Baadhi ya fani zenye ajira kubwa Duniani: Wazazi somesheni watoto nje Degree za Cyber Security na Aeronautical Engineering

Baadhi ya fani zenye ajira kubwa Duniani: Wazazi somesheni watoto nje Degree za Cyber Security na Aeronautical Engineering

Ah ah
Dah mkuu unatu motivation speaker au ya kweli haya.

Yaani utaamjniwa vipi bila cheti sasa??
Hebu tufafanulie kabla hatujaenda darasani.
Me nilisoma ICT(informational communication technology)
Mzee nawe unauza kava nini...yote maisha kweli
 
Kwa ajira mkuu hapo ni tatizo. Nadhani mimi na wewe tunahusika pia ktk kutengeneza ajira kwa vijana.
Ni sawa kweli tunapaswa kuzitengeneza ajira kwa vijana wenzetu ila mazingira yanayotuzunguka na hata selkali ilipaswa angalau hata kwa miaka 5 hii tatizo la ajira lingepungua kwa namna moja ama nyingine ila tukiangalia ajira za selkali sidhani kama ni nyingi kipindi hiki kama miaka ya nyuma
 
Changamoto ya watanzania tulio wengi tunaona course yenye jina gumu basi ndio hot cake. Iyo ulioitaja Aeronautical engineering sio kama unavodhani ni rahisi kupata ajira. Aliesoma iyo course akirudi Tanzania ku[ata ajira sio kazi rahisi sababu apa nchini kuna makampuni yanahitaji zaidi Aircraft Maintenance Engineer + license sasa ukitoka chu ako na iyo degree yako bila kua na license utasota sana labda ujuane na mtu akusaidie. Vijana wengi wa kitanzania sasa wana degree za Aeronautical Engineering wako mtaani na kupata kazi nje ya nchi sio rahisi kama tunavyodhani, wengi wamerudi Tanzania baada ya kutofanikiwa kupata kazi nje ya nchi.
Waombe jeshini
 
Certificate zinakubeba sana ,tatizo gharama kuna kipindi nilikuwa nilisha soma CCNP R and S ,tatizo hela ya kufanyia pepa ilikata na issue yenyewe nikapiga chini ila nataka nipige CCNA cyber ops,nilishaanza kuisoma najua mpaka Mwisho wa mwaka Mungu akijalia nitakuwa ninayo.
Hongera kwa hiyo hatua.Nakuombea ufanikiwe ili tuongeze wataalamu wa cyber nchini wenye soko hadi kimataifa.
 
Labda ni sahihi kwa upande wao.Sababu huu uwanja hauhitaji sana coding especially entry level. Ila kuna wakati unaweza amua ku-move on.Na kadri unavyoendelea kwenda juu basi kujua programming hakuepukiki.Unaweza kuwa mtaalamu wa career fulani katika level za nchi yako.Ila tukiku-rank according to international standard unakuwa mweupe.Yaweza kuwa hiyo inatokana na mwamko wenyewe wa career husika kwa nchi hiyo.Mfano sisi Tz upande wa Infosec bado.Na hata mtu akiwa hata hatua zile za awali T unaweza kumwita 'professional'.Mfano upande wa cyber security huwa wanajali sana certifications.Na wana cert yao maarufu inaitwa CISSP.Hii ukiwa nayo ndo wanasema umeingia rasmi kwa hii carrier.Ila uliza wabongo wangapi wanayo.Wachache sana.Wengi wanaojiita wataalamu wa cyber kwetu hawana.Kuna mwingine nilimwambia kuhusu certs akanicheka.Akasema dunia ya leo haihitaji certs ni skills tu.Nikasema poa.Ila nakumbuka 2017 TCRA walitoa ajira upande huu.Tukazicheki.Ilikuwa inahitaji experience ya miaka mitatu sijui.Sema niliyomwambia yote aliyakuta.hata hiyo cert ilihitajika.Pamoja na vingine pia.Hata programming ilihitajika pia(java,c).Akachukua maamuzi ya kujiendeleza.So coding inahitajika kwa upande wa level za juu kaka.Kuna article nzuri sana nilikuwa naisoma ntakupatia nikiitafuta tena.Inaeleza vizuri sana.
Ila pia hii nyanja ukiipiga vema ukajiendeleza ukawa tayari kwa ushindani wa kimataifa inakutoa vizuri sana.Kuna jamaa yangu ambaye kwangu ni kama role model wangu kwenye haya mambo aliamua kuikamatia hii ngoma.Kachukua certs zote za entry level. Kajiendeleza akabeba hadi vile vya level za juu.Alikuwa anahudhuria hadi makongamano ya hawa watu huko Marekani.Sasa hivi anafanya kazi UK kama senior kwenye haya mambo,analipwa £500 per day!
Mimi nami nilipanga hii iwe carrier yangu sema nilijitoa nilipoona ina 'multiple layers'.
Mkuu naomba mwongozo nina dogo anamaliza olevel mwaka huu anapenda sana haya mambo, naomba nishauri apige course/certification zipi kwa kuanzia hataki kwenda advance yeye pia ni mtundu wa computer. Physics na number ni mzima pia. Nashukuru
 
Kuna degree Tanzania hamna ila zina soko sana duniani, vijana wa PCM zinawafaa.

Wazazi, mkiwa na pesa na mkiwa na watoto wazuri waliofaulu vizuri PCM pelekeni Ulaya au Marekani wakasome degree za Cyber Security na Aeronautical Engineering.

Ni baadhi ya hot cake degrees, dunia nzima inawataka.
Mie ni Cyber Security ( Penetration tester)... kwa hapa bongo bado maluwe luwe tu, labda wasome huko na wabaki huko huko ulaya.. ila sio hapa bongo
 
Kuna kozi nje ni hot cake ila ukirudi huku utasugua benchi vizuri.

Hiyo Aeronautical Engineering kuna jamaa yangu nilisoma nae A'Level akabahatika kwenda nje kusoma karudi saizi mwaka wa 3 yupo anaendelea kubeba bahasha ya kaki mtaani.

Huwa nikikutana nae mtaani naona ana stress haamini, huwa namwambia mzee baba vyeti tuviweke ukumbusho ndani. Tuendelee kupambana na harakati nyingine za maisha.
 
Hahah kuna mwana alisoma Robortics&Artificial intelligence akajifanya mzalendo akarudi zake bongo.

Kapigwa vumbi balaa hakuna kazi wala nini kajaribu kufanya projects/start up za hapa na pale(Funds zikawa ni kikwazo) akapoteza miaka 4 yake hapa bongo.

Akaona upuuzi huu,akatafuta scholarship yuko Sweden.
Kiherehere kilimponza huyooo!
 
Nakukatalia mimi toka nimalize chuo nina miaka saba,jamaa zangu kwenye field hii ya cyber wana miaka mitano,najua ninacho kiongea.Programming ni shughuli si ya kitoto,programming wana gusa gusa tu ila sio deep,wazuri kwenye Server,Linux,Networking na Database kidogo.

Nina wanangu watatummoja yupo eGA programmer anapiga kazi kampuni mbili,hapo kuna viproject vidogo vidogo vya pembeni kwa wiki hakosi laki tano.

Mwengine kajenga ndani ya mwaka,huyu ndio hatari hii Java na C++ anaipiga tokea yupo advance ,huyu sasa anachukuliwa kutengeneza zile system konki na makampuni makubwa.

Mwengine tulivyo maliza chuo kasema yy hatoajiliwa na kweli sasa komaa kama miaka miaka mitatu,sasa hivi anapata project mfululizo na ndiye aliye nishauri nikazanie code.
Mkuu sio general. Mie by Pro.. ni Mechanical Eng, nina Bacheraol ya IT na nina PGD ya Electrical.. na ni certified Penetration Tester.. programing nilikuwa najua zaidi hata ya ma programer. Kwenye field ya Security nilikuwa nawalaza na ukija kwenye programing na kulaza.. sema now days nimeacha vyote niliona upumbavu nanufaisha watu
 
The majority of entry-level
cybersecurity jobs do not
require coding skills. However, being able to write and understand code may be necessary for some mid-level and upper-level cybersecurity positions that you will become qualified for after you've built a few years of experience.

Huo ndo uhalisia uliopo.
Huyo ameongelea General.. ila mie programing nilikuwa mwiba na security nilikuwa fimbo.. nili balance.. but tanzania ilinivunja moyo nimeacha kabisa.. haya makitu.. nalima tu sasw hivi
 
Course za IT kama una kichwa kizuri unasoma mwenyewe,hiyo cybersecurity hiyo unaweza ukaisomea home mwenyewe na PC yako,Youtube,Torrent kuna tutorial na pdf kibao.

Ila kitu chenye ajira za wazi ni Programming,hiyo cyber haifui dafu kwa programming.Piga zako Java,Python,PHP,C++ utapiga hela mpaka utazikataa .
Ninapo ona comment kama hii humu na pata nguvu ya kuendelea kujifunza programming.
 
Huyo ameongelea General.. ila mie programing nilikuwa mwiba na security nilikuwa fimbo.. nili balance.. but tanzania ilinivunja moyo nimeacha kabisa.. haya makitu.. nalima tu sasw hivi
Mkuu unalima nini?
Ni vitu vya kusikitisha.

Kuna rafiki yangu wa karibu sana anaishi Marekani, yeye yupo upande wa IT huwa ananiambia kazi za field yako na yake yeye nje nje huko.
 
Kuna degree Tanzania hamna ila zina soko sana duniani, vijana wa PCM zinawafaa.

Wazazi, mkiwa na pesa na mkiwa na watoto wazuri waliofaulu vizuri PCM pelekeni Ulaya au Marekani wakasome degree za Cyber Security na Aeronautical Engineering.

Ni baadhi ya hot cake degrees, dunia nzima inawataka.
Ili uje kuajiriwa SENTERO uwe unafatilia IMEI ,IP na MAC Adress za watu?
 
Mkuu unalima nini?
Ni vitu vya kusikitisha.

Kuna rafiki yangu wa karibu sana anaishi Marekani, yeye yupo upande wa IT huwa ananiambia kazi za field yako na yake yeye nje nje huko.
Mahindi, viazi vitamu na vitunguu.
Kwa nje ni kweli wanalipa vizuri field za cyber security hata hapa tanzania kwa baadhi ya maeneo ila ni nadra kuyapata.. watu mnakuwa 20 position moja, inakuwa kama tani vile.
 
Back
Top Bottom