Baada ya kukamatwa mtoto was El Chapo, Zimepigwa Kinoma Mexico

Baada ya kukamatwa mtoto was El Chapo, Zimepigwa Kinoma Mexico

Hayo ndio madhara ya ufisadi. Mtu anajijenga, anamiliki jeshi dogo kwa kisingizio cha ulinzi binafsi. Anatumia pesa kupenya mihimili muhimu huku vyombo vya ulinzi vimelala. Anatoa misaada kwa fedha chafu hadi jamii inamuamini.

Sasa unafikia hatua kupambana na mtu kama huyu unatumia jeshi sio Polisi na bado casualties kibao! Ana jeshi dogo lenye mafunzo na silaha kali, wananchi pia wanamuunga mkono sababu ya misaada ya pesa chafu.

Tuombe Mungu tuwe na wazalendo wa kulinda Taifa kwa gharama yoyote.

Sent from my SM-A315F using JamiiForums mobile app
Kinachohitajika ni serikali kutenda haki na kuletea raia wake wote maendeleo.
 
sober methadone haitumiki inatolewa muhimbili pekee ! wapo watoto wakishua wanapelekwa na wazazi wao
Anasema madon wengi huwezi kuwakuta sober house. Ingawa watoto wa kishua huwa wao wanaowekwa kwenye mpango mkakati wa masoko yaani hao wanatengenezwa na watu wao wa karibu waingie kwenye uraibu, ili mzigo utembee kwa zungu.
 
Aha kwaiyo tatizo ni ulinzi hafifu yani jamaa anaeza kutoroka.
Makubaliano ya marekani na hizi nchi zenye cartels,marekani Kuna pesa anawapa,hata hapa kikosi Cha kupambana na drugs kinalipwa na marekani,na Obama alishatoa order ya kukamata drug kingpin wa hapa akiwemo mwamba wa magomeni aliyekuwa na mtandao USA
 
Ovidio El chapo Guzman.
 

Attachments

  • Screenshot_20230108-103115_Google.jpg
    Screenshot_20230108-103115_Google.jpg
    24.3 KB · Views: 6
  • Screenshot_20230108-103137_Google.jpg
    Screenshot_20230108-103137_Google.jpg
    24.2 KB · Views: 6
Ndio maana tunawaambia siku zote usipo ziba ufa utajenga ukuta.

Serikali ya Mexico iliachilia hili genge la wauza madawa chini ya kiongozi wao Elchapo (baba) likakua na kujiimarisha kiuchumi na silaha sasa wanafanya wanavyo taka. kila kukicha serikali inahangaika.

Hili ni funzo kwa Serikali yetu ya Tanzania kupitia kitengo cha kupambana na madawa ya kulevya wanapaswa wapambane kikamilifu na kuwatokomeza wauza madawa ya kulevya, vinginevyo mkiwaachia watajiimarisha kiuchumi kupitia biashara hiyo na hivyo kuteteresha hali ya usalama wa nchi yetu.
Naukute hao viongoz wajuu serikalin ndio wauza poda wakuu
 
[emoji1787][emoji1787]
waseahili tunamsemo:
"mchelea mwana.......hulia mwenyewe"
Serikali ya Mexico ilimchekea kabla hajawa na nguvu kubwa na alipo jiimarisha alianza kuwatesa hadi sasa limekuwa genge hatari sio tu mexico bali hata ktk maitafa ya marekani.
Hii biashara inafanywa na magenge mengi tu kule na wote wanazo pesa, viongozi wengi wa serekali wamewekwa na magenge haya. Hata hii kamatakamata ni shinikizo tu kutoka nje. Serekali ya kule ni kivuli cha haya magenge.
Na wanachotaka mtu wao akikamatwa ashtakiwe palepale mexico kwa sababu wanaweza kumtoa wakitaka! Haijalishi yupo polisi au jela.
Na kama hakuna madhara wanamuacha jela lakini kila kitu kinakuwa under control.

Kiufupi jamii za wamexico zinafaidika kutoka kwa hizi cartel na zinawalinda.
Marekani kwa maslai yake ndo hawataki.
Hivo ni vita ya kibiashara.
 
Back
Top Bottom