wanajiamini kwa sababu wameshauwa sana mashetani hao, wameshaona watu wengi wakikata roho mbele yao na mioyo yao imeota sugu. ila yupo Mungu mbabe wa wote.
Mama yao ni mungu wa mazombi na machawa wa Bangladeshi. .
Hawaogopi mtu .
Wanateka watu wanawaibia pesa zao na kuwaua.
Haya naona yanaeneo kwa kasi maana waalishaambiwa kifo ni kifo tu.
Ila mimi bwana ndugu yangu huwezi kumteka kihuni hivyo nitafanya tukio baya sana ambalo litakua ndio mageuzi ya kweli kabisa mpaka kiyama.
Hawa binadamu wa ovu wenye damu na nyama wanajibiwa kiovu hivyo hivyo.
Mungu hakua mjinga aliposema jino kwa jino ,uhai kwa uhai ,Anayemwaga damu ya mtu lazima ya kwake nayo imwagwe. Mungu ni mwema kuliko wa anadamu alielekeza hayo kwa ajili ya kudili na wana wa uzao wa nyoka . Kizazi kiovu kinafutwa kwa kuuawa na sio kuwalalamikia kwenye mitandao. Majitu yasiyomhofu hata Mungu ni vipi utakabiliana nayo zaidi ya kuwapiga vyuma .
Ndio maana hata Mwamposa ana walinzi na makanisa na misikiti haikai tu bila waangalizi kwa sababu wapo watu waovu wasiomhofu Mungu wa anadeza hata kuiba Kanisani na msikitini hata kwa kuvunja. Hawa wanakabiliwa kwa damu na nyama sio kwa maombi. Wakifanya tukio bila kujulikana na kuonekana basi tunawasomea duwa mbaya kuwamaliza na vizazi vyao viwe juu ya laana lakini wakionekana wanapaswa kufyekwa na ni kosa na kuacha uovu utamalaki.
Hata Marekani nchi iliyojaa uovu na waovu lakini wanaofanya matukio kama hayo wakionekana au kurekodiwa wanachukuliwa hatua na kufikishwa mahakamani hata kama ni vyombo vya dola.
Wema na Rehema ni kwa watu wanaomhofu Mungu na kujutia makosa yao. Sasa kwa Tanzania ni wazi kuwa hawa watekaji ni kundi lililohalalisha uovu wao na kuna watu nyuma yao wenye nguvu kubwa ya kisiasa na kifedha.
Kuna mmarekani mmoja nilimuuliza vipi nchi yetu anaionaje ukilinganisha na kwao kuhusu amani.!!
Akasema Tanzania ni nchi nzuri sana lakini kwa sasa wetu wanauawa na kupotea tofauti na walivyokuwa wanaiona Tanzania zamani. Akasema kwao pia watu wanauana sana ila alisema ni kwa sababu silaha ni nyingi sana kwa watu mitaani tofauti na huku kuna watu wasiojulikana na hawajulikani wanaopata silaha na lakini wanawaua watu wasio na hatia na wasio na silaha.
Nilishangaa sana jinsi wageni wanavyofuatilia maisha na mambo ya kwetu kwa undani sana.
Serikali ya CCM imevamiwa na watu wasio na utu na wasiojali kesho ya watangayika zaidi ya wao binafsi na vyeo vyao na mali zao. Ni kakikundi kenye tamaa kubwa sana ya mali bahati mbaya tumeendelea kupata mkuu wa nchi anayejali fedha na mali kuli watu na uhai wao . Ni uasi mkubwa sana katika ardhi aliyoyaweka Muumba wa vyote . Mungu hakuumba fedha bali watu kwa ajili ya kuishi kwa amani na hekima kubwa kwa kuweka sheria za haki kwa kila mmoja kulinda haki za mwingine katika kustawisha jamii nzima na sio wale wenye madaraka na mali peke yao.
Kwa sasa utawala wa awamu hii sheria na haki inawalinda mafisadi na watawala na wakubwa tu wengine wote ni kama takataka kama Bideni alivyowaita wapiga kura wa Trump na baadae Trump akapanda gari la taka na kisha kushinda.
CCM imeshindwa kabisa kusimamia serikali latokeo yake ni muda mchache saa sana amani itakua mashakani maana hakuna anayeamini tena katika vyombo vya dola . Mbaya zaidi Mchengerwa anatuchagulia viongozi wa ngazi za chini za serikali kwa matakwa yake na familia yao. Hali itakayomfanya serikali iwe katika wakati mgumu zaidi maana wa wajumbe na wenyeviti wa serikali za mitaa hawatapata ushirikiano wowote kwa watu na utekelezaji wa shughuli za serikali utakua mgumu mara kumi wa ule wa Magufuli ambaye angalau hakuwa na chembe ya ufisadi na kuwabeba mafisadi hivyo wananchi kidogo walimwelewa na kukubaliana naye kwa kiwango kikubwa zaidi pamoja na mapungufu yake mengine ya kuminya mikutano ya kulalamikia vyeo na madaraka hadharani maana ufisadi ambayo ni kero kubwa alikabiliana nayo kwa kiasi kikubwa sana.