Baada ya muhula huu, Rais Samia Suluhu Hassan anaweza kuchaguliwa kushika kiti hicho mara moja

Baada ya muhula huu, Rais Samia Suluhu Hassan anaweza kuchaguliwa kushika kiti hicho mara moja

Mitano hii anamaliza na anagombea tena mi5
Sisi wananchi wakaazi wa Tanzania ndio tunamtaka[emoji378][emoji95]
Mungu atutunzie tuu[emoji120]
Mama D punguza bana,mtawauwa wenzenu kwa presha eti.
Waambieni tu mama Samia atapiga hii minne tu.
 
Mama D punguza bana,mtawauwa wenzenu kwa presha eti.
Waambieni tu mama Samia atapiga hii minne tu.

Hawa tuwape Muda tuu..... walipokea taarifa za msiba kwa furaha hawakujua John Pombe Magufuli aliyeondoka ameacha kina John Pombe Magufuli wa kutosha!

Halafu wakahisi Samia mwepesi kama Salum wao.

Muda unakuja na watakiri kwa vinywa vyao kwamba wanawake ni jeshi kubwa

Mungu ibariki Tanzania Mungu mbariki rais wetu Samia Suluhu Hassan🇹🇿🔥💪

Alale salama kipenzi chetu John Pombe Magufuli 💔💔
 
Mama ataongoza miaka minne zilizobakia na ataruhusiwa kugombea tena kwa mujibu wa ibara ya 37(5) mara moja tu ambayo itamfanya aongoze kwa miaka 9 tu. Punguza Propaganda soma na uelewe!

You must be a desperate attention seeker. Mchango wako haujaongeza au kupunguza chochote kile. Sana sana ulikimbilia kujibu bila kuelewa nilichoandika!
 
Wanaomsimanga mo dewji kuwa pesa zake za urithi wamsimange na mama samia na urais wake wa kurithi
 
Ukisema mitano mingine ni kama kwa sasa ana kipindi cha miaka mitano ambacho si kweli, kwa sasa hana 5 kamili.
Kifungu cha katiba kilichowekwa hapo juu umekiona? Kama angekua amechukua madaraka chini ya miaka mitatu muda huu angeweza gombea tena mihula 2, yaani kama jpm angefariki 2022 angekua amebakiza miaka 3 kumaliza muhula wake hivyo kama samia angechukulia hapo angeweza gombea mihula 2 tena...
Sasa kwa scenario hii ya sasa, katiba yasema kama makamu atachukua madaraka huku kukiwa kumebaki zaidi ya miaka mitatu ambayo kwa sasa ni minne basi anakua na muhula mmoja mwingine anaruhusiwa kugombea ambao ni miaka mitano tena, hivyo anamaliza hii miaka minne alafu anayo miaka mitano tena kama atapitishwa na chama chake...
 
Kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya 1977 na marekebisho yake yote, baada ya mhula huu mfupi wa urais wake wa kurithi kwa mujibu wa masharti ya Ibara ya 37(5), Rais Samia Suluhu Hassan anaweza kuchaguliwa tena kwa mhula mwingine mmoja. Ibara ya 40(4) ambayo ndiyo inahusika inasema hivi:

Endapo Makamu wa Rais anashika kiti cha Rais kwa mujibu wa masharti ya ibara ya 37(5) kwa kipindi kinachopungua miaka mitatu ataruhusiwa kugombea nafasi ya Rais mara mbili, lakini kama akishika kiti cha Rais kwa muda wa miaka mitatu au zaidi ataruhusiwa kugombea nafasi ya Rais mara moja tu.

Obviously, kulikuwa na sloppiness katika uandishi wa Ibara ya 40(4). Limit ni ya kuchaguliwa sio kugombea. Kama hujachguliwa unaweza kugombea hata mara tano kama alivyofanya Hayati Maalim Seif kule Zanzibar. Ukiisoma ibara hii sanjari na ibara ya 40(1), utabaini kwamba walichokusudia kuweka katika ibara ya 40(4) ni ukomo wa kuchaguliwa na sio ukomo wa kugombea kama waandishi wa Katiba walivyoandika!

Kwa kuwa mhula huu mfupi unazidi miaka mitatu, Rais Samia Suluhu Hassan anaweza kugombea na kuchaguliwa tena kushika kiti hicho mara moja tu, baada ya mhula huu.

Tofauti na ilivyozoeleka, kwa uchaguzi wa 2025, Lissu na wafuasi wake (na Kambi ya Upinzani kwa ujumla) wajiandae kukimbizwa mchakamchaka na mwanamama (iwapo ataamua kugombea).
Kwa marekebishi mazuri yaliyowazi uliyoyaonyesha hapo juu ya ukomo wa kugombea (kuchaguliwa), hii inatuonyesha wazi kwamba katiba yetu itakua na mapungufu mengi hivyo kuhitaji marekebisho au katiba mpya ya wananchi. Nadhani ni wakati muafaka serikali ya CCM iache uoga, tupate KATIBA mpya kwa ustawi wa Taifa letu. Hii katiba ina mapungufu mengi sana, CCM wanaogopa kitu kinaitwa KATIBA mpya.
 
Usiogope
Uhai wetu sote ni mali ya Mungu

Mi10 tena kwa mama rais Samia Suluhu Hassan[emoji1241][emoji95]
Mama usimpangie Mungu. Muulize Kessy atakua anajisikiaje na ile kauli yake ya "Atake asitake"
 
Binadamu anapaswa kupanga mambo yake kama vile atakuwepo for the foreseeable future. Hayo ya kutwaliwa yako kwenye mamlaka nyingine, isiyoshirikisha mtu yeyote!
Anapaswa kupanga lakini siyo kwa kejeli.
 
Hawa tuwape Muda tuu..... walipokea taarifa za msiba kwa furaha hawakujua John Pombe Magufuli aliyeondoka ameacha kina John Pombe Magufuli wa kutosha!

Halafu wakahisi Samia mwepesi kama Salum wao.

Muda unakuja na watakiri kwa vinywa vyao kwamba wanawake ni jeshi kubwa

Mungu ibariki Tanzania Mungu mbariki rais wetu Samia Suluhu Hassan[emoji1241][emoji91][emoji123]

Alale salama kipenzi chetu John Pombe Magufuli [emoji174][emoji174]
Mama Samia ni moto Magufuli anasubiri,kapikwa na JPM na akaiva.
"Acha kazi iendelee"
 
Huyo Samia nae anaweza asifikishe hata hiyo 2025 wewe unaanza kuleta zile arrogance kama za walee waliosema atake asitake lazima aongezewe
Umeanza kuchukua nafasi ya Mungu
 
Mama Samia ni moto Magufuli anasubiri,kapikwa na JPM na akaiva.
"Acha kazi iendelee"
Kwa kweli tumshukuru Mungu kwaajili ya zawadi ya uhai wa John Pombe Joseph Magufuli
Katujengea miundombinu hadi rasilimali watu

Wenzetu wanaona amekufa ila sisi tunaona anaishi kati yetuyetu

Moto ni uleule, Mungu atulindie rais wetu mama Samia Suluhu Hassan
 
Makamu wa Rais mpya ndio atakaeandaliwa kuja kuwa Rais wa awamu ya 7.

Huyu Mama bado hakujiandaa kwa hii nafasi. Si ajabu hata miaka minne isiishe utasikia nae anaumwa tatizo la Moyo, kisha makamu anapasha jaramba.
Kwaiyo huyu mama yuko kwenye awamu ya sita now?
 
Atagombea..tena wanawake wataungana na wao ndio wapiga kura wakuu, sioni wapinzani wakotoboa. 2030 lissu atakua babu mbowe kastaafu nusu chadema imekufa...
Magufuli alipokuja madarakani 2015 alidai kufika 2020 vyama kama Chadema vitakuwa vimekufa sasa leo Magufuli ndio amekufa na hivyo vyama ndivyo vinamzika 26/03/2021.

Mnaporopoka humu kumbukeni msiwe mbali na akili zenu haujui kesho utakuwa wapi.
 
Kifungu cha katiba kilichowekwa hapo juu umekiona? Kama angekua amechukua madaraka chini ya miaka mitatu muda huu angeweza gombea tena mihula 2, yaani kama jpm angefariki 2022 angekua amebakiza miaka 3 kumaliza muhula wake hivyo kama samia angechukulia hapo angeweza gombea mihula 2 tena...
Sasa kwa scenario hii ya sasa, katiba yasema kama makamu atachukua madaraka huku kukiwa kumebaki zaidi ya miaka mitatu ambayo kwa sasa ni minne basi anakua na muhula mmoja mwingine anaruhusiwa kugombea ambao ni miaka mitano tena, hivyo anamaliza hii miaka minne alafu anayo miaka mitano tena kama atapitishwa na chama chake...
Katiba haina vifungu bali ibara, kwa sasa ana miaka almost miaka minne na anaweza miaka mitano ikiwa atapata ridhaa ya chama. Hoja ilikuwa ndogo sana, kutumia mitano tena kana kwamba kwa sasa ana kipindi cha miaka mitano.
 
Back
Top Bottom