Baadhi ya Viwanda vya kimkakati alivyoanzisha Mwl. Julius Kambarage Nyerere ambavyo ni magodauni na magofu

NAONA UMEISAHAU GENERAL TYRE MKUU, ONGEZEA HAPO

ova
Abood alikichukua kimoja hapo morogoro kwa ajili ya katani, baada ya muda kakigeuza kuwa godown la katani kutoka nje. Kuna siku nitamueleza mama samia hili, Magufuli aliwahi kumwambia huu ukweli abood. Natamani mama Samia nae amwambie ukweli huu. Mwingine aliyefanya ujinga huu ni Mo
Wapo wengi sana
 
Asante kwa ufafanuzi, maana kati ya marais niliokua na imani nao juu ya utendaji wao mkapa alikua namba moja kwangu, japo mwalimu alikua mbele kifikra na kiutendaji ila nyakati zilimbana, mkapa kwa akili yake nchi hii isingekuwa hapa kama sio yeye.
 
Huenda tungekuwa mbali sana kama maono haya yangeendelezwa.
 
Hili jambo la kuiuza NBC lilimuuma sana Mwalimu... Benki ilikuwa na mtaji mzuri kabisa lakini iliuzwa kwa bei ya kutupwa...
Hii ndio ile ilimpekeka mwalimu mpaka kwa kardinali pengo kwa msaada wa kumzuia mkapa, bahati mbaya pengo nae hakua msaada benki ikauzwa.
 
Abood alichukua moproco, canivas na kingine lakini vyote sijui kama vipo active.
 
Vilikufa kipindi gani?

..Viwanda vingi vilikufa wakati wa Nyerere.

..Na mazingira ya kuendesha viwanda kwa faida hapa Tz ni magumu sana.

..Ni rahisi na faida kwa wenye mitaji kuagiza bidhaa toka nje kuliko kuzalisha bidhaa hizo hapa Tz.

..Wawekezaji wako kwa ajili ya kutengeneza faida, kama kungekuwa na faida ktk kufufua viwanda wawekezaji wasingesita kuvifufua.
 
Mkapa alijua siku zijazo watanzania watakua hawavai nguo.
Eti nasema uongo ndugu zangu ?
 
Hiyo 34 sio mafuta tu hata lami ilitengenezwa hapa hapa nchini sidhani Kama hata miaka mitano kilifikisha baada ya kuanza kazi kikafungwa na watanzania wengi hawajui hilo.
 
Duh tungekuwa mbali Sana,
Mungu amrehemu
Amuweke "panapostahili" unajua wafanyakazi wangapi walipoteza kazi? Halafu wakasitishiwa mafao yao hadi wafikishe miaka 55 na wengi wao wanalipwa pensheni ya kila.mwezi laki moja sidhani Kama serikali inajua kwamba Kuna watu wanaendelea kunyanyasika hadi leo. Malipo ya mkupuo Kama Kuna aliyepata m3 ashukuru Mungu. Anapotajwa Mkapa msimsahau Sumaye na yule mzee mmoja namuonea huruma kuweka jina lake uzi wote utahamia kwake na kichambo juu.
 
Kuna mmoja alishtakuwa kwa JPM kwamba viwanda haendelezi anafungia mbuzi
 
CCM ni janga na watakua wamekunja ndita kuona mleta mada ametoa facts kwa vijana wa kizazi kipya juu ya tulipotoka na tulipo sasa.
Masikini vijana wetu wasingeishia kuvuta bangi maana ajiri zilijuwa za kumwaga hata darasa la Saba anapata kazi anakwenda jiendekeza akiwa kazini
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…