemba ni majina bandia ila vyeti ni vya kweli
Paskali
Pasco tunaomba uthibitisho wa hiyo story tafadhali.
 
Mbowe ana tuhumu kuhusu elimu yake, Mwigulu na Kigwangala pia wana tuhuma, hao wote hawaguswi ila anayepigiwa kelele ni Makonda tu. Tena ukiuliza kuhusu Mbowe ndio utaambiwa elimu si uongozi.
Watanzania wengi ni manyumbu na wanafiki kupita maelezo.
Mbowe ni mkuu wa Chama cha siasa bado hajaongoza serikali,ikifika wakati wake na yeye atahukumiwa stahiki,usichanganye mambo,serikali ni wananchi wote,na chama cha siasa ni cha kundi fulani tu la wananchi,kwa hiyo katiba ya chama chake imemruhusu ashike nyadhifa hiyo,umenifahamu hapo???.
 
Historia ya Ndg RC Mhe. Paul Makonda.

Nitangulize kuomba radhi kwa ndg Makonda kwa sababu hajanipa ridhaa yake ya kuelezea Historia yake.
Nimelazimika kutoa historia hii ili kuondoa upotoshaji unaoendelea ktk mitandao ya kijamii na mitaani.
Kwa hiyo kosa langu kubwa litakuwa ni hilo

Kwa ufupi Mhe. Makonda ni mhitimu wa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi ndiko alikokupatia Digrii ya uchumi na maendeleo ya jamii.
Hata hivyo safari yake ya kitaaluma ilikuwa ngumu kutokana na hali ya kipato.
Kabla hajaenda Chuo Moshi, alipita ktk shule ya msingi Kolomje na amesoma pia ktk Chuo cha uvuvi Mbegani Bagamoyo ambako alisoma hadi ngazi ya Diploma ktk masuala ya uvuvi.

Safari ya Makonda ya kisiasa ilianzia Chuoni Moshi akiwa waziri mkuu wa Serikali ya wanafunzi.
Amekuwa kiongozi pia ktk Jumuiya ya Vijana CCM kama makamu Mwenyeki taifa nk.
Hakuna asiyejua misukosuko na minyukano ya kisiasa ndani ya CCM vijana walivyokuwa wanagawika kutokana na wanasiasa mafisadi kuwagawa vijana wa UVCCM.
Makonda alikipigania chama kutokana na misimamo yake lakini alienda mbali zaidi na kuwataja wanasiasa waliokuwa wanawagawa vijana wa CCM kwa rushwa na hila,-jambo ambalo halikuwa rahisi kwa wakati huo.
Hatimaye Rais Kikwete akamteua kuwa Mkuu wa wilaya ya Kinondoni.

Makonda ni mwana CCM ambaye hajapitia mafunzo ya kiitikadi kama wengine lakini siasa za Makonda ni zile zinazoendana na wakati husika na zinawavutia watu wengi lakini pia zinawaumiza vichwa vya wana siasa wengine ndani na nje ya CCM, kiasi kwamba wanamuonea wivu na kutaka kumkwamisha kwa kila namna ili asifanikiwe kwa sababu wanaamini mafanikio yake yatampa umaarufu.
Hili ndilo linalokwamisha maendeleo ya kijamii kutokana na wanasiasa kukwamishana wala hawana huruma na watanzania.

Makonda ni mbunifu, kwani yeye ndiye mwanzilishi wa mashindano kama lile la "Kinondoni Talent Seach" lililopelekea hata baadhi ya wakuu na wabunge mbalimbali nao kuanzisha mashindano ya ligi za mpira wakiziita ligi hizo mara nini nini cup, clab, jock kwa majina yao nk.
Bahati mbaya hawakufanikiwa zaidi ya kutafuta sifa, si hawakujua mwenzao alilenga nini!.

Kwa nini Makonda, kwa nini vyeti na kwa nini utajiri wa Makonda?

Kabla ya Makonda kuibua vita ya biashara ya madawa ya kulevya mambo yaliyozuka hivi sasa ya utajiri, vyeti na mara viongozi wanasema hazingatii sheria. sababu ni...

Kwanza wanaosema Makonda hafuati sheria ni wapumbavu na si wazalendo wa taifa hili na ni wanafiki wakubwa.
Kwa sababu kama hoja ni sheria, sheria zilitungwa tangu lini na hapakuwa na wasimamizi wa sheria wala wauza madawa ya kulevya?.
Na je kwa nini hazikufanya kazi kwa kiwango ambacho amekifikia Makonda?.
Je tatizo ni sheria au tatizo ni watu?.

Pili ni wapi kunachuo cha u-DC na u-RC mpaka watu wahoji elimu ya Makonda?.
Kwani kuendesha vita ya madawa ya kulevya ni kuvunja katiba ya Nchi? au kuendesha vita hii hadi uwe na Digrii au Phd?
Si vita ya kila watanzania wote?.

Tatu suala la utajiri wa Makonda kuhoji kwa wakati huu wa sakata la madawa ya kulevya linawafanya wanaohoji kutudhihirishia kwamba wao ni watetezi wa wafanyabiashara hiyo kwa sababu, watanzania haituingii akilini kabisa;
Yaani kuona mtu ameanzisha mapambano ya madawa ya kulevya halafu mjinga mmoja au kikundi cha watu fulani kinaibuka na swali ambalo halihusiani na agenda ya vita husika.
Vita ya madawa ya kulevya inaingilianaje na utajiri wa mtu?,
Kama waliona kuna haja ya kuhoji kuhusu utajiri wa Makonda kwa nini wakae kimya muda wote huo hadi Makonda aanzishe vita ya madawa ya kulevya?.

Mwisho.
Siri ya mafanikio ya Makonda kisiasa itawachukua muda wanasiasa wengine kuijua kwa sababu wanasiasa wengi wanatamaa ya kupenda sifa na kufanya kila jambo waonekane ni lao au wamelianzisha wao huku lengo lao kuu wasifiwe, lakini pia kung'ang'ana sifa hizo zibaki kwao kwa vyovyote vile.
Kwa Makonda ni tofauti, Makonda yeye anatabia ya kuwatanguliza mbele viongozi wakubwa au walio juu ya mamlaka yake.
Siri nyingine ya Makonda ni jasiri na ana msimamo.
Asanteni.

Haya wanaobisha leteni ujinga mwingine.

Msisahau kutuletea cv ya elimu ya Mbowe, aliyewashikia akili zenu na kubaki mazuzu.

hoja binafsi.asanteni

Inaelekea umetumwa na humfahamu huyo ndugu ila unajipendekeza tu kwa kumfariji ili ajione yupo na watetezi. Katika vita ya dawa za kulevya unataja watumiwa hadharani, ndiyo umewapa nafasi kukimbia au kuweka mazingira ya kupoteza ushahidi.
 
Mwigulu kanunua jina tu la mtu, makonda kanunua jina na elimu ya mtu.
Hatutaki RC mwenye elimu ya mtu mwingine lakini kichwani hamna kitu.
Please ndugu tunaomba ushahidi wa manunuzi ya elimu na jina la mtu.
 
mbowe hana vyeti vya fake au hakununua vyeti kwaiyo bwana mdogo usichanganye madesa , Daudu Alberty Bashite kijana wa Ilomije ana vyeti fake vya bwana Paulo chritian Muyange na baada ya kwenda maakamani Muyange ikawa Makonda , kama Mbowe alinunuq vyeti leta details
Zero form 4 ya Mbowe unaingia vipi A level ?
 
Mwigulu alishaeza hapa kwamba yeye alirudia shule ndo akapewa jina la mtu aliyeacha shule akafanyia mtihani na akafaulu. Tofauti na huyu Bashite anayedaiwa kufeli kisha kanunua cheti cha mtu aliyefaulu mtihani huo ulomshinda kaifanya yake. Kagushi cheti. Kugushi cheti cha mtu ni kosa la jinai. Kuhusu Kigwangala sina maelezo ya kina.
Unao huo ushahidi wa kugushi cheti cha MTU mwingine? Hebu tuwekee hapa!
 
Acha uongo Paschal,Mwigulu hakupata Division One kali Ilboru alipata Division One ya kawaida ya kawaida ndo maana 1998 aka-join Mazengo High School.Wenye Division One kali walikuwa wanaenda Mzumbe,Ilboru,Tabora Boys na Kibaha. Hata pale Mazengo alitoka na Division Two ya point 10 akiwa na E ya Uchumi (alisoma EGM -ECONOMICS alipata E,Geography alipata C na Mathematics alipata B) ,ambao ni ushindi wa kawaida kabisa miongoni mwa ma-"bookworms"!
Hata pale Mlimani First Degree hakupata First Class bali alipata Upper Second! Tatizo ni VI.LA.ZA walioshindwa kuelewa pale alipofikia nafasi ya Mchumi daraja la kwanza (Senior Economist) pale BOT wakajua Mchumi daraja la Kwanza ni First Class,hiyo ndo tatizo la elimu ya Tanzania ya kukariri mambo! Hivyo Paschal Mayala fanya research yako kama"Fumadilu Kalimanzila unabisha haya!
Mkuu "Fumadilu Kalimanzila, kwanza asante kunipatia matokeo ya Mwigulu na wala hata sikujua kumbe alisoma O-Level, hivyo sikubishiI kabisa.

Mimi pia nilisoma Ilboru A-Level, na nilipotembelea shule yangu ya zamani kiukweli niliikuta kwenye hali ya kutisha na kusikitisha. Hapo ndipo nikatajiwa jina la Mwigulu na Nyalandu among the success story za waliosoma hapo Ilboru, bila kuelezwa walikuwa ni O-Level, kwa vile Iliboru ni shule ya vichwa na Mwigulu ni Mchumi Grade 1 wa BOT, mimi niliasume Mwigulu aliunganisha hadi A-Level, hivyo nakiri I was wrong.

Hata hivyo nilipandisha humu bandiko hili na nilimtaja Mwigulu.

Mwito kwa Wana Ilboru wa JF: Tuisaidieni Shule Yetu. Hali Yake Inatisha na Kusikitisha


Hali ya Shule ya Sekondary ya Ilboru - YouTube

Hali ya Shule ya Sekondari ya Ilboru Part II 25 min Pro .

Hali ya Shule ya Sekondari ya Ilboru Part III 28 min Pro ..
Paskali
 
Mbowe ni mkuu wa Chama cha siasa bado hajaongoza serikali,ikifika wakati wake na yeye atahukumiwa stahiki,usichanganye mambo,serikali ni wananchi wote,na chama cha siasa ni cha kundi fulani tu la wananchi,kwa hiyo katiba ya chama chake imemruhusu ashike nyadhifa hiyo,umenifahamu hapo???.
Makonda ni RC, ni wadhifa ambao hauhitaji vyeti wala akupeleka CV kwa Magu, kwa hiyo usimtetea kwa kutumia justification za kitoto, Mbowe alikula zero form 4 aliingia vipi A level ?
 
Wana Jamvi nimekuwa nikiangalia na kuona MAWE anayotupiwa RC Makonda kuhusu madai yanayohusu uhalali wa MAJINA na ELIMU yake.

Ninapoandika hivi sisemi Makonda hana mapungufu katika maamuzi na utendaji wake hasa wa juzi juzi, hata hivyo tukiangalia upande mwingine wa SARAFU yaonekana kuna ZAIDI ya CHETI, bali ni kutaka huyu RC afukuzwe kazi, ili WENGINE WAFURAHI.

Kwanza kabisa PROFILE ya Makonda ILIVUJWA maksudi kwa sababu ya watu walio na SABABU zao mbaya ili aonekane mbele ya Mwajiri wake ambaye ni rais kwamba yeye ni MHALIFU mkuu.

Na hivyo KUJARIBU kum influence mwajiri wake indirectly kutumia BLACKMAIL ili AMFUKUZE kazi.

Jambo hili limeendelea kwa muda sasa. Swali langu wanajamvi. Kabla ya kumtupia mawe turudi NYUMA.Waziri Mwigulu Nchemba alikuwa na issue kama hii, mbona ya Makonda kila mtu ANAMTUPIA MAWE?

Ni vizuri tusiwe na DOUBLE STANDARD katika kutoa haki bali tuwe FAIR/na USAWA. bila WIVU, UBAGUZI , na FITINA. Kama Waziri Mwigulu Nchemba HAKUJIUZURU basi TUMWACHE Makonda afanye kazi. Yeye si mkamilifu mara nyingi AMEJIKWAA je hilo ndo tumpe mob justice wampige mawe. ASIYE na DHAMBI na awe wa Kwanza kutupa JIWE!
KAJIPANGE UPYA DADA
 
Back
Top Bottom