Sikio la kufa halisikiagi dawa.
Ushauri maridhawa kama huu hawezi kuufanyia kazi hata siku moja, kwa mantiki kwamba, atapoteza maslahi yake binafsi mengi.
Ni muda sana waTz washapaza sauti zao juu ya kuwaondoa kwa vyovyote hao viongozi vimeo lakini kaziba masikio, siyo kwamba hasikii, anasikia sana.
Hadi hapo wananchi watakapoweza, kuongea lugha moja na kutumia demokrasia yao iliyomo hata kwenye katiba hii mbovu ya viraka iliyopo bado inayotabua mamlaka ya wananchi!
Generation zinabadilika viongozi bado wamekariri akili za raia wa kizazi kilichopita, lakini ipo siku hawataamini kama ambavyo Ruto wa Kenya hakuamini, leo kalazimika kuamini kwa lazima na kuchukua hatua madhubuti ambazo hakutarajia kuzichukua kwa hiari yake, kalazimika kazichukua kwa mashinikizo toka kwa wananchi wenye mamlaka kikatiba.
Nasi ndiko tunakoelekea,
one day yes!