Baada ya kupaona nyumbani kwa marehemu Mafuru, sina budi kusema bado nina safari ndefu sana ya kutafuta pesa

Baada ya kupaona nyumbani kwa marehemu Mafuru, sina budi kusema bado nina safari ndefu sana ya kutafuta pesa

Niliona video fupi mtandaoni ikionyesha msiba wa hayati Mafuru.

Ile ni nyumba au hekalu? Nyumbani kwa marehemu ndani ya fensi pana lami. Nyumba ipo Kijazi fly over geti la nyumba lipo Stand ya Magufuli!!

Ngoja nitafute sana pesa, sitaki kupoteza muda wakuu
Nashauri hiyo pesa ukiipata Jenga Hilo jumba la kifahari Mbinguni/Peponi. Huko hakuna kufa Wala kupotea.
Vya Dunia na fahari zake zooote vitapita Wala havitakusaidia.
 
Kuishi maisha mazuri kila mtu anapenda japo nawakumbusha tu kuwa, huko kwa Mungu kutakuwa kugumu sana. Tutengeneze mambo yetu hapa duniani, muda tunao....
Ukipata kipato kizuri, usisahau kuwasaidia wenye shida lakini muhimu zaidi jitahidi usiwe sababu ya wengine kuishi maisha ya taabu hapa duniani
 
Mimi nawakumbusha tu kuwa, huko kwa Mungu kutakuwa kugumu sana
Tutengeneze mambo yetu hapa duniani
Tunakimbizana na miaka 80 ya hapa duniani tunasahau miaka elf, elf ya huko kwa Mungu
Ndicho wazungu walichofanikiwa kutupumbaza, wao wanavuna madini yetu na kutupa moyo kwamba tubaki masikini ili tuenjoy na Mungu.., kwani wao hawataki kuenjoy na Mungu? Mungu yupo hapa hapa duniani, na maisha ndio haya haya, enjoy.
 
🤣🤣🤣🤣 sasa kwani hajafa?

Huo ndio ukweli mchungu, unahangaika kutafuta mali, unaiba, unakula rushwa, unafisadi nchi, unajenga mahekalu, MWISHO UNAKUFA.

Tena unaanguka kama GUNIA... kishindo!

Kuna faida gani? Kwanini usitafute vitu kidogo ukaridhika tu?
Hata ukiishi mtaroni ukifa unauacha mkuu.
 
Wala hupajui, video tu imekuchanganya.
Kajenga uswahilini kazungukwa na waswahili ila pembeni kuna mshua mmoja tu, ana eneo kubwa.
Kajenga nyumba kwa ndaani kaweka paving blocks.
Sasa ukitaka upate kichaaa kutafuta hela nenda mbweni malindi.

Kuanzia kona ya kuingia mbweni njoo kata kushoto uchungulie kulia kwako au nyoosha kama unaenda jkt kuelekea malindi uchungulie kushoto kwako utalaani kuzaliwa.

Mafuru kajenga uswaaa sana na nasikia eneo alipwa na ba mkwe mzee marehemu SHAO, EX EMPLOYEE TANESCO
Duh ila watu mna data aisee..mpaka aliyempatia kiwanja!

Au ndo maana hajazikwa kwao Mara, mke wa kichagaa alikataa?
 
Pambana kadri uwezavyo lakini duniani hakuna usawa na haki,usawa na haki unaanzia kwenye kifo,kifo anachokufa masikini ndio kilekile anachokufa tajiri,pepo anayoingia tajiri ndio ileile anayoingia masikini,moto anaochomwa tajiri ndio uleule anaochomwa masikini.

Kwenye kifo hakuna tume ya kuwaengua wengine wala kuwekeana mapingamizi.
Nipo msibani kwa marehemu bunju A karibu na mianzini. Hakuna anayelia hata mmoja sijui kwann?
 
Mkuu hata uwe na suruali 200 kwenye kabati hakuna siku utqvaa mbili mbili kwa pamoja.

Wazungu wana hela ila wanaishi kwa kiasi. Pesa inayozidi wanatoa misaada ndio hizi pesa tunazoletewa misaada kuchimba vyoo, Shule bure, matibabu ya TB HIV bure, miradi ya matibabu kwa Mama na Watoto bure.

Sisi wafrika tunawekeza kwenye umimi na Ubaltazsar.

Ndio maana hatuendelei. Uchoyo hauleti maendeleo hata siku moja
Umenena vyema.
Waafrica tusingekuwa wabinafsi nchi zetu zingeendelea sana.
Imagine mtu kapewa dhamana ya kusimamia mradi wa maji ama zahanati ila anaiba ela za mradi na kufanya mradi usikamilike ambapo wananchi wanakosa matibabu na huduma za maji.
Sema tatizo waafrica tunaleana sana. Siku ikitokea tukapata viongozi wenye kuweka miongozo mikali na kuisimamia,naamini tutafika mbali.
 

Attachments

  • 20241111_211746.jpg
    20241111_211746.jpg
    302.5 KB · Views: 5
Niliona video fupi mtandaoni ikionyesha msiba wa hayati Mafuru.

Ile ni nyumba au hekalu? Nyumbani kwa marehemu ndani ya fensi pana lami. Nyumba ipo Kijazi fly over geti la nyumba lipo Stand ya Magufuli!!

Ngoja nitafute sana pesa, sitaki kupoteza muda wakuu
Ndo hajaifaidi kaiacha sasa.

Kikubwa ni legacy aliyoiacha
 
Nimesoma comments zimejaa chuki kwa kweli, watu wameacha kukubali ukweli kuwa jamaa alikuwa anaishi sehemu nzuri enzi za uhai wake ila watu wamebaki jifariji na maneno ya uwoga, chuki, wivu na makasiriko kuwa vyote ameacha duniani kikubwa He lived his best life thats what matter.
kabisa full umasikini mindset na kujifariji kipuuzi.
 
Back
Top Bottom