Na wengine humu hata hawajui mamazao walitoa wapi ada ziliwapa ujuzi hta wa kuingia Jf!Mimi ni mwanaume, lakini siwezi kumbeza mwanamke kwa hali yake yoyote ile. Hata mwanamke anayeitwa malaya ni mama. Na hataacha kuwa mama hata kama ni mwendawazimu. Umewahi kumwona mwanamke hata ambaye akili yake siyo timamu ameukumbatia mdoli wake? Unapata ujumbe gani? Watu waache kuwabeza wanawake, ni wazazi wetu. Kama humpendi mwanamke fulani sema humpendi lakini hiyo labeling haikubaliki kwa jamii iliyostaarabika.