Baadhi ya miradi ya uwekezaji inayoweza kufanywa na wastaafu

Wiki iliyopita nilikuwa morogoro mvomero asee nisiseme Sana ila Tz Kwa upande wa ardhi imebarikiwa sana nitaenda huko kufuga na kulima
Ni kweli, Mkoa wa Morogoro, Katavi, Rukwa na Ruvuma Wana Ardhi nzuri sana ya Kilimo

Ni suala la kuamua tu pamoja na Mtaji
 
Hiyo safi Mkuu

Unaamka asubuhi na Meseji za Miamala kuonesha mauzo ya Jana kwenye miradi yako

Kwa kufanya hivyo, unakuwa na uwezo wa kusafiri Ndani ya Nchi na nje ya Nchi kwaajili ya kupumzika na kutalii

Tujiandae sasa kuwekeza
 
Hongereni kumtunza Mzee wenu Kwa hicho kidogo mnachomtumia

Maisha ya kusubiri kupewa Kwa hisani kama hivyo sio mazuri, ndiyo maana tunakumbushana kujiwekeza

Mzee wenu angefata Ushauri wenu huenda angekuwa mbali kupitia Kilimo ama ufugaji

Kuna Mkulima mmoja, anavuna magunia 3000 hadi 5000 Kwa Mwaka ya Mahindi na Mpunga

Mtu wa hivyo, hata akiwa na shida ya milioni 5 haitaji kuwasumbua Vijana wake kumtumia

Huyo unakuta hiyo hela anayo kwenye akaunti yake tayari
 
Kama utani ila ndo yanayotokea
Hatari sana Mkuu

Kuna vitu ni haki kabisa ya raia lakini tunaona ugumu kuvidai πŸ™Œ

Hatuguswi na jambo hadi likutokee binafsi ama mtu anayekuhusu

Na hayo ndiyo maisha yetu waTZ
 
hatari sana mkuu, tuendelee kutafuta mkate tu, maana watanzania kwa ujumla wetu mpaka tuamke bado sana
Ni kweli Mkuu

Tuendelee kujifunza kuwekeza mdogo mdogo wakati huo ukipata muda nenda usome vitabu vitakavyo kuhamasisha kuwekeza

Baada ya hapo, Uwekezaji unakuwa kwenye damu ya familia maana hata watoto wako utawaambukiza hizo hustle
 
Baadhi walikuwa wanahisi ni mbali, kumbe ni hapo tu

Imagine umebakiza miaka 10 Ustaafu lakini huna hata Mradi mmoja wa kukuingizia hata 20,000 Kwa Siku πŸ™Œ

Tuamke Wakuu, muda haupo upande wetu
Tena ukiangalia hiyo chat ya muda na age retirement unaona muda sio RAFIKI KABISA
 
Tena ukiangalia hiyo chat ya muda na age retirement unaona muda sio RAFIKI KABISA
Ni hakika Mkuu, kumbe waliozaliwa miaka ya 70' wamebakiza miaka 7 hadi 10 tu kabla ya kustaafu

Lakini ukiwakuta mtaani, wako busy balaa kuzifunua sketi na Ulabu πŸ™Œ
 
Yaan, unaweza kuogopa ukiangalia age vs muda wa kustaafu na unaona Bado hujafanya la maana
Kwa kweli wakati ukuta

Unakuta umebakiza miaka 7/8/11 Ustaafu lakini hata kibanda cha Kulala bado hujajenga, wakati huo hata Mradi mmoja hujaanza kuufanya

Ukisikia mtu anatembea na kuongea peke yake njiani ndiyo wakati huo πŸ™Œ

Ni muhimu sana kuanza Uwekezaji mapema
 
Mstafu yoyote asipofanya chochote kwa hela zake,atazila mpaka kufa.Mfano Mama yangu alikuwa Mwalimu mafao yake alipata 92.5M na fedha ya kila mwezi anapata 500K.
Alisitafu na 55,ukiweka makadirio kuwa ataishi 25 yrs to come maana yake ataishi mpaka 80 yrs.Akisema atumie 92.5 kwa miaka hiyo 25 kila mwaka atatumia 3.7M wastani wa 308,000 kwa mwezi,fedha hii ukijumuisha na 500K anayopata kila mwezi maana yake kila mwezi atakuwa na kipato cha 800K.
Kwa mstafu anayeishi wilayani 800,000 ni hela nyingi sana,ukitegemea hana mtoto hata moja anamtegemea.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…