Baadhi ya miradi ya uwekezaji inayoweza kufanywa na wastaafu

Baadhi ya miradi ya uwekezaji inayoweza kufanywa na wastaafu

Wiki iliyopita nilikuwa morogoro mvomero asee nisiseme Sana ila Tz Kwa upande wa ardhi imebarikiwa sana nitaenda huko kufuga na kulima
Ni kweli, Mkoa wa Morogoro, Katavi, Rukwa na Ruvuma Wana Ardhi nzuri sana ya Kilimo

Ni suala la kuamua tu pamoja na Mtaji
 
Shida ya kutoelewa unachosoma. kustaafu ni kupumzika hutafanya kazi kama ulivyokuwa mwanzoni, hutaamka na kukimbizana kama mwanzo, hutashinda kazini kama mwanzo.
Utapita kukusanya maokoto ina maana utakwenda kwenye shughuli zako ila si kwa ubize kama zamani, ni kama kusimamia na kuangalia tu kazi zinavvyoenda.
utakaa chini ya mwembe ina maana kuna wakati utapumzika hii haina maana wewe utakaa tuuuu maisha yako yote, nooo kuna vipindi vya kuburudika na kupiga umbea kwa kuwa shughuli zako ulizozianzisha zinaendelea vizuri na kukulipa huna stressss . ukistaafu sio muda wa kusimamia mijengo.... ni muda wa kupokea kinachozalishwa kwenye mijengo uliyonayo. Kutembelea wajukuu maana yake utakuwa na mitoko yako midogo midogo nje ya mkoa wako kwa raha ukasalimie kwenu au kokote utakako. THINK BIG EEEEEE
Hiyo safi Mkuu

Unaamka asubuhi na Meseji za Miamala kuonesha mauzo ya Jana kwenye miradi yako

Kwa kufanya hivyo, unakuwa na uwezo wa kusafiri Ndani ya Nchi na nje ya Nchi kwaajili ya kupumzika na kutalii

Tujiandae sasa kuwekeza
 
Mkuu Mimi naona Kwa watu wote hata wale wasio ajiriwa!

Unatakiwa itegeshe vitega uchumi vya kudumu biashara ya kudumu ama kilimo endelevu pamoja na ufugaji. Hii itakupa uhakika wa maisha hata kama utapata faida kidogo ni vyako. Ahsantee sana Kwa Uzi huu.

Mzee wangu tulimshauri awekeze kwenye nyuki,ufugaji samaki pamoja na ng'ombe wa maziwa kamwe hakutuelewa kabisa Tena tulionekana sisi tunazitaka Hela zake!

Sasahivi anakumbuka misitu upo binde lipo Hela hamna na sisi tuna mambo yetu ya kuwekeza vilevile anapata laki ama 50k nikiwa nayo au zaidi hata400k mara Moja moja
Hongereni kumtunza Mzee wenu Kwa hicho kidogo mnachomtumia

Maisha ya kusubiri kupewa Kwa hisani kama hivyo sio mazuri, ndiyo maana tunakumbushana kujiwekeza

Mzee wenu angefata Ushauri wenu huenda angekuwa mbali kupitia Kilimo ama ufugaji

Kuna Mkulima mmoja, anavuna magunia 3000 hadi 5000 Kwa Mwaka ya Mahindi na Mpunga

Mtu wa hivyo, hata akiwa na shida ya milioni 5 haitaji kuwasumbua Vijana wake kumtumia

Huyo unakuta hiyo hela anayo kwenye akaunti yake tayari
 
Kama utani ila ndo yanayotokea
Hatari sana Mkuu

Kuna vitu ni haki kabisa ya raia lakini tunaona ugumu kuvidai 🙌

Hatuguswi na jambo hadi likutokee binafsi ama mtu anayekuhusu

Na hayo ndiyo maisha yetu waTZ
 
hatari sana mkuu, tuendelee kutafuta mkate tu, maana watanzania kwa ujumla wetu mpaka tuamke bado sana
Ni kweli Mkuu

Tuendelee kujifunza kuwekeza mdogo mdogo wakati huo ukipata muda nenda usome vitabu vitakavyo kuhamasisha kuwekeza

Baada ya hapo, Uwekezaji unakuwa kwenye damu ya familia maana hata watoto wako utawaambukiza hizo hustle
 
Tena ukiangalia hiyo chat ya muda na age retirement unaona muda sio RAFIKI KABISA
Ni hakika Mkuu, kumbe waliozaliwa miaka ya 70' wamebakiza miaka 7 hadi 10 tu kabla ya kustaafu

Lakini ukiwakuta mtaani, wako busy balaa kuzifunua sketi na Ulabu 🙌
 
Yaan, unaweza kuogopa ukiangalia age vs muda wa kustaafu na unaona Bado hujafanya la maana
Kwa kweli wakati ukuta

Unakuta umebakiza miaka 7/8/11 Ustaafu lakini hata kibanda cha Kulala bado hujajenga, wakati huo hata Mradi mmoja hujaanza kuufanya

Ukisikia mtu anatembea na kuongea peke yake njiani ndiyo wakati huo 🙌

Ni muhimu sana kuanza Uwekezaji mapema
 
Mstafu yoyote asipofanya chochote kwa hela zake,atazila mpaka kufa.Mfano Mama yangu alikuwa Mwalimu mafao yake alipata 92.5M na fedha ya kila mwezi anapata 500K.
Alisitafu na 55,ukiweka makadirio kuwa ataishi 25 yrs to come maana yake ataishi mpaka 80 yrs.Akisema atumie 92.5 kwa miaka hiyo 25 kila mwaka atatumia 3.7M wastani wa 308,000 kwa mwezi,fedha hii ukijumuisha na 500K anayopata kila mwezi maana yake kila mwezi atakuwa na kipato cha 800K.
Kwa mstafu anayeishi wilayani 800,000 ni hela nyingi sana,ukitegemea hana mtoto hata moja anamtegemea.
 
Back
Top Bottom