P, Mradi wa treni umuhimu wake kila mtu anajua na tumekuwa makini sana na kutumia pesa zetu. Bandari ni tatizo. Kwanini tusikuze bandari ya Tanga wakati tayari kuna mafuta pale au Tanga nayo imejaa!!. Tanga sio mbali sana kama kweli hii bandari ni strategic ingekuwa Tanga na sio Dar. Lakini ukweli ni kwamba hii bandari haitakuwa chini ya bandari zetu sisi ni wadau tu na hii mimi sikubaliani nayo. Mimi sikubaliani na Tanzania kutoa bandari kama kwa nchi nyingine. Uendeshaji wa bandari sitashauri apewe nchi tena tujue China kampuni haziko huru zinaendeshwa kisiasa. China kwa wenyewe hii sio bandari ambayo wanategemea faida bali ni kuweka supply chain yao vizuri tu. Treni , ndege na mradi wa stigler ni wetu huu mradi hautakuwa wetu. Na ndiyo maana ni muhimu kuweka mkataba wazi. Je kuna siri gani kubwa za kuficha zaidi ya umiliki na kwanini wafiche. P mimi nashughulikia mikataba kazini najua kampuni zinavyojua kuiba.
Haya maswali sio kwa P pekee ni ya kujiuliza tu.
1. Na hapa ndiyo tunapishana maana mkataba hauko wazi bandari itakuwa ya nani?
2. Je $10B ni mkopo au ni wezezaji kama Mo wa Simba?
3. Je tunawamilikisha wachina uendeshaji wa bandari Je uendeshaji ukiwa mbovu tutafanyaje? tunaweza kufukuza management na kuweka nyingine kama hao CEO wengine au?
4. Vitu gani ambavyo hatutaruhusu China wafanye? mfano meli ya kijeshi ya USA itaruhusiwa kupiga nanga kwenye bandari hii kama wamekuja kufanya shughuli za kijeshi na JWTZ?
5. Wanasema wanajenga viwanda tunaomba list ya viwanda ambavyo wanavijenga na ni kiasia gani cha $10B ni viwanda? au watakuwa wanauza viwanja kwa wawekezaji wengine . Hapa tusipokuwa makini patajegwa magodown tu!
6. Kwenye matumizi na uhakiki wa ujenzi ni kampuni gani ina hakiki gharama za ujenzi? Nani anaiteua hii kampuni Tanzania au China?
7. Je ni vifaa gani vya ujenzi kama chuma, cement ..... vitatoka tanzania?