Baadhi ya Viwanda vya kimkakati alivyoanzisha Mwl. Julius Kambarage Nyerere ambavyo ni magodauni na magofu

Bado mnalia lia tuu viwanda vimejifia miaka 30 iliyopita na hata vilipokuwa vinafanya kazi ilikuwa ni hasara tupu, na hivyo viwanda sio vya mkakati ni viwanda vidogo vidogo tuu, viwanda vya mkakati ni kama chuma na aluminium, hivyo viwanda watu binafsi waanze kujenga vipya na vya kisasa sio serikali tena, fursa hiyo sio mnalialia tuu
 
Hiyo siyo sababu ya kuua na kuuza viwanda vyoote hivyo. Wapi uliona upembuzi yakinifu uliotumika kufikia uamuzi huo? Huwezi kuamua kuua viwanda na mashirika mengi namna hiyo. Kwanini asitembee kutafuta ushauri wa kitaalam hata nchi za nje? Kwa nchi ni afadhali ku-negotiate mikopo yenye masharti nafuu kuliko kuzima uchumi wa nchi nzima. Unatetea nini Mkuu wakati yeye mwenyewe alifika mahali akakiri hadhani kuwa alifanya makosa? Ila inakubidi ukumbuke kuwa wakati anakiri hilo alikwisha kuwaita waliopinga maamuzi yake jina baya "Makanjanja" . Hakuna kitu kibaya kama ulevi wa madaraka.
Kulikuwa hakuna viwanda pale vyote vilikuwa vinaendeshwa kwa hasara kubwa sana, imagine kiwanda kama cha beer TBL na wateja walivyokuwa wengi walikuwa wanauza beer kwa mgawo kwa sababu walishindwa kuzalisha, hivyo viwanda vyote havikuwa vya mkakati, ningewaelewa kama wangewekeza na kuhakikisha viwanda kama vya chuma na mbolea vinafanikiwa lakini sio viwanda vya ngozi na viberiti, bora vilikufa tuu maana ilisaidia serikali kushusha zigo la ruzuku kwa mambo ya kipuuzi kama viwanda vya viatu, time sasa muonyeshe uzalendo muanzishe viwanda hata vya viberiti sio kuchangiana harusi tuu
 
Serikali haipaswi fanya biashara
Basi tusinunue TV za Hisense na magari ya Fuso kiutoka China kwani ni viwanda vya serikali ya China. Viwanda vikubwa nchini China ni vya seriikali; kwa mfano viwanda vya magari, viwanda vya ndege, viwanda vya materni, na mabenki kama exim bank nayo ni ya serikali.
 
Hiyo siyo sababu ya kuua na kuuza viwanda vyoote hivyo. Wapi uliona upembuzi yakinifu uliotumika kufikia uamuzi huo? Huwezi kuamua kuua viwanda na mashirika mengi namna hiyo. Kwanini asitembee kutafuta ushauri wa kitaalam hata nchi za nje? Kwa nchi ni afadhali ku-negotiate mikopo yenye masharti nafuu kuliko kuzima uchumi wa nchi nzima. Unatetea nini Mkuu wakati yeye mwenyewe alifika mahali akakiri hadhani kuwa alifanya makosa? Ila inakubidi ukumbuke kuwa wakati anakiri hilo alikwisha kuwaita waliopinga maamuzi yake jina baya "Makanjanja" . Hakuna kitu kibaya kama ulevi wa madaraka.

..viwanda vilidorora au kufa wakati wa utawala wa mwalimu nyerere, na ndio maana kulikuwa na uhaba wa kila bidhaa hata mkate wa boflo watu walikuwa wanapanga foleni.

..kwa kweli mnafanya makosa makubwa sana kusema uongo kwamba mkapa aliua viwanda hapa tanzania, wakati mkijua matatizo yalianzia ktk awamu ya kwanza.

..kosa alilokiri mkapa ni kutokuwa na utaratibu wa kuwasimamia na kuhakikisha waliouziwa viwanda ktk zoezi la ubinafsishaji wanavifufua viwanda hivyo. mkapa hajawahi kusema kwamba alikosea kubinafsisha au hakukuwa na ulazima wa kubinafsisha viwanda na mashirika ya umma.

..tumsikilize mkapa hapa chini ili kujiridhisha kuhusu alichokisema.

Bado mnalia lia tuu viwanda vimejifia miaka 30 iliyopita na hata vilipokuwa vinafanya kazi ilikuwa ni hasara tupu, na hivyo viwanda sio vya mkakati ni viwanda vidogo vidogo tuu, viwanda vya mkakati ni kama chuma na aluminium, hivyo viwanda watu binafsi waanze kujenga vipya na vya kisasa sio serikali tena, fursa hiyo sio mnalialia tuu
Wewe unaweza kujenga hata cha matofali? mbona unajitoa? ndo uvivu wenyewe kufikiri kuna watu zaidi yako wa kujenga viwanda
 
Hivi ni baadhi tu ya Viwanda vya kimkakati alivyoanzisha Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere bahati Mbaya vingi ni magodauni na magofu vijana inawezekana mmesahau

1. TANGANYIKA PACKERS - usindikaji,upakiaji na usambazaji wa nyama ya ng'ombe. Kiwanda hiki kilikuwa Kawe na kingine mkoani Shinganya.
2. URAFIKI,Nguo 3.MWATEX, Nguo
4. KILTEX,Nguo
5. MUTEX, Nguo
6. POLYTEX- Nguo, vitenge
7. MOROGORO CANVAS - MAGUNIA, MATURUBAI
8. MOROGORO SHOES- VIATU
9. MOROGORO TANNERIES- NGOZI.
10. MWANZA TANNERIES- NGOZI.
11. BORA SHOES- UTENGENEZAJI WA VIATU.
12. KIBO MATCH FACTORY- Viberiti.
13. NATIONAL, MATSUSHITA, PHILLIPS- Utengenezaji wa batteries, radio na radio cassete.
14. PAMBA ENGINEERING- Uchongaji wa vipuri vya mashine za uchambuaji pamba.
15. SIDO - Shirika la kuhudumia viwanda vidogo
16. Kiwanda cha kubangua Korosho Mtwara
17.Viwanda vya kusindika na kubangua , Kahawa, Alizeti, Pareto, Karanga na Miwa. Morogogo/Kilimanjaro/Singida
18. Kiwanda cha vipuri vya mashine cha Mang'ula
19. Kiwanda cha vipuri za mashine cha Kilimanjaro
20. Kiwanda cha malori (kuunda mabasi na malori) cha Scania.
21. Kiwanda cha magari cha Nyumbu cha jeshi Kibaha.
22. TANALEC- kiwanda cha kutengeneza vifaa mbalimbali vya umeme.
23. Kiwanda cha karatasi cha Mgororo Mufindi mkoani Iringa.
24. Kiwanda cha kusindika na kusambaza maziwa cha UTEGI mkoani Mara.
25. Kiwanda cha usindikaji wa nafaka cha National Milling Corporation cha Dar-es-Salaam.
26. Tanga Steel Rolling Mill- vyuma, saruji na mabati.
27. Viwanda vya saruji vya Tembo Cement, Twiga Cement, Simba Cement pamoja na vile vya ALAF na GALCO.
28. Kiwanda cha zana za kilimo - UFI
29. Kiwanda cha madawa ya binadamu cha KPC - Keko Pharmaceutical Company.
30. Viwanda vya Bia vya Dar, Ndovu na Pilsner Arusha
31. Kiwanda cha Mvinyo Dodoma
32. Kiwanda cha matairi cha General Tyre kilichopo Arusha
33. Kiwanda cha katani cha Amboni mkoani Tanga.
34. TIPER - kiwanda cha kusafisha mafuta machafu, kusambaza mafuta ya dizeli, petrol na mafuta ya taa.j
Tungekuwa mbali sana.... Ila Mkapa si mchezo inaelekea Kambarage alivyodondoka alipata washauri mabeberu
 
Kweli ila kuna wengine ni kiongozi wa chama cha upinzani hajui kwe

Kweli ila kuna wengine ni kiongozi wa chama cha upinzani hajui kweli?.
Mkuu upinzani
..mnamsingizia Nkapa kuwa aliua viwanda.

..Waziri Mkuu Sokoine aliwahi kutembelea mikoa ya kusini akakuta wananchi wanavaa kaniiki.

.Sasa kama viwanda vya nguo vya Nyerere vilikuwa vinazalisha kwanini wananchi walilazimika kuvaa kaniki?

..Hapo kuna maana moja tu kwamba viwanda vilikuwa vimekufa au vimedorora tangu wakati wa Mwalimu.

..Pia maeneo ya mijini kila wakati kulikuwa na kurupushani za mgambo na JKT kukamata wazururaji na kuwapeleka wakalimu. Hali hiyo ilisababishwa na tatizo la ukosefu wa ajira. Kama viwanda vingekuwa vinazalisha na kutoa ajira tusingekuwa na tatizo la wazururaji enzi za Mwalimu Nyerere.

..Mwalimu alikuwa na nia njema kabisa kuanzisha viwanda. Lakini wakati wa utekelezaji wa nia hiyo tulikosea na kushindwa kukabiliana na changamoto za kukuza viwanda tulivyoanzisha.

..Kuna umuhimu wa kuambiana ukweli kuhusu viwanda vyetu vinginevyo hatutajifunza kutokana na makosa yetu.
Kauua
 
Tungekuwa mbali sana.... Ila Mkapa si mchezo inaelekea Kambarage alivyodondoka alipata washauri mabeberu

..tungekuwa mbali kivipi?

..kulikuwa na FOLENI mpaka za mkate wa boflo.

..kulikuwa na uhaba wa bia ukiwa na sherehe ilibidi upate KIBALI serikalini kununua bia.

..wananchi wa kusini walikosa nguo wakawa wanavaa KANIKI.

..ukweli ni kwamba tulianzisha viwanda lakini tuliviendesha vibaya na kilichotuponza ni siasa za Ccm kuingilia utendaji.

..pia wapo viongozi ambao walimshauri Mwalimu Nyerere atafute wabia, na wawekezaji, ktk viwanda na mashiriki, lakini ushauri huo ulipingwa, na walioutoa waliitwa WASALITI wa Ujamaa.

..Kosa letu lilikuwa kuchelewa kubinafsisha tukajikuta tunafanya hivyo wakati viwanda vimekufa.

NB:

..Ubinafsishaji wa Tanzania Breweries ulipingwa sana. Watu walikasirika kwasababu aliyeuziwa ni KABURU.

..lakini wakati Breweries inabinafsishwa bia zilikuwa haba. Quality ya bia ilikuwa mbaya, wakati mwingine bia zilikuwa na uchafu. Kampuni ilikuwa imekwama ktk ujenzi wa kiwanda cha Mbeya.

..Tanzania Breweries ni moja ya makampuni ambayo yalibinafsishwa at the right time, to the right investor.
 
Mbona Komoni ilikuwepo..
images (19).jpeg

IMG_4180.JPG
IMG_4180.JPG
IMG_4180.JPG
 
Hivi ni baadhi tu ya Viwanda vya kimkakati alivyoanzisha Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere bahati Mbaya vingi ni magodauni na magofu vijana inawezekana mmesahau

1. TANGANYIKA PACKERS - usindikaji,upakiaji na usambazaji wa nyama ya ng'ombe. Kiwanda hiki kilikuwa Kawe na kingine mkoani Shinganya.
2. URAFIKI,Nguo 3.MWATEX, Nguo
4. KILTEX,Nguo
5. MUTEX, Nguo
6. POLYTEX- Nguo, vitenge
7. MOROGORO CANVAS - MAGUNIA, MATURUBAI
8. MOROGORO SHOES- VIATU
9. MOROGORO TANNERIES- NGOZI.
10. MWANZA TANNERIES- NGOZI.
11. BORA SHOES- UTENGENEZAJI WA VIATU.
12. KIBO MATCH FACTORY- Viberiti.
13. NATIONAL, MATSUSHITA, PHILLIPS- Utengenezaji wa batteries, radio na radio cassete.
14. PAMBA ENGINEERING- Uchongaji wa vipuri vya mashine za uchambuaji pamba.
15. SIDO - Shirika la kuhudumia viwanda vidogo
16. Kiwanda cha kubangua Korosho Mtwara
17.Viwanda vya kusindika na kubangua , Kahawa, Alizeti, Pareto, Karanga na Miwa. Morogogo/Kilimanjaro/Singida
18. Kiwanda cha vipuri vya mashine cha Mang'ula
19. Kiwanda cha vipuri za mashine cha Kilimanjaro
20. Kiwanda cha malori (kuunda mabasi na malori) cha Scania.
21. Kiwanda cha magari cha Nyumbu cha jeshi Kibaha.
22. TANALEC- kiwanda cha kutengeneza vifaa mbalimbali vya umeme.
23. Kiwanda cha karatasi cha Mgororo Mufindi mkoani Iringa.
24. Kiwanda cha kusindika na kusambaza maziwa cha UTEGI mkoani Mara.
25. Kiwanda cha usindikaji wa nafaka cha National Milling Corporation cha Dar-es-Salaam.
26. Tanga Steel Rolling Mill- vyuma, saruji na mabati.
27. Viwanda vya saruji vya Tembo Cement, Twiga Cement, Simba Cement pamoja na vile vya ALAF na GALCO.
28. Kiwanda cha zana za kilimo - UFI
29. Kiwanda cha madawa ya binadamu cha KPC - Keko Pharmaceutical Company.
30. Viwanda vya Bia vya Dar, Ndovu na Pilsner Arusha
31. Kiwanda cha Mvinyo Dodoma
32. Kiwanda cha matairi cha General Tyre kilichopo Arusha
33. Kiwanda cha katani cha Amboni mkoani Tanga.
34. TIPER - kiwanda cha kusafisha mafuta machafu, kusambaza mafuta ya dizeli, petrol na mafuta ya taa.j
Viwanda vya kukoboa na/ au kusaga nafaka (Nationa Milling) vilikuwepo angalau kimoja kila mkoa
 
..tungekuwa mbali kivipi?

..kulikuwa na FOLENI mpaka za mkate wa boflo.

..kulikuwa na uhaba wa bia ukiwa na sherehe ilibidi upate KIBALI serikalini kununua bia.

..wananchi wa kusini walikosa nguo wakawa wanavaa KANIKI.

..ukweli ni kwamba tulianzisha viwanda lakini tuliviendesha vibaya na kilichotuponza ni siasa za Ccm kuingilia utendaji.

..pia wapo viongozi ambao walimshauri Mwalimu Nyerere atafute wabia, na wawekezaji, ktk viwanda na mashiriki, lakini ushauri huo ulipingwa, na walioutoa waliitwa WASALITI wa Ujamaa.

..Kosa letu lilikuwa kuchelewa kubinafsisha tukajikuta tunafanya hivyo wakati viwanda vimekufa.

NB:

..Ubinafsishaji wa Tanzania Breweries ulipingwa sana. Watu walikasirika kwasababu aliyeuziwa ni KABURU.

..lakini wakati Breweries inabinafsishwa bia zilikuwa haba. Quality ya bia ilikuwa mbaya, wakati mwingine bia zilikuwa na uchafu. Kampuni ilikuwa imekwama ktk ujenzi wa kiwanda cha Mbeya.

..Tanzania Breweries ni moja ya makampuni ambayo yalibinafsishwa at the right time, to the right investor.
Kwanini hii bidhaa moja ndiyo inayochukua nafasi kubwa kwenye mawazo yako? Unataka kuniambia NBC ilikuwa na sababu ya kuuzwa, ATC? Viwanda vya kubangua korosho? vya kusindika mafuta nk. nk? Nakushauri ungalie mambo kwa upana zaidi, lakini kama ulikuwa ni mfaidika wa huo mkakati ni bora ukatulia maana hutaweza kutuelewa hata kidogo.
 
..viwanda vilidorora au kufa wakati wa utawala wa mwalimu nyerere, na ndio maana kulikuwa na uhaba wa kila bidhaa hata mkate wa boflo watu walikuwa wanapanga foleni.

..kwa kweli mnafanya makosa makubwa sana kusema uongo kwamba mkapa aliua viwanda hapa tanzania, wakati mkijua matatizo yalianzia ktk awamu ya kwanza.

..kosa alilokiri mkapa ni kutokuwa na utaratibu wa kuwasimamia na kuhakikisha waliouziwa viwanda ktk zoezi la ubinafsishaji wanavifufua viwanda hivyo. mkapa hajawahi kusema kwamba alikosea kubinafsisha au hakukuwa na ulazima wa kubinafsisha viwanda na mashirika ya umma.

..tumsikilize mkapa hapa chini ili kujiridhisha kuhusu alichokisema.

Unaweza kusikia wazi kwamba anajichanganya, alifanya maamuzi bila proper feasibility study. Kwanini Raisi mzima aseme alibinafsisha mashirika na viwanda bila mkakati wa kuhakikisha kuwa nia ya kubinafsisha inatekelezeka? He is simply qualified katika kulaumu na ku- critisize wengine. He was simply a failure!
 
Kuna vingine vingi tu ambavyo sisi ambao hatukuwepo enzi hizo tuliokuta masalia masalia tumeshavisahau.

Mwalimu kwa ujumla alianzisha mashirika takribani 600 (ila sio mashirika yote yalikuwa ni viwanda).
Kwenye suala la viwanda mwalimu kazishinda awamu zote nne zilizopita.

ANgalau jiwe alijitahidi kwa mbaaaaaaali
 
Back
Top Bottom