Baadhi ya Viwanda vya kimkakati alivyoanzisha Mwl. Julius Kambarage Nyerere ambavyo ni magodauni na magofu

Baadhi ya Viwanda vya kimkakati alivyoanzisha Mwl. Julius Kambarage Nyerere ambavyo ni magodauni na magofu

NAONA UMEISAHAU GENERAL TYRE MKUU, ONGEZEA HAPO

ova
Abood alikichukua kimoja hapo morogoro kwa ajili ya katani, baada ya muda kakigeuza kuwa godown la katani kutoka nje. Kuna siku nitamueleza mama samia hili, Magufuli aliwahi kumwambia huu ukweli abood. Natamani mama Samia nae amwambie ukweli huu. Mwingine aliyefanya ujinga huu ni Mo
Wapo wengi sana
 
Kabla haujambebesha lawama Mh. Mkapa ni vyema ukaangalia sababu ambazo zilimfanya Mkapa kufikia hatua hiyo.

Iko hivi. Viwanda vingi havikuwa vinajiendesha kwa faida. Serikali ilikuwa ina vipa ruzuku ili viendelee kuwepo. Kuna sababu mbalimbali ambazo zilisababisha haya.
1. Management Mbovu. Wabongo tunajijua. Pamoja na kwamba Nyerere alijitahidi kusomesha watu na kuwapa nafasi..wengi walimuangusha.

2. Technolojia iliyopitwa na wakati. Baadhi ya viwanda alikuwa anapewa msaada...vilikuwa vimeshapitwa na wakati. Kumbe wale jamaa walikuwa wanatafuta sehemu ya kuvitupa. Wao wana move kwenye tech mpya ile ya zamani ndo wanawa wapa au kuwauzia. Hivyo ilikuwa gharama kubwa kuviendesha na havikuwa na ubora kama vya ulaya. Hivyo kufanya kutokuwa na ushindani katika soko. Maana una produce low quality at high cost.

So kipindi cha Mwinyi vingi ya hivyo viwanda vilifungwa. Hali ilikuwa mbaya sana. Watu walikaa nyumbani huku wakiendelea kulipwa mishahara.

Mkapa alipokea nchi ikiwa namna hiyo. Yaani una watu wako nyumbani wanalipwa mishahara. Una viwanda ambavyo havifanyi kazi na technolojia yake imepitwa na wakati.

Je utafanya nini.?

Mkapa aliamua kuvibinafsisha. Kwa sababu ni dhahiri serikali haiwezi kuendesha miradi ya kibiashara. Angali tu kwa mfano Mabasi ya Mwendo kasi, Angalia Tanesco etc..zote zinaendeshwa kwa ruzuku.

Sasa kwa nini uchukue gela ya walipa kodi uvipe viwanda visivyoingiza faida.?

Hivyo Mkapa akaamua kuvibinafsisisha. Ili private investors waendeshe na watoe ajira. Akawapunguza wafanyakazi kwa kuwalipa haki zao ili wasiendelee kula mishahara bila kazi.

Kuna tuhuma kwamba Mkapa aliuza viwanda kwa bei rahisi bei ya kutupa. Ukweli ni kwamba ingawa vilikuwa vinaitwa viwanda...havikuwa viwanda kiuhalisia. Mitambo yake mingi ilikuwa ya kizamani na haifanyi kazi. Hivyo Mkapa aliuza vyuma chakavu na majengo.

Baadhi ya walionunua walifanya vizuri..Viwanda kama TBL vinafanya vizuri hadi sasa. Ila baadhi ya walio nunua walivigeuza ma godown na wao ukiwauliza kwa nini hawakuviendeleza wana sababu zao.
Asante kwa ufafanuzi, maana kati ya marais niliokua na imani nao juu ya utendaji wao mkapa alikua namba moja kwangu, japo mwalimu alikua mbele kifikra na kiutendaji ila nyakati zilimbana, mkapa kwa akili yake nchi hii isingekuwa hapa kama sio yeye.
 
  • Kiwanda cha nyembe Perma Sharp
  • Kiwanda cha magunia - Tanzania Bag Corporation (hivi vilikuwa viwili kwa pamoja MILL I na MILL II)
  • Viwanda vya Sukari TPC na Kilombero
  • Kwanda cha mafuta - MAPROCO Morogoro na kingine cha Mwanza/Shinyanga nimekisahau jinakilichokuwa
kinatengeneza mafuta ya Tanbond na Supa Ghee
- Kiwanda cha baiskel - Swala
Huenda tungekuwa mbali sana kama maono haya yangeendelezwa.
 
Hili jambo la kuiuza NBC lilimuuma sana Mwalimu... Benki ilikuwa na mtaji mzuri kabisa lakini iliuzwa kwa bei ya kutupwa...
Hii ndio ile ilimpekeka mwalimu mpaka kwa kardinali pengo kwa msaada wa kumzuia mkapa, bahati mbaya pengo nae hakua msaada benki ikauzwa.
 
Abood alikichukua kimoja hapo morogoro kwa ajili ya katani, baada ya muda kakigeuza kuwa godown la katani kutoka nje. Kuna siku nitamueleza mama samia hili, Magufuli aliwahi kumwambia huu ukweli abood. Natamani mama Samia nae amwambie ukweli huu. Mwingine aliyefanya ujinga huu ni Mo
Wapo wengi sana
Abood alichukua moproco, canivas na kingine lakini vyote sijui kama vipo active.
 
Vilikufa kipindi gani?

..Viwanda vingi vilikufa wakati wa Nyerere.

..Na mazingira ya kuendesha viwanda kwa faida hapa Tz ni magumu sana.

..Ni rahisi na faida kwa wenye mitaji kuagiza bidhaa toka nje kuliko kuzalisha bidhaa hizo hapa Tz.

..Wawekezaji wako kwa ajili ya kutengeneza faida, kama kungekuwa na faida ktk kufufua viwanda wawekezaji wasingesita kuvifufua.
 
Mkapa alijua siku zijazo watanzania watakua hawavai nguo.
Eti nasema uongo ndugu zangu ?
 
Hivi ni baadhi tu ya Viwanda vya kimkakati alivyoanzisha Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere bahati Mbaya vingi ni magodauni na magofu vijana inawezekana mmesahau

1. TANGANYIKA PACKERS - usindikaji,upakiaji na usambazaji wa nyama ya ng'ombe. Kiwanda hiki kilikuwa Kawe na kingine mkoani Shinganya.
2. URAFIKI,Nguo 3.MWATEX, Nguo
4. KILTEX,Nguo
5. MUTEX, Nguo
6. POLYTEX- Nguo, vitenge
7. MOROGORO CANVAS - MAGUNIA, MATURUBAI
8. MOROGORO SHOES- VIATU
9. MOROGORO TANNERIES- NGOZI.
10. MWANZA TANNERIES- NGOZI.
11. BORA SHOES- UTENGENEZAJI WA VIATU.
12. KIBO MATCH FACTORY- Viberiti.
13. NATIONAL, MATSUSHITA, PHILLIPS- Utengenezaji wa batteries, radio na radio cassete.
14. PAMBA ENGINEERING- Uchongaji wa vipuri vya mashine za uchambuaji pamba.
15. SIDO - Shirika la kuhudumia viwanda vidogo
16. Kiwanda cha kubangua Korosho Mtwara
17.Viwanda vya kusindika na kubangua , Kahawa, Alizeti, Pareto, Karanga na Miwa. Morogogo/Kilimanjaro/Singida
18. Kiwanda cha vipuri vya mashine cha Mang'ula
19. Kiwanda cha vipuri za mashine cha Kilimanjaro
20. Kiwanda cha malori (kuunda mabasi na malori) cha Scania.
21. Kiwanda cha magari cha Nyumbu cha jeshi Kibaha.
22. TANALEC- kiwanda cha kutengeneza vifaa mbalimbali vya umeme.
23. Kiwanda cha karatasi cha Mgororo Mufindi mkoani Iringa.
24. Kiwanda cha kusindika na kusambaza maziwa cha UTEGI mkoani Mara.
25. Kiwanda cha usindikaji wa nafaka cha National Milling Corporation cha Dar-es-Salaam.
26. Tanga Steel Rolling Mill- vyuma, saruji na mabati.
27. Viwanda vya saruji vya Tembo Cement, Twiga Cement, Simba Cement pamoja na vile vya ALAF na GALCO.
28. Kiwanda cha zana za kilimo - UFI
29. Kiwanda cha madawa ya binadamu cha KPC - Keko Pharmaceutical Company.
30. Viwanda vya Bia vya Dar, Ndovu na Pilsner Arusha
31. Kiwanda cha Mvinyo Dodoma
32. Kiwanda cha matairi cha General Tyre kilichopo Arusha
33. Kiwanda cha katani cha Amboni mkoani Tanga.
34. TIPER - kiwanda cha kusafisha mafuta machafu, kusambaza mafuta ya dizeli, petrol na mafuta ya taa.j
Hiyo 34 sio mafuta tu hata lami ilitengenezwa hapa hapa nchini sidhani Kama hata miaka mitano kilifikisha baada ya kuanza kazi kikafungwa na watanzania wengi hawajui hilo.
 
Duh tungekuwa mbali Sana,
Mungu amrehemu
Amuweke "panapostahili" unajua wafanyakazi wangapi walipoteza kazi? Halafu wakasitishiwa mafao yao hadi wafikishe miaka 55 na wengi wao wanalipwa pensheni ya kila.mwezi laki moja sidhani Kama serikali inajua kwamba Kuna watu wanaendelea kunyanyasika hadi leo. Malipo ya mkupuo Kama Kuna aliyepata m3 ashukuru Mungu. Anapotajwa Mkapa msimsahau Sumaye na yule mzee mmoja namuonea huruma kuweka jina lake uzi wote utahamia kwake na kichambo juu.
 
Kinachosikitisha sana ni kwamba vimekaliwa na Waasia na matajiri wengine wenye asili ya kiarabu wakitumia kama ma Godown ya kuhifradhia bidhaa wanazoagiza kutoka nje ambazo wala hazifikii ubora wa zile zilizokuwa zinazalishwa na hivyo viwanda. Kwa maksudi kabisa ya kulihujumu Taifa.

Haya mambo yako wazi kabisa, wanasiasa wakiamua kuyafanyia uchunguzi ukweli wote utabainika na hatua stahiki kuweza kuchukuliwa. Hapo ndiyo pale baadhi ya viongozi walijaribu kufahamu nini kilichoko nyuma ya huo uhujumu uchumi, lakini wakaishia kukiri kuwa makaburi mengine ni hatari kuyafukua.

Hapo ikimaanisha kuwa kuna baadhi ya watu hapa nchini ambao wako juu ya sheria na Hawagusiki!
Kuna mmoja alishtakuwa kwa JPM kwamba viwanda haendelezi anafungia mbuzi
 
CCM ni janga na watakua wamekunja ndita kuona mleta mada ametoa facts kwa vijana wa kizazi kipya juu ya tulipotoka na tulipo sasa.
Masikini vijana wetu wasingeishia kuvuta bangi maana ajiri zilijuwa za kumwaga hata darasa la Saba anapata kazi anakwenda jiendekeza akiwa kazini
 
Back
Top Bottom