Baada ya kumsafirisha mke najisikia amani, furaha na wepesi wa kutosha. Ndoa inahitaji umakini usiomithilika

Baada ya kumsafirisha mke najisikia amani, furaha na wepesi wa kutosha. Ndoa inahitaji umakini usiomithilika

Omba katika ndoa usije ukapata mwanamke mwenye gubu na mchafu wa mwili na mazingira utasalimu amri tu.........ndoa isikie kwa wezio omba yasikukute.
Sawa mkuu.

Ila huo uchafu wa mwili si unauona tangu mwanzo?

Sisi wanawake tulivyo mume akikwambia ni mchafu utajitakari mwaka mzima kwa aibu. Ni kwamba huwa hamuwaambii uchafu wao au mnawaambia na bado hawajali?

Wanawake wa hivyo wana matatizo makubwa.
 
Tunashauriwa kuweka akiba , sio kupewa hela yote na kuitumia yote bila kubakiza hata senti.
Kama 7000 inatosha kwa chakula ni sahihi alivyofanya. Sasa inategemea hiyo 3000 inaenda kwenye matumizi gani.

Huyo mke ana akili.
Akili ya kushirikiana na house girl kula ganchi? hii dunia ina mambo kwel.
 
Pamoja na ukorofi wa mkeo, hata wewe hujakomaa au hujawa tayari kuishi kwa ndoa.

TV sio kitu cha kupigania kama baba, na sio kitu cha kulalamika kama mama. Mda wa taarifa, ikiwa wewe ni mpenzi wa kuangalia wanakupa nafasi, ukimaliza waendelee na ratiba zao, sioni cha kulalamika hapo.

Matumizi, ukishatoa Matumizi ya siku (kama ni mtoaji wa siku siku), usipende kurudi nyuma tena kuchungulia.

Mke hatakiwi kukusachi mifuko, yeye sio askari kuanza kufanya searching.

Set rules mkuu, acha kulalamika. Ninachoona, ulitamani tu ule uhuru wa kibachela..kuwa peke yako kidogo.
 
Sawa mkuu.

Ila huo uchafu wa mwili si unauona tangu mwanzo?

Sisi wanawake tulivyo mume akikwambia ni mchafu utajitakari mwaka mzima kwa aibu. Ni kwamba huwa hamuwaambii uchafu wao au mnawaambia na bado hawajali?

Wanawake wa hivyo wana matatizo makubwa.
Asili ya mwanamke ana uwezo wa kuficha na ku-fake tabia zake kwa zaidi ya miaka 10, ukamuona kama malaika na ukaingia mpaka ukamuoa, sasa kuja kujua her 'true colours', ni pale anapo clock miaka 35, 40, 45, zile akili za kuficha na uwezo zina isha kabisa, hapo ndo utalipata la ntema kuni.........
 
Kuishi mwenyewe ni bora zaidi, kuna wanawake kazi yao ni kukupa stress 24/7, unakuta jitu libinafsi na wala halina shukrani hata ulifanyie nini!

Mimi wangu alianza chokochoko za naenda kwetu, huo ukawa wimbo kila muda. Kuna siku akajichanganya, naomba nauli naondoka, nikampa chaap, asubuhi nikampeleka Ubungo. Sasa mwaka wa 3 huu maisha yamekuwa na amani sana, kila siku analilia kurudi..huwa nawaza arudi kunipa stress tena?

NB: Mnaotaka kuoa mjitafakari mara mbili, kuna muda wale jamaa wa KATAA NDOA, wana hoja!
 
sina details sn ila nahisi unambana sana waifu wako, kiasi anakosa visenti vya matumizi yake madogomadogo (hadi akuibie). hiyo sio poa, maana mwingine akianza kumpa, ndio itakuwa tamati ya hiyo ndoa.

hayo ya kuangalia tv, ni madogo, huna haja ya kushindana nao, ww una options nyingi. wape space, na hizo ndo sacrifice za ndoa.

hayo mengine ya kurudisha mke kwao ndo nayaskia leo, hivi bado yapo miaka hii? ili kitokee nini? na je akipata sweet baby mwingine huko? utarudi hapa kufungua uzi mwingine au utaendeleza huu?
Kwanza atarudi na mimba ambambikie,

BTW utaangaliaje Tv ndani na watoto? Bar zimejaa, au basi angenunua ki screen hata cha laki 2 aweke chumbani kwake, swala la vijichenchi, huyu sijui mpare? Mwanamke wako mpe hela, kama humpi acha chenchi achukue, mkeo ndo mhasibu mkuu wa familia yako, kama hutaki achukue chenchi usirudi nazo ndani, na Sokoni nenda mwenyewe ukanunue mahitaji yote kama mpare Mshana Jr 😄
 
Back
Top Bottom