Baada ya Dr.Kigwangala, Mwigulu, sasa ni zamu ya Makonda kuhusu jina, hii inaweza kuwa kweli au?

Baada ya Dr.Kigwangala, Mwigulu, sasa ni zamu ya Makonda kuhusu jina, hii inaweza kuwa kweli au?

Haiingii akilini kuja kujisemesha humu kuwa eti safari ya makonda kitaaluma ilikuwa ngumu sababu kipato kilikuwa chini. Huwezi kuwa na kipato cha chini uzunguke mashule na vyuo vingi kiasi icho. Huyu alikuwa anakimbia sup zake tu.

Wanafunzi waliokuwa wanajiweza darasani sikuzote wamesoma kwenye vyuo vya serkal na kupata mkopo 100%
 
Ngoja haters waje
Kila mtu Makonda ana vyeti feki, nani ana ushahidi?

Kuweni Makini na muwe na akiba ya maneno safari bado ndefu, wakati ule tuliaminishwa Lowasa fisadi alipojiunga nasisi kugombea urais saiv tunaona aibu kuzungumzia ufisadi.

Tunzeni akiba ya maneno wakuu, hii skendo hatujui lengo lake nini maana kama ni Makonda alikuepo siku nyingi hata kabla ya kua RC alikua DC Kinondoni na alikua UVCCM huko kwanini hawakuzungumza kuhusu vyeti vyake?

Kwanini watu wanajitahidi kupoteza ishu ya madawa ya kulevya kwa nguvu hivi?

Wewe na Mimi ambao ni wananchi wa kawaida tusiokua na chama tuwe kimya kwanza tusijekujikuta tumetumika kisiasa.

Wengi wetu tuliwahi kutumika kisiasa kumuita Lowassa fisadi, leo mtu asimame aseme Lowassa ni fisadi basi [emoji23] [emoji23] [emoji23]

Najua kuna mapovu yatakuja hapa [emoji23] [emoji23]
 
Jamaa mpuuzi kweli wewe? Yani unaona umeandika kitu tofauti na wengine tunachokifahamu?
 
Historia ya Ndg RC Mhe. Paul Makonda.

Pili ni wapi kunachuo cha u-DC na u-RC mpaka watu wahoji elimu ya Makonda?.
Nilipofikia kusoma hilo swali hapo juu kwenye maelezo yako, NIKASHANGAA SANA na kuona kama Tanzania bado tuna watu wana mtazamo huu, BASI MAENDELEO YENYE TIJA tutayasikia kwa wenzetu tu...

ELIMU YA RAISI ILISHAWAHI KUJADILIWA KUWA IWE ANGALAU DEGREE... chuo gani kinatoa hiyo degree ya uraisi?
 
Ina maana makonda alisoma shule ya msingi kalomje, akaruka hadi chuo cha uvuvi, akaruka hadi chuo cha ushirika moshi kuchukua degree ya uchumi..[emoji15] [emoji15] [emoji15]
 
He
Historia ya Ndg RC Mhe. Paul Makonda.

Nitangulize kuomba radhi kwa ndg Makonda kwa sababu hajanipa ridhaa yake ya kuelezea Historia yake.
Nimelazimika kutoa historia hii ili kuondoa upotoshaji unaoendelea ktk mitandao ya kijamii na mitaani.
Kwa hiyo kosa langu kubwa litakuwa ni hilo

Kwa ufupi Mhe. Makonda ni mhitimu wa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi ndiko alikokupatia Digrii ya uchumi na maendeleo ya jamii.
Hata hivyo safari yake ya kitaaluma ilikuwa ngumu kutokana na hali ya kipato.
Kabla hajaenda Chuo Moshi, alipita ktk shule ya msingi Kolomje na amesoma pia ktk Chuo cha uvuvi Mbegani Bagamoyo ambako alisoma hadi ngazi ya Diploma ktk masuala ya uvuvi.

Safari ya Makonda ya kisiasa ilianzia Chuoni Moshi akiwa waziri mkuu wa Serikali ya wanafunzi.
Amekuwa kiongozi pia ktk Jumuiya ya Vijana CCM kama makamu Mwenyeki taifa nk.
Hakuna asiyejua misukosuko na minyukano ya kisiasa ndani ya CCM vijana walivyokuwa wanagawika kutokana na wanasiasa mafisadi kuwagawa vijana wa UVCCM.
Makonda alikipigania chama kutokana na misimamo yake lakini alienda mbali zaidi na kuwataja wanasiasa waliokuwa wanawagawa vijana wa CCM kwa rushwa na hila,-jambo ambalo halikuwa rahisi kwa wakati huo.
Hatimaye Rais Kikwete akamteua kuwa Mkuu wa wilaya ya Kinondoni.

Makonda ni mwana CCM ambaye hajapitia mafunzo ya kiitikadi kama wengine lakini siasa za Makonda ni zile zinazoendana na wakati husika na zinawavutia watu wengi lakini pia zinawaumiza vichwa vya wana siasa wengine ndani na nje ya CCM, kiasi kwamba wanamuonea wivu na kutaka kumkwamisha kwa kila namna ili asifanikiwe kwa sababu wanaamini mafanikio yake yatampa umaarufu.
Hili ndilo linalokwamisha maendeleo ya kijamii kutokana na wanasiasa kukwamishana wala hawana huruma na watanzania.

Makonda ni mbunifu, kwani yeye ndiye mwanzilishi wa mashindano kama lile la "Kinondoni Talent Seach" lililopelekea hata baadhi ya wakuu na wabunge mbalimbali nao kuanzisha mashindano ya ligi za mpira wakiziita ligi hizo mara nini nini cup, clab, jock kwa majina yao nk.
Bahati mbaya hawakufanikiwa zaidi ya kutafuta sifa, si hawakujua mwenzao alilenga nini!.

Kwa nini Makonda, kwa nini vyeti na kwa nini utajiri wa Makonda?

Kabla ya Makonda kuibua vita ya biashara ya madawa ya kulevya mambo yaliyozuka hivi sasa ya utajiri, vyeti na mara viongozi wanasema hazingatii sheria. sababu ni...

Kwanza wanaosema Makonda hafuati sheria ni wapumbavu na si wazalendo wa taifa hili na ni wanafiki wakubwa.
Kwa sababu kama hoja ni sheria, sheria zilitungwa tangu lini na hapakuwa na wasimamizi wa sheria wala wauza madawa ya kulevya?.
Na je kwa nini hazikufanya kazi kwa kiwango ambacho amekifikia Makonda?.
Je tatizo ni sheria au tatizo ni watu?.

Pili ni wapi kunachuo cha u-DC na u-RC mpaka watu wahoji elimu ya Makonda?.
Kwani kuendesha vita ya madawa ya kulevya ni kuvunja katiba ya Nchi? au kuendesha vita hii hadi uwe na Digrii au Phd?
Si vita ya kila watanzania wote?.

Tatu suala la utajiri wa Makonda kuhoji kwa wakati huu wa sakata la madawa ya kulevya linawafanya wanaohoji kutudhihirishia kwamba wao ni watetezi wa wafanyabiashara hiyo kwa sababu, watanzania haituingii akilini kabisa;
Yaani kuona mtu ameanzisha mapambano ya madawa ya kulevya halafu mjinga mmoja au kikundi cha watu fulani kinaibuka na swali ambalo halihusiani na agenda ya vita husika.
Vita ya madawa ya kulevya inaingilianaje na utajiri wa mtu?,
Kama waliona kuna haja ya kuhoji kuhusu utajiri wa Makonda kwa nini wakae kimya muda wote huo hadi Makonda aanzishe vita ya madawa ya kulevya?.

Mwisho.
Siri ya mafanikio ya Makonda kisiasa itawachukua muda wanasiasa wengine kuijua kwa sababu wanasiasa wengi wanatamaa ya kupenda sifa na kufanya kila jambo waonekane ni lao au wamelianzisha wao huku lengo lao kuu wasifiwe, lakini pia kung'ang'ana sifa hizo zibaki kwao kwa vyovyote vile.
Kwa Makonda ni tofauti, Makonda yeye anatabia ya kuwatanguliza mbele viongozi wakubwa au walio juu ya mamlaka yake.
Siri nyingine ya Makonda ni jasiri na ana msimamo.
Asanteni.

Haya wanaobisha leteni ujinga mwingine.

Msisahau kutuletea cv ya elimu ya Mbowe, aliyewashikia akili zenu na kubaki mazuzu.

hoja binafsi.asanteni
...mbona hii wanaijua. Kuna jipya lolote??
 
Naimani na mod watachanganya huu uzi na mwengine, maana huyu buku 7 hakuna alichofanya hapa
 
kwa sifa kedekede ulizommwagia makonda
Tegemea kupata cheo hata cha kufungua geti

Umefanya kazi nzuri sana kwa makonda
lazima akukumbuke katika katika ufalme wake.
 
Wana Jamvi nimekuwa nikiangalia na kuona MAWE anayotupiwa RC Makonda kuhusu madai yanayohusu uhalali wa MAJINA na ELIMU yake.

Ninapoandika hivi sisemi Makonda hana mapungufu katika maamuzi na utendaji wake hasa wa juzi juzi, hata hivyo tukiangalia upande mwingine wa SARAFU yaonekana kuna ZAIDI ya CHETI, bali ni kutaka huyu RC afukuzwe kazi, ili WENGINE WAFURAHI.

Kwanza kabisa PROFILE ya Makonda ILIVUJWA maksudi kwa sababu ya watu walio na SABABU zao mbaya ili aonekane mbele ya Mwajiri wake ambaye ni rais kwamba yeye ni MHALIFU mkuu.

Na hivyo KUJARIBU kum influence mwajiri wake indirectly kutumia BLACKMAIL ili AMFUKUZE kazi.

Jambo hili limeendelea kwa muda sasa. Swali langu wanajamvi. Kabla ya kumtupia mawe turudi NYUMA.Waziri Mwigulu Nchemba alikuwa na issue kama hii, mbona ya Makonda kila mtu ANAMTUPIA MAWE?

Ni vizuri tusiwe na DOUBLE STANDARD katika kutoa haki bali tuwe FAIR/na USAWA. bila WIVU, UBAGUZI , na FITINA. Kama Waziri Mwigulu Nchemba HAKUJIUZURU basi TUMWACHE Makonda afanye kazi. Yeye si mkamilifu mara nyingi AMEJIKWAA je hilo ndo tumpe mob justice wampige mawe. ASIYE na DHAMBI na awe wa Kwanza kutupa JIWE!
Wewe usiwe unamchanganya bwana daudi bashite na kina mwigulu au vinginevyo,za huyu jamaa time will tell, ishu ni ukimnyooshea kuna kidole mwenzako vingine vinakunyooshea wewe na si kimoja,it's a law na inaendelea vizuri,acha tu tukashughulikie haka ka bwana daudi kaelewe dunia ni mzunguko na busara na hekima iwe nguzo pekee katika utendaji wake.atulize kipele ashughulikiwe.
 
Hiyo ni historia ya mtu au ulitaka kumaanisha nini? Angeandika historia yake yeye mwenyewe ningekuwa na swali la kumuuliza lakini sasa wewe na hii porojo mgando sijui ulitegemea kuachieve nini hasa. Anyway let me just shut my mouth
 
oops! Tunamuokoa vp nanilii wa daslam? Mbona mi nashndwa,
 
Mbona Mwigulu alishatoa ufafanuzi wa kina humu na tukaelewa?!

Usilete diversion hapa ... RC naye aje atoe ufafanuzi. Ndo maturity hiyo..!
 
Peleka lalamiko kwenye vyombo vya sheria na uwe tayari kutoa ushahidi mkuu, itakua vizuri ukitusaidia kusema yaliyochini ya kapeti
Kuna uwezakano mkubwa wa kisheria hata yeye Magufuli akatumbuliwa ikiwa hiyo phd yake Ni ya mizengwe,Kwa sababu upo ushahidi wa kauli zake kupinga hilo,ambao unamtia hatiani,sheria ni haki na ni kama msumeno hauchagui unakata popote.tusubiri muda mfupi hayo yanakuja.
 
Kitendo cha kamanda SIRO Kumuacha Makonda akitamalaki na vyeti Feki hapa Dasalaam inaonyesha kiongozi wa kanda Maalum anapwaya.

Makonda aliwahi kuhoji utendajikazi wa kamanda Siro kuwa haukizi viwango. nimeanza kuamini,kelele zetu zote hizi na inteligensia zake ameshindwa kufungua jarada la uchunguzi dhidi ya Daudi Bashite! only in Tanzania.

forgery is a criminal offence in the eyes of the law Kamanda Siro!
Hahaha
 
Kuna tofauti kubwa kati ya sakata la Mwigulu na lile la David Bashite. Mwigulu (kwa maelezo yaliyotolewa) alirudia darasa na kutumia jina la mtu mwingine wakati akirudia. Utaratibu kama huo huko nyuma ulikuwepo sana; yaani watu walikuwa wanafeli halafu wanaenda kurudia kwenye shule nyingine. Kuna taarifa Profesa Muhongo alirudia mara saba kabla ya kufaulu! Kujaribu kuleta issue za akina Madelu hapa ni kumpa faraja ya muda tu Bashite!

Tuhuma zinazomkabili Bashite ni kwamba alifeli kidato cha nne (alipata ziro), akachukua (kununua?) vyeti vya mtu mwingine ndio akaingilia katika chuo cha uvuvi Mwanza na kuendelea hadi kuwa bosi wa chipukizi ya chama chetu, DC Kinondoni na sasa RC Dar es Salaam! Mkuu hapa kuna kesi ya jinai ambayo mtu akipatikana na hatia, na mahakama ikafanya kazi kama JPM anavyotaka zifanye, Bashite anakula mvua saba mapema tu. Yaani kiuhalisia wakati wewe unaleta andiko lako hapa Bashite alitakiwa awe anamalizia kuandika maelezo polisi tayari kwa kufikishwa kortini kujibu jinai nyingi ambazo ziko ndani ya sakata hilo!
Weka ushahidi wako hapa jamvini!!!
 
Nimejaribu kusoma Hili bandiko ila..
 
Attachments

  • FB_IMG_1485890173173.jpg
    FB_IMG_1485890173173.jpg
    36.8 KB · Views: 43
Mbowe ana tuhumu kuhusu elimu yake, Mwigulu na Kigwangala pia wana tuhuma, hao wote hawaguswi ila anayepigiwa kelele ni Makonda tu. Tena ukiuliza kuhusu Mbowe ndio utaambiwa elimu si uongozi.
Watanzania wengi ni manyumbu na wanafiki kupita maelezo.

mbowe hana vyeti vya fake au hakununua vyeti kwaiyo bwana mdogo usichanganye madesa , Daudu Alberty Bashite kijana wa Ilomije ana vyeti fake vya bwana Paulo chritian Muyange na baada ya kwenda maakamani Muyange ikawa Makonda , kama Mbowe alinunuq vyeti leta details
 
Back
Top Bottom