Baada ya Dr.Kigwangala, Mwigulu, sasa ni zamu ya Makonda kuhusu jina, hii inaweza kuwa kweli au?

Baada ya Dr.Kigwangala, Mwigulu, sasa ni zamu ya Makonda kuhusu jina, hii inaweza kuwa kweli au?

Suala hili la RC wa Dar es Salaam, Paul Makonda linaelekea kubaya. Linaelekea kukisawajisha chama na hata Serikali yake. Hayati Mwalimu Nyerere,kwa tuliokuwa karibu naye kimatendo na kimaneno, alikuwa akisema kuwa tuhuma tu dhidi ya mtumishi wa umma zinatosha kuchukuliwa kwa hatua dhidi ya mtumishi huyo. Umefika muda wa kulinda hadhi ya Serikali na chama chetu tawala (CCM).

Kufuatia kutuhumiwa kutumia cheti cha mtu mwingine cha kidato cha nne katika kufika alipofika, Paul Makonda anapaswa kujitokeza na kujisafisha kwa kuonesha cheti chake hicho kilicho na jina lake la Paul Makonda. Suala lake laweza kuleta ukabila na hata udini.

Kiongozi ni kioo. Kioo kinapaswa kuwa safi ili kioneshe taswira ya anayekitazama. Kiongozi anapaswa kutenda na kusema kwa umakini na kwa usahihi wa kiasi kikubwa. Kiongozi anapaswa kuwa na sifa za uongozi wake badala ya kuwa na sifa zenye shaka. Shaka huzaa tuhuma. Tuhuma hutaka suluhisho na hatua za kuchukuliwa.

Sasa, natoa siku 30 kuanzia kesho kwa Paul Makonda kujitokeza na kutolea ufafanuzi wa tuhuma za kutumia cheti cha sekondari cha mtu mwingine. Kesho nakwenda Arusha. Nitakapotoka huko,nitakwenda Mwanza. Nitafika Misungwi na kufanya 'ushushushu' wa kutosha kumhusu Makonda. Nitachimba kila jambo linalomhusu.

Cheti kisipoanikwa hadharani na mhusika ndani ya siku 30 kuanzia kesho,nitayaanika yote ambayo nitayapata kule Kolomije, Misungwi mkoani Mwanza na kwingineko. Nisije kulaumiwa nikianika hadi yale ambayo hayapo katika mjadala kwasasa. Kama unatakiwa ushahidi, endapo kutabaki kuwa kimya hata kwa anayetuhumiwa,ushahidi utawekwa hapa. Atakayeutaka,ataupata hapa.

Mwafaaaaa!

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam
 
Ziko jinai za aina mbili, public offences na private offences. Public offense ni makosa ya uvunjifu wa sheria za public laws kama mikosanyiko, maandamano, uharibifu wa malí ya umma or makosa yoyote against the public.

Personal/private crimes ni makosa ya jinai yanayofanywa na individual dhidi ya individual or individual ndidi ya entities be it public or private.

Kosa la theft, forgery, fraud, bodily injuries, sexual offences other than incest or sodomy, hata rape, beating, Polisi haiwezi kuinitiate uchunguzi hadi mtu au taasisi ipeleke malalamiko kufungua RB. Hakuna mtu yoyote au taasisi yoyote iliyopeleka malalamiko yoyote kuitisha uchunguzi. Waliochunguza ni wale "jamaa zetu" tuu. Hivyo hakuna lalamiko lolote dhidi ya Mkuu wetu wa mkoa Mhe. Sana Daudi Albert Bashite AKA Paul Makonda.

Hata kama unaishi jirani na Kamanda Siro na akashuhudia mke anapokea kisago, mke huyo asipolia kuomba msaada, Siro haji kuingilia.

Au mtu akiibiwa na mwizi akakatwa red-handed Siro hawezi kunfungulia mashitaka kama wewe hujakwenda kulalamika.

Paskali

Sure
Hat ukijipersonate kama the real person hajalalamika haina shida
Tatizo ni kujivunjua heshima na uadilifu wako
Kama ni muhuni tu wa mtaani poa ila kwa kiongozi haipendezi
 
Kwa sababu wauza madawa ya kulevya HASWA na watumiaji pamoja na wenye wivu nae na wapinzani hawataki apambane kusaidia wananchi.
unaposema wewe ni msafi na ukaamua kuwa wasafisha na kuwafichua walio wachafu ni lazima usafi wako usiwe na mashaka mashaka,pia hata kama dhamila yako nikusafisha yaliyo machafu ili hali wewe huko nyuma ulikwisha potoka nilazima utathimini njia sahihi za kupambana nalo...!!Always good approach has no boundaries unapo amua kukomoa jiandae kukomolewa
 
Historia ya Ndg RC Mhe. Paul Makonda.

Nitangulize kuomba radhi kwa ndg Makonda kwa sababu hajanipa ridhaa yake ya kuelezea Historia yake.
Nimelazimika kutoa historia hii ili kuondoa upotoshaji unaoendelea ktk mitandao ya kijamii na mitaani.
Kwa hiyo kosa langu kubwa litakuwa ni hilo

Kwa ufupi Mhe. Makonda ni mhitimu wa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi ndiko alikokupatia Digrii ya uchumi na maendeleo ya jamii.
Hata hivyo safari yake ya kitaaluma ilikuwa ngumu kutokana na hali ya kipato.
Kabla hajaenda Chuo Moshi, alipita ktk shule ya msingi Kolomje na amesoma pia ktk Chuo cha uvuvi Mbegani Bagamoyo ambako alisoma hadi ngazi ya Diploma ktk masuala ya uvuvi.

Safari ya Makonda ya kisiasa ilianzia Chuoni Moshi akiwa waziri mkuu wa Serikali ya wanafunzi.
Amekuwa kiongozi pia ktk Jumuiya ya Vijana CCM kama makamu Mwenyeki taifa nk.
Hakuna asiyejua misukosuko na minyukano ya kisiasa ndani ya CCM vijana walivyokuwa wanagawika kutokana na wanasiasa mafisadi kuwagawa vijana wa UVCCM.
Makonda alikipigania chama kutokana na misimamo yake lakini alienda mbali zaidi na kuwataja wanasiasa waliokuwa wanawagawa vijana wa CCM kwa rushwa na hila,-jambo ambalo halikuwa rahisi kwa wakati huo.
Hatimaye Rais Kikwete akamteua kuwa Mkuu wa wilaya ya Kinondoni.

Makonda ni mwana CCM ambaye hajapitia mafunzo ya kiitikadi kama wengine lakini siasa za Makonda ni zile zinazoendana na wakati husika na zinawavutia watu wengi lakini pia zinawaumiza vichwa vya wana siasa wengine ndani na nje ya CCM, kiasi kwamba wanamuonea wivu na kutaka kumkwamisha kwa kila namna ili asifanikiwe kwa sababu wanaamini mafanikio yake yatampa umaarufu.
Hili ndilo linalokwamisha maendeleo ya kijamii kutokana na wanasiasa kukwamishana wala hawana huruma na watanzania.

Makonda ni mbunifu, kwani yeye ndiye mwanzilishi wa mashindano kama lile la "Kinondoni Talent Seach" lililopelekea hata baadhi ya wakuu na wabunge mbalimbali nao kuanzisha mashindano ya ligi za mpira wakiziita ligi hizo mara nini nini cup, clab, jock kwa majina yao nk.
Bahati mbaya hawakufanikiwa zaidi ya kutafuta sifa, si hawakujua mwenzao alilenga nini!.

Kwa nini Makonda, kwa nini vyeti na kwa nini utajiri wa Makonda?

Kabla ya Makonda kuibua vita ya biashara ya madawa ya kulevya mambo yaliyozuka hivi sasa ya utajiri, vyeti na mara viongozi wanasema hazingatii sheria. sababu ni...

Kwanza wanaosema Makonda hafuati sheria ni wapumbavu na si wazalendo wa taifa hili na ni wanafiki wakubwa.
Kwa sababu kama hoja ni sheria, sheria zilitungwa tangu lini na hapakuwa na wasimamizi wa sheria wala wauza madawa ya kulevya?.
Na je kwa nini hazikufanya kazi kwa kiwango ambacho amekifikia Makonda?.
Je tatizo ni sheria au tatizo ni watu?.

Pili ni wapi kunachuo cha u-DC na u-RC mpaka watu wahoji elimu ya Makonda?.
Kwani kuendesha vita ya madawa ya kulevya ni kuvunja katiba ya Nchi? au kuendesha vita hii hadi uwe na Digrii au Phd?
Si vita ya kila watanzania wote?.

Tatu suala la utajiri wa Makonda kuhoji kwa wakati huu wa sakata la madawa ya kulevya linawafanya wanaohoji kutudhihirishia kwamba wao ni watetezi wa wafanyabiashara hiyo kwa sababu, watanzania haituingii akilini kabisa;
Yaani kuona mtu ameanzisha mapambano ya madawa ya kulevya halafu mjinga mmoja au kikundi cha watu fulani kinaibuka na swali ambalo halihusiani na agenda ya vita husika.
Vita ya madawa ya kulevya inaingilianaje na utajiri wa mtu?,
Kama waliona kuna haja ya kuhoji kuhusu utajiri wa Makonda kwa nini wakae kimya muda wote huo hadi Makonda aanzishe vita ya madawa ya kulevya?.

Mwisho.
Siri ya mafanikio ya Makonda kisiasa itawachukua muda wanasiasa wengine kuijua kwa sababu wanasiasa wengi wanatamaa ya kupenda sifa na kufanya kila jambo waonekane ni lao au wamelianzisha wao huku lengo lao kuu wasifiwe, lakini pia kung'ang'ana sifa hizo zibaki kwao kwa vyovyote vile.
Kwa Makonda ni tofauti, Makonda yeye anatabia ya kuwatanguliza mbele viongozi wakubwa au walio juu ya mamlaka yake.
Siri nyingine ya Makonda ni jasiri na ana msimamo.
Asanteni.

Haya wanaobisha leteni ujinga mwingine.

Msisahau kutuletea cv ya elimu ya Mbowe, aliyewashikia akili zenu na kubaki mazuzu.

hoja binafsi.asanteni
Mbowe siyo saizi ya Daudi Albert Bashite. Hakuwahi kufoji cheti
Alipozungusha O safari yake ya Elimu alikiri. Akaendelea Na jina lake.
 
nilifikiri kitu cha maana kumbe upuuzi tupu!
 
Makonda ni RC, ni wadhifa ambao hauhitaji vyeti wala akupeleka CV kwa Magu, kwa hiyo usimtetea kwa kutumia justification za kitoto, Mbowe alikula zero form 4 aliingia vipi A level ?
Mbona unaruka Kama Samaki wa mkizi,anaruka Kwa jazba na anajimaliza,unataka kunambia kwamba anayeongoza ni sawa sawa na mwandazimu aliyepewa rungu,katiba ya nchi sio katiba ya chama,Huyo mwenyekiti wako wa chama ,amekuwa tayari akizikiuka sheria,Kwa kumpa power RC ambaye wa kuwaongoza wananchi mwenye dhambi zakukosa elimu na fojari,hapo amekosa sifa ya kuwaongoza wananchi wote,lingine Ni nguvu tu zinatumika kukwepa uhalisia,lakini ulimwengu mzima popote utakapokwenda,Meya wa mji ndio kiongozi mkuu wa mji.mnataka kujifanya mnajua sana,Kumbe mnakiuka maadili ya kisheria,ndio maana nikasema umekuwa na ubongo wa samaki wa mkizi,Ni kweli Amani hakukosea mna bongo za samaki.
 
IMG-20170301-WA0011.jpg
 
Back
Top Bottom